Uchaguzi 2020 Hii ndio awamu iliyofeli kuliko awamu zote zilizopita

Mkuu hii corona itatusaidia kujua hivyo vituo vya afya na zahanati vimejengwa nchi gani.mpaka sasa corona imeshatusaidia kujua kuwa serikali haina pesa,Yale tuliyokuwa tunaambiwa kwamba pesa ipo yalikuwa yanatokana tu na kiburi cha uzima
 
Alitegemea dhana ya kutawala kwa mkono wa chuma,matokeo yake imemuharibia .

Ni mambo ya muda tu,hata kule Sudan Al Bashir hakutegemea kama siku moja angekuwa mfungwa.
 
Naunga hoja
 
Awamu hii 5, wasomi ajira yao kuu ni kucheza kamali za wachina a. k. a Bonanza. Magufuli Mungu anakuona.
 
sasa shangaa poliice,tume na watanzania wengine wanavyompigania aongeze miaka 5,yaani sometime unashindwa elewa Kama hao watu ni binadamu au wanyama
Hapa wa kulaumiwa ni wazee wa dsm wakiongozwa na Mzee Ganze walikabidhi nchi kwa shetani badala ya MUNGU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii awamu ya tano imelitia aibu Taifa hili rekodi yetu ya haki za binadamu imevunjiliwa mbali kwa Watanzania kupigwa risasi hadharani na wengine kuuwawa huko Rufiji

Cha ajabu zaidi hawana nia ya kuibadili tume ya uchaguzi na wizi wa kura na upendeleo utabakia pale pale
 
Ukandamizaji ni asiri ya mwanadamu inawezekana hata wewe wapo ndugu zako unaowakandamiza kwenye familia yenu. Yawezekana una miaka kadhaa hata wazazi wako huendi kuwasalimia, itazame kasoro yako. Nimeona barabarani mwenye Lori anamdharua wa kosta, na wa kosta anamdharau wa bajaji, wa bajaji anamdharau wa pikipiki wa pikipiki anamdharau mwenda kwa miguu.
 

Binadamu asili yake ni ubinafsi sio ukandamizaji kuna tofauti ya ubinafsi na ukandamizaji


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa wa kulaumiwa ni wazee wa dsm wakiongozwa na Mzee Ganze walikabidhi nchi kwa shetani badala ya MUNGU

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtawalaum sana Ila tatizo si wao,tatizo ni wewe na Mimi,tulio wengi tunadhani Mambo ya nchi hii hayatuhusu so tumeachia kikundi cha watu wasio zidi 1000 na wafuasi wao Kama milioni 9 na ndo waamue kila kitu kinachomhusu watanzania wote milioni 55,
 
Ameanzisha mamiradi yanayoitwa WHITE ELEPHANT; ile SGR na Stiglers Gorge. Hii miradi inakula fedha nyingi, itachukua muda mrefu kukamilika na hawezi kuleta FAIDA hata ikikamilika.

Amehamishia Serikali Dodoma lakini muda wote viongozi wanaongoza wakitokea DSM. Wanakwendaga Dodoma karibu na vikao vya Bunge ili kuwatisha wabunge wa CCM kwenye party caucuss.

Awamu ya 5 imerudisha maendeleo nyuma kwa miaka 50 kama alivyosema Jenerali Ulimwengu. Tulikosea sana mwaka 2015, hasa KIKWETE kwa kumg'ang'ania BENARD MEMBE ndipo tukaangukia kwenye AJALI hii.
 
Ndio awamu pekee ambayo 1.5 trillion inaibiwa alafu poa tu hakuna maelezo Yani poa tu
 
Ajira imeshuka katika sekta binafsi na kampuni zinakufa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inabambikia wafanyabiashara kesi Leo watu wameondoa mitaji Yao imeshindwa kuiwezesha sekta binafsi Leo tenda utasikia jkt mara magereza hizo ajira zitakuja je kwenye sekta binafsi


Sent using Jamii Forums mobile app
Mara TBA, TEMESA, TANESCO.
Sasa ukiangalia hapo kampuni za ujenzi zinakufa Mana JKT na TBA wanamchukua dili , TEMESA nao wanamchukua dili , umeme ivyoivyo TANESCO wanamchukua dili. Kampuni kibao zinakufa .
Zidumu fikra za awamu ya tano kwa ubunifu didimizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…