Hii ndio hatari na tishio linalotokana na changamoto ya upumuaji

Hii ndio hatari na tishio linalotokana na changamoto ya upumuaji

U.s.a wanapima wanatoa taharifa na wanachukua tahadhali zote imesaidia Nini.
Umechagua USA, na nina uwezo wa kueleza kwa nini hawafanikiwi.

Lakini mbona hukuchagua China, kwa mfano mmoja tu!
 
Wapi nimeweka watu gizani? mimi nimehimiza elimu itolewe kutoka kwetu sisi member wa jf kupitia thd zetu,hayo ya kuhimiza watu wapimwe kwanini usihimize wewe? unataka kunipangia cha kuchangia humu?

JF is an open forums kila mtu anatoa maoni yake,ukiona una maoni tofauti ya mwenzako basi yaweke hapa hayo maoni/ushauri wako,

Hayo mambo ya kuambiana sijui kuweka watu gizani peleke huko kwenye vijiwe vyenu vya kahawa.
Kwani wajibu wa serikali ni nini?

Unaelewa wajibu ilionao serikali juu ya maisha ya raia zake?

Badala ya kutimiza wajibu huo, serikali hiyo hiyo inatishia (vyombo vya habari) wasiwaelimishe wananchi..., unakuja hapa kupiga propaganda unadhani sote ni wajinga?
 
Ata akisema aitasaidia kitu zaidi ya kuzidisha HOFU
NB: akuna mbadala wa kukwepa kifo
Mkuu last year alipokiri kuwa ipo na kuwataka wananchi kuchukua tahadhali na kufata ushauri wa wataalamu huoni kuwa corona ilishindwa kirahisi? Je alizidisha hofu au alileta suluhu? Au wew una maoni gani hapo?
 
Kwani wajibu wa serikali ni nini?

Unaelewa wajibu ilionao serikali juu ya maisha ya raia zake?

Badala ya kutimiza wajibu huo, serikali hiyo hiyo inatishia (vyombo vya habari) wasiwaelimishe wananchi..., unakuja hapa kupiga propaganda unadhani sote ni wajinga?
Huna akili wewe,kumbe unapayuka kisa ushabiki wa kisiasa? mimi sishabikii hayo mambo,
Kwahiyo watu wasielimishane kuhusu gonjwa hili? Najua kila nchi ni wajibu wa serikali but watu hawawezi kubweteka na kukaa tu ndio maana nikasema japo tutumie hii platform kuelimishana.
 
Haya mambo mimi nimejionea mwenyewe yaani sio kuambiwa, kaka alikosa mashine tukaambiwa masine iko moja na ina mtu kama tuna hela kidogo tutoe jamaa anyofolewe nilishindwa tukapambana kumuomba mungu tu wakaja kumwekea usiku saa nane asubuhi saa moja kaka yangu akafariki ....sitasahahau hii changamoto ya upumuaji imemuondoa mtu aliyekuwa nguzo kwangu
Pole mkuu, Mungu akupe uvumilivu...
 
Mmmh. Pole sana. Inaskitisha kwa kweli
 
Acheni kutishana, hakuna corona.
Kwa jinsi ninavyoijua corona haina mipaka Ba haihitaji wapigadebe na watetezi huwa inajipigia debe yenyewe kwa kuanza kuangusha vigogo na magogo hadi wenyewe watangaze nchi nzima...
 
Umsema kweli. Mimi nilikuwa nasema hata mwaka jana ule mlipuko wa kwanza walifariki watu wengi kabisa lakini kuna watu walikuwa wanabisha hapa. Huenda hata wengien wamekuja kupoteza watu wao kwa ubishi wao wa kijinga.

Tungekuwa tumekubali ukweli wa pigo la mwaka jana basi mwaka huu tungekuwa tumejifunza kitu. Badala yake mjinga mmoja akasema corona imeshaondoka kwa maombi.
Utasikia kuna ndugu yako yoyote kafariki? Binafsi nashukuru Mungu ila kuna jamaa kanusirika sio mda alikuwa anakohoa homa yaani mwili kuuma angalau alikuwa na tuhela aka hire daktari wa kumuuguza,kalala zaidi ya wiki kwa bed
 
Huwa nashangaa imekuwaje wajinga wengi namna hiyo wapate uongozi na wengine kufika mpaka kwenye ngazi za juu kabisa. Huo msemo wa ''kuna ndugu yako yoyote kafariki?'' itakuwa wamemsikia huyo baba yao anasema na wao wakakariri. Hawajui kuwa unaweza kumaliza hata miaka miwili au mitatu bila kuwa na ndugu aliyefariki kwa eg malaria lakini hii haiondoi ukweli kuwa kuna watu wengi wanafariki kwa malaria. Mbona mtu anaweza kukaa hata mwaka bila kufiwa na ndugu yoyote wa karibu? Je hii inaondoa ukweli kuna watu wengi wanakufa kila siku? Phd za kufoji zina mambo!
 
