Hii ndio hatari na tishio linalotokana na changamoto ya upumuaji

Hii ndio hatari na tishio linalotokana na changamoto ya upumuaji

The only thing that will save lives from this disease is to stick our asses at home. But the problem comes Black asses are not adhesive at all!
Umemaanisha "Adherent?" Au obeisant au compliant? Adhesive sio correct English kabisa mkuu. Kwa kweli English ya JF inaniachaga hoi sana 😂😂😂
 
Kule italy,,kuna padri alikuwa kwenye ventilator,,akamwona kijana mmoja kaletwa yuko hoi,amekosa ventilator,,padri ilibii aombe wamtoe kwenye mashine,wamwekee kijana,,juu yeye ameshaishi miaka mingi,akaona bora kijana apate fighting chance kuliko kumuacha afe angali bado mdogo,
Padri akafa
Duh..🙏🙏
 
Corona yenyewe ina tendency ya kupandisha sukari mwilini hata kama hauna sukari...
Corona yenyewe ikipandisha hiyo sukari na BP inakuwa imerahisishia wakuda kutoa sababu ya kifo. Changamoto ya upumuaji. Hata KM anajua. Huyu naona ni Mfaransa. Huko, mwalimu wa chekechea tunayemuita ticha, anaitwa le/la professor! Nimemkumbuka bure Prof. Jay wa Mitulinga.
 
Serikali inayokaa kimya watu wakiangamia inakosa utu. Kwa sasa baba anaweza kurudi nyumbani na ugonjwa akitokea safari ya mbali lakini kwa vile hakuna anayepima huyo naye anasambaza kwa familia nzima. Tukio la Profesa wa SUA mmeliona jinsi familia ilivyoteketea kwa Kutojua nani anao.
Mwaka Jana Waziri Majaliwa alizindua kampeni ya kupima Ukimwi wenye nao wajijue waweze kuwakinga wasio nao.
Leo upimaji corona unazuiwa ili asijulikane nani anao nani hana, kama siyo njama za kutaka watu wafe kwa wingi ni nini?
Wanawalipisha wapimwaji na hivyo wanaopimwa ni wale tu wanaosafiri na kwa uchache wanaoingia nchini na sababu kuu ni watalii.Tunaangamiza watu wetu kwa kuwavutia watalii waje Tanzania kwa kuwa hakuna Corona.Hili janga la COVID tunalichukulia kuwa linaangamiza wengine na siyo sisi.Utadhani tupo kisiwani au tuna maumbile tofauti na wanadamu wenzetu.Tumeumbiwa natural immunity ambayo wenzetu hawana?
Nyerere aliwahi kusema ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne ambavyo ni Ardhi,Watu,Siasa safi na Uongozi bora.Jiulize tunakwama wapi?Ukiona hivyo tunavyovikosa tunaweza kuendelea?
 
Umeandika kwa uchungu sana !
Uchungu nilio nao unatokana na jinsi tunavyopoteza raslimali watu na fedha kuwahudumia wanaofahamika kama walio na matatizo ya kupumua.Tunazika karibu Kila Siku wapendwa wetu lakini hakuna anayethubutu kukiri ukweli.
Tunapelekwa kichinjio tukiimbiwa mapambio ya matumaini na kuambiwa tupo salama.
 
Na matamasha taking koff yanaendelea kama kawaida
Nilisema humu haya matamasha vijana wanazoa Corona wanaenda kuuwa wazazi wao. leo Chege Kigunda Mama yake kafa, yule meneja wa Wema Martin Kadinda naye Mama yake kafa, mtangazaji wa Wasafi sijui nani naye Mama yake chali. Wote hawa wanazoa Corona kwenye Matigo tumewasha wanaenda kuuwa wazazi wao. Why serikali ISIPIGE marufuku haya matamasha uchwara
 
Nyungu na ule uji wa NIMRI ni upumbavu mtupu. Hakuna mwenye acute Covid 19 anayeweza kusaidiwa na hizo takataka.

Kama unataka kumwahisha mgonjwa wako kaburini, mpige nyungu.
Najitambua sana kiongozi,nipo against nyungu kwa sababu haina scientific evidence kuwa inatibu.Hakuna formula yoyote ya nyungu inayofahamika/documented anywhere in the world.

Napinga unywaji wa pilipili kichaa,limao,tangawizi na vinginevyo vingi maana hakuna data za uhakiki wa ufanisi wake popote.

Watanzania tusiposema hapana kwa propaganda za kisiasa na kushika maelekezo ya WHO tunamalizika.
 
Mimi nalia na wahudumu wetu wa afya, hawana vifaa kinga vya kutosha, wanafanya kazi kama wamejitolea liwalo na liwe, Vifaa tiba walivyonavyo ni mask tu navyo sidhani kama wote wanapata.
Mask za vitenge Nazi wajitafutie,hakuna Gloves wala PPE zingine katika vitu vingi ukiachilia mbali wimbo wa uhaba wa dawa.
Nakumbuka Airbus ilivyoenda Madagascar ikiwa na Mh. Kabudi, wakatuletea Juice wakanywa na box zote zikapelekwa. Alihujumu uchumi?Zipo wapi zile dawa? Watapewa wagonjwa wa Corona itakapoingia Nchini?
 
Kama korona inasababisha microthrombi ambazo kwenye mapafu zinaziba vile vimishipa vidogo vya damu ambavyo vinahusika pia na gaseous exchange.

Nilitarajia quick improvement kama wagonjwa watapewa anticoagulant drugs, mfano Aspirin kuliko kuwaweka kwenye ventilator pekee.
 
Hivi wagonjwa wa Pressure na Kisukari zamani walikuwa wanakufaje? Hizi shida za kupumua zilikuwa haziwakumbi? Mbona tulikuwa hatusikii mialiko kama sasa hivi?
 
Haya mambo mimi nimejionea mwenyewe yaani sio kuambiwa, kaka alikosa mashine tukaambiwa masine iko moja na ina mtu kama tuna hela kidogo tutoe jamaa anyofolewe nilishindwa tukapambana kumuomba mungu tu wakaja kumwekea usiku saa nane asubuhi saa moja kaka yangu akafariki ....sitasahahau hii changamoto ya upumuaji imemuondoa mtu aliyekuwa nguzo kwangu
Ni kwa sababu ya watu wenye akili kama punda ndiyo maana tumefika hapa. Nchi ilitakiwa ijitayarishe kwa kuongeza huduma za oxygen tangu mapema. Pole sana kwa msiba.
 
Back
Top Bottom