Hii familia, licha ya kuwa wanastahili sana kutambuliwa kwenye historia ya nchi hii, lakini I don't see any thing noble in them kama ambavyo wanahistoria kama
Mohamed Said wanataka kutuaminisha. Ukifuatilia historia yao, walikuwa ni Opportunists sana, na pengine haya malalamiko ya kutengwa anayoyadai MS, ni kama Karma.
Mzee Sykes miaka ya 1800-1900 mwenyewe alikuwa ni Mamluki wa Kijerumani, ameshiriki vita za kijerumani zilizoua watanganyika na kusimika utawala wa kijerumani. Tena amepigana dhidi ya hao wanaodaiwa kuwa ni waislam—kina Bushiri. Miaka
Kleist Sykes miaka ya 1914-1918, kama baba, yake amewapigania pia Wakoloni wa Kijerumani wakati wa vita ya kwanza ya dunia.
Watoto wa Kleist, yaani Abdul na Ally wamempigania mkoloni muingereza 1940s huko Burma.
Huyo Ally Sykes, alipotoka kumpigani Muingereza, akarudi direct Kenya kuendeleza kumfanyia kazi mkoloni ya kudhulmu ardhi wakenya kupitia kampuni ya Peter Colmore.
Kwa kweli hawa watu, kabla ya kudai kuwa Nyerere aliwatupa, waanze kwanza kuomba radhi Watanganyika na wakenya kwa kusimika ukoloni na kudhulumu ardhi.