rommy shabby
JF-Expert Member
- Jun 26, 2017
- 1,123
- 1,302
Yupo kwenye wimbo wa feruz wema wangu umeniponza, alikuwa anapiga guitarNdio babu yake Dully Sykes?
Naona babu brazameni kavaa hereni na kanyoa kiduku.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yupo kwenye wimbo wa feruz wema wangu umeniponza, alikuwa anapiga guitarNdio babu yake Dully Sykes?
Naona babu brazameni kavaa hereni na kanyoa kiduku.
HII NDIO HISTORIA YA FAMILIA YA SYKES.
Historia hii inaanzia kwa MZEE SYKES MBUWANE KLEIST. Huyu ndiye baba yake KLEIST SYKES.
MZEE SYKES MBUWANE KLEIST ni nani?
Sykes Mbuwane ni mamluki wa KIZULU aliyechukuliwa yeye na vijana wenzake wa kizulu kutoka kijiji cha LIKUNYI MSUMBIJI.
Walifikaje Tanganyika?
Kipindi cha UTAWALA wa kikoloni wa kijerumani chini ya HERMANN VON WISSMAN aliwachukuwa kwa meli ya kivita kama askari mamluki mpaka Pangani Tanga, Tanganyika kuja kupigana na ABUSHIRI BIN SALIM AL HARITH NA MTWA MKWAWA WA IRINGA.
KLEIST SYKES ALIZALIWA WAPI?
KLEIST SYKES alizaliwa mwaka 1894, Pangani Tanga kwa baba yake SYKES MBUWANE KLEIST na MAMA yake ni Mnyatulu, baada ya baba yake kufariki Kleist Sykes baadae alikuja Dar es salaam.
MAISHA YA KLEIST SYKES BAADA YA KUJA DAR.
KLEIST SYKES alimuoa Bi MLUGURU BINT MUSSA, na alibahatika kupata watoto watatu wa kiume.
(1) ABDULWAHEED KLEIST SYKES. (1924__1968).
(2) ALLY KLEIST SYKES. (1926__2013).
(3) ABBAS KLEIST SYKES. (1929__2021).
Kama inavyoonekana katika Picha namba (1). Waliosimama kutoka kulia ni Abdulwaheed Kleist Sykes, na Ally Kleist Sykes. Aliyekaa kutoka kulia ni Abbas Kleist Sykes na Baba yao mzazi Mzee Kleist Sykes.
Picha hii ilipigwa 1942, kipindi Abdulwaheed Kleist Sykes alipokuja kumuaga baba yake akitokea LOWER KABETE KENYA mafunzoni kabla ya kwenda BURMA kama Askari wa KAR BURMA INFANTRY. Na picha namba 2, ni MZEE ALLY KLEIST SYKES kipindi cha uhai wake.
Vile vile MZEE KLEIST SYKES ALIKUWA NA WAJUKUU.
Wafuatao ni baadhi ya wajukuu wake:
(1) EBRAHIM (EBBY) ABDULWAHEED KLEIST SYKES. 1952__2015). Kama anavyoonekana katika picha namba 3. Huyu ndiye Baba yake mzazi DULL SYKES msanii wa bongofleva.
(2) MUSSA ABBAS KLEIST SYKES.
(3) KLEIST ABDULWAHEED SYKES. Alifariki 22 novemba 2017.
(4) ABRAHAM ALLY KLEIST SYKES.
ASANTENI:
View attachment 2657367View attachment 2657369View attachment 2657370
Afro...Anhaa kumbe wewe ndiye unaefaidika.
Wewe unapata faida ya kuuza vitabu na hayo madili.
ila sisi jamii ya watanzania hautusaidii chochote,unatupotezea tu muda. Usitake kutuektia hapa eti hizo historia zina umuhimu sana kwetu ili utuuzie hivyo vitabu..Wewe ni kama dalali au tapeli fulan.
Unaongea maneno mengi ila hauoneshi faida ya unachokifanya kwenye jamii.Afro...
Ikiwa unaona naandika vitabu na makala zisizo na manufaa kwako ucha kuzisoma usipoteze muda wako.
Lakini isemee nafsi yako kwani mimi napendwa na wengi katika ukumbi huu.
Mimi ni mwandishi sihusiki na uuzajiji wa vitabu.
Na uandishi ni usomi si biashara.
Sijui ni nini kimekughadhibisha hadi unanitolea matusi.
Jamii ya Tanzania wananufaika na kalamu yangu.
Nimehusishwa katika uandishi wa kitabu cha maisha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ("Nyerere Biograph.")