Naambiwa timu ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje aliambatana na matabibu kutoka China waliomchanja Jiwe, na wote wa karibu naye.

Kama corona siyo hatari, kwa nini uji wa Madagascar, wao ndio wawe wa kwanza kuunywa? Chanjo ya China, wao wawe wa kwanza kuchanjwa? Uongozi wa kinafiki kiasi hiki upo kwetu tu. Kiongozi anawaambia watu wake chanjo mbaya halafu yeye anaenda kuchanjwa!!
 
Bado hujagombania hewa ya oksijeni, lakini kuna siku zinakuja hao watu wa ughaibuni unaowaona ndio wameendelea ndio watakaosababisha dunia kukosa hewa baada ya kuanzisha vita kwa vsingizio vya kitoto sijui hapo utamlaumu nani.

Upenyo unaojaribu kuupenyeza kupitia matokeo hasi ya ugonjwa wa UVIKO kwa sababu za kisiasa

Hebu panua ubongo wako kwa kumsikiliza mtumishi wa Mungu kutokana ufunuo wa maono ya ulimwengu ujao:
 
Points ni zire zire
Barakoa, mazoezi, lishe bora na chanjo.
Mimi nadhani ni vizuri zaidi kama watu wakajikita katika kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na gonjwa hili kuliko kutangaza vifo vya watu wa familia zingine, sijasema kutangaza vifo vya familia zingine haifai au inafaa ila elimu ya kujikinga na gonjwa hili ni muhimu zaidi.

Kama inawezekaza basi Mods wangeweka thd ya namna hiyo kama sticky thd.
 
Unaambiwa pale makumbusho eneo la kuchomea marehemu mabohora pamezidiwa na foleni ni ndefu mno .
Mi sijui itakuwaje mkuu.
Naambiwa hii corona ya sa hivi ni airborne imekuja kwa jina la pneumonia au tatizo la upumuaji,dah Mungu atusaidie kwa kweli,
Yani itafika wakaati barakoa itavaliwa 24hrs.
 
Tatizo watu wabishi upo kwenye daladala unakutana na mstaafu unamuuliza unaenda wapi? Eti Kariakoo kununua vitenge au Posta kufanya dili, miaka 60 hakuliona sasa akipigwa vivid tumemsahau
Taratibu ni zile zile Mkuu.

1. Kuvaa barakoa
2.Kutumia "SANTAIZA".
3.Kunawa Mikono na maji tiririka na sabuni.
4.Social Distancing.
5.Kama hakuna ulazima wa kutoka basi ni bora utulie nyumbani.
6.Kufanya Mazoezi.
7.Kula vyakula vya kuongeza kinga za mwili.
 
Huwa nashangaa imekuwaje wajinga wengi namna hiyo wapate uongozi na wengine kufika mpaka kwenye ngazi za juu kabisa. Huo msemo wa ''kuna ndugu yako yoyote kafariki?'' itakuwa wamemsikia huyo baba yao anasema na wao wakakariri. Hawajui kuwa unaweza kumaliza hata miaka miwili au mitatu bila kuwa na ndugu aliyefariki kwa eg malaria lakini hii haiondoi ukweli kuwa kuna watu wengi wanafariki kwa malaria. Mbona mtu anaweza kukaa hata mwaka bila kufiwa na ndugu yoyote wa karibu? Je hii inaondoa ukweli kuna watu wengi wanakufa kila siku? Phd za kufoji zina mambo!

Acha tu huwa nachukia sana wanaosemaga hivyo wakati ulioandika ndio ukweli wenyewe.
 
Mimi nadhani ni vizuri zaidi kama watu wakajikita katika kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na gonjwa hili kuliko kutangaza vifo vya watu wa familia zingine, sijasema kutangaza vifo vya familia zingine haifai au inafaa ila elimu ya kujikinga na gonjwa hili ni muhimu zaidi.

Kama inawezekaza basi Mods wangeweka thd ya namna hiyo kama sticky thd.
Hiyo ni kazi ya serikali ambayo ilitakiwa ifanywe na Dr. Gwajima na team yake. Sasa badala ya kufanya hivyo wao wamebakia kusifia nini Rais amesema au ameamua kama nchi tufanye .... Mask, hand sanitation na social distancing bado ni njia bora na pekee zinazojulikana kupunguza maambukizi. Mpaka sasa wamekaa kimya kuhusu hayo!! Watu wajue kuwa hizo Malimao, tangawizi na vitunguu saumu peke yake haviwezi kusaidia.
 
Back
Top Bottom