Hii ndio hali ya Bumbuli ambayo Mbunge wake ni Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi

Ni ipi sababu ya hayo yote mkuu, hapa kwetu wananchi tunasema ni viongozi wanafuja pesa, huko kwao kima cha chini au cha juu wanacholipwa viongozi wao ni kiasi gani??

Maana hapa kwetu ukiritimba unaanzia kwenye mishahara ya viongozi na kusahau kada muhimu.
 
Kuanzia kazungula, pandamatenga, ngwasha, nata, francis town, palapye, mahalapye, Gaborone, A3 ni super road, kwakweli, Namibia kupitia katima mulilo boda, ni super. Na ni landlocked countries. Sijui tumelogwa wapi Watanzania. Dah inauma sana.

Namibia siyo landlocked, ina ufukwe wa atlantic, nimeshaogelea Swakopmund bahari ya Atlantic ila maji yake baridi sana siyo kama kwetu …
 
Watu wakiambiwa mikoa ifanye kazi kama majimbo wanakua mbogo
Huu mfumo tulio-nao ni mbovu sana na ni ngumu kuleta maendeleo
 
Nikijaaliwa ni moja ya nchi ya kutembelewa mkuu, inasifiwa sana kwa amani na maendeleo bila rushwa
Yes mkuu,ukiwa na private car ni safi zaidi,unaweza tembelea na familia au marafiki,ingilia Botswana thr kazungula OSBP,lala pale Kasane na ujionee tembo/swala/warthog mitaani (relax wana corridors zao na elewa in Botswana animals ana right of the way),next drive to Nata ,kata kulia pale nenda Maun,geuza drive to Francis Town lala pale,then to GABS thr palapye na off course ingia SA thr Mafeking then to joberg,radiation nyumbani kupitia Zimbabwe na malawi (kasumulu border),good luck...andaa kama 4000usd kwa budget ya 4 pax
 
Kwanza jimbo hilo waliunda kina makamba tu ili kutokea ubunge. Hana muda kushughulikia jimbo maana saa zote ni mipango ya upigaji na kutaka kuja kua rais.
 
Mkuu 'Vishu Mtata', binafsi nisingejali hata kidogo hawa waliopo serikalini wanalipwa vizuri sana kama kazi zao wanazozisimamia zinaleta tija kwa taifa.

Tena ningehimiza walipwe vizuri zaidi, na kwa wale wanaokwapua mali za waTanzania hata kunyongwa wanyongwe kama ushahidi usiokuwa na shaka upo.

Botswana na Namibia viongozi wao na hata wafanya kazi wanalipwa vizuri kulingana na hali zao za uchumi. Wanazo taratibu zao zinazoeleweka, siyo hizi za hapa kwetu za tozo na vikokotoo vinavyoibuliwa bila mpangilio maalum.
 
kiongozi makini hujali taifa kwa ujula

hata mwalimu hakusukumiza mandeleo butiama pekee
Na ndo maana leo butiaMa inaendelea kua kijiji ukifka butiama ni km umeenda kijijini kwenu tu utofauti ni lami na taa za barabarani
 
Uwe unatumia akili, Waziri hamiliki hazina, Wala Baraza la mawaziri halijipelekei miradi majimboni kwao kwa zamu
 
Hyo hali ni ya Nchi nzima maeneo ya vijijini..
 
Selfishness ndio hulka yetu !
Tunafikiria kujilimbikizia kwanza !!
Maendeleo baadaye !
 
Watu wakiambiwa mikoa ifanye kazi kama majimbo wanakua mbogo
Huu mfumo tulio-nao ni mbovu sana na ni ngumu kuleta maendeleo
"Majimbo" si ndiyo hayo hapo kwa jirani Kaskazini? Ufisadi na takataka zote zinazofanyika kwenye serikali kuu sasa zinazalishwa kwenye majimbo 47?

Katika kushindwa kwetu kuwajibishana kwenye hiyo serikali, sasa tunakimbilia kudhani itakuwa bora zaidi kuanzisha mfumo ule ule kwenye serikali za majimbo?
Dhana ya namna hii sijawahi kuielewa hata siku moja.
 
Kwanini umetolea mfano kenya na sio u.s.a, canada, china au australia unaakili ndogo sana

Unataka watu wawajibike kivip nawakati mkuu wa mkoa, wa wilaya na mkurugenzi ni wateule wa rais
Hawaka pale kwa ajili ya wananchi bali kwa ajili ya Rais

Ukitaka watu wawajibike wachaguliwe na wananchi
 
Kwanini umetolea mfano kenya na sio u.s.a, canada, china au australia unaakili ndogo sana
Huu mstari umeonyesha ni kiasi gani ulivyo mtupu kichwani, na mara nyingi watu wa aina yako huwa sina simile nao hata kidogo. Hii Tanzania unailinganisha na hizo nchi ulizotaja hapo wewe, au shule uliyonayo haikupi uwezo wa kujuwa umuhimu wa kulinganisha vitu vinavyo fanana?
Hata hivyo, historia ya hizo nchi unaijuwa wewe; unajuwa walikoanzia na kufika hapo walipofika?

Ngoja kwanza nitazame unajiita nani tena..., pumbavu kabisa, sipotezi tena muda na kenge kama wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…