Maalim, nimewahi kuwasikia wawili kati ya hao uliowataja, naona tatizo halikuwa jina bali asili ya hao akina Sykes, Nyerere alimtenga pia Kambona kwa kuwa na asili ya Malawi.Jabulani,
Umepata kuwasikia akina Manning, Humplink, Taylor, Frisch, Schneider, Lee kwa kuwataja wacgache?
Eti kwa nini hilo jina lao la ukoo sio la kibantu, SykesAfro...
Mimi ndiye nilyeieleza historia ya ukoo wa Sykes kwa kuandika kitabu cha maisha yao Tanganyika kwa kutumia nyaraka zao zinazokwenda nyuma kuanzia miaka ya mwanzoni karne ya ishirini.
Hizi nyaraka zipo na wamenimefungulia nikazisoma zote.
Hizi ni nyaraka za Kleist Sykes Mbuwane alizotumia kuandika kitabu cha maisha yake.
Kwa simulizi alizopokea kwa wazee wake ambao ndiyo mamluki wenyewe walioingia Tanganyika wakiongozana na Hermann von Wissmann historia ya ukoo wao inaanza na Chaka alipoanza vita kutokea Kwa Bulawayo mwaka 1828 akiteka majirani zake.
Katika kukimbia vita hivi Ukoo wa Sykes wakahamia Kwa Likunyi, Imhambane ambayo sasa ni Mozambique.
Hapo ndipo walipochukuliwa na Wissmann kuja kuwasaidia Wajerumani kuituliza Germany Ostafrika.
Wazulu waliwashinda Bushiri bin Salim Al Harith na rafiki yake Mtwa Abdallah Mkwawa.
Yapo mengi vipi ukoo huu ukaja kuwa mashuhuri hata wakaasisi African Association 1929, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 na TANU 1954.
Sasa hakika historia hii ilikuwa haijulikani na zilifanyika juhudi kubwa kuwafuta katika historia ya kuasisi African Association na TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Wanaogopa kutumia jina la ukoo Mbuwane wataonekana sio wazawa, ila itoshe tu kusema kwamba tuwatambue kama waswahili, ambao ni mchanganyiko wa makabila na mataifa mbalimbaliEti kwa nini hilo jina lao la ukoo sio la kibantu, Sykes
Afro...Unaongea maneno mengi ila hauoneshi faida ya unachokifanya kwenye jamii.
Au kupendwa na watu ndio faida?
Huo ni unini tuite? Unge heshimu alicho leta mbona ni jambo jema kujua historia.Tukishajua then what?
I think kuna vitu vya maana zaidi kufocus kwa sasa
Johnny....Eti kwa nini hilo jina lao la ukoo sio la kibantu, Sykes
Mzee...Huo ni unini tuite? Unge heshimu alicho leta mbona ni jambo jema kujua historia.
Achana na historia hizi zinaweza kutwistiwa ili kufit narrative na malengo ya wanayoisimulia.Huo ni unini tuite? Unge heshimu alicho leta mbona ni jambo jema kujua historia.
Jabulani,Wanaogopa kutumia jina la ukoo Mbuwane wataonekana sio wazawa, ila itoshe tu kusema kwamba tuwatambue kama waswahili, ambao ni mchanganyiko wa makabila na mataifa mbalimbali
Afro...Achana na historia hizi zinaweza kutwistiwa ili kufit narrative na malengo ya wanayoisimulia.
Muda tunaoishi ni sasa.
Muda unaomatter ni sasa.
Muda wa kufanya mabadiliko ni sasa.
Jabulani,Kuhusu Taylor na Frisch naomba utujuze japo machache
Kinyungu,Kama Mohamed Said hajachangia huu uzi ni batili
Hii kwamba Nyerere alipokelewa na Abdul Sykes na akaikuta TANU, hapa umeamua kutumia kalamu yako vibaya kupindisha ukweli sababu ya chuki zako binafsi dhidi ya Nyerere. Unajipa kazi ngumu ambayo huwezi kubadili ukweli.Mzee...
Kuna watu wamekasirishwa na mimi kusahihisha historia ya uhuru.
Historia ilikuwa inaeleza kuwa TANU iliundwa na Julius Nyerere.
Nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes na kueleza kuwa Mwalimu alipokelewa na Abdul Sykes na akaikuta TANU kwa Abdul Sykes hawakupendezewa.
Ikawa historia hii imewaudhi.
Sidhani kama ilikuwa inawezekana Wajerumani kuchukua askari kutoka koloni la Wareno Msumbiji au babu yako mmanyema kutoka koloni la wabelgiji kuja kuwasaidia kupigana Tanganyika , wakati kwenye hayo makoloni napo kulikuwa na vurugu. Kuna changa la macho unatupiga hapa.HII NDIO HISTORIA YA FAMILIA YA SYKES.