Ni lazima Historia iwepo, so hata asingebakia yeye, ni lazima historia ingekuwepo kwa mwingine. Nachosema imekuwa na manufaa makubwa kwa nchi historia hii kuwa ilivyo kuliko namna ambavyo Wanahistoria wa mrengo wa kiislam kama
Mohamed Said wanavyotaka historia ya nchi hii kuipaka rangi ya uislam, wakati ukweli ni kuwa waislam na wakristo wote wamepigania uhuru—HATARI.
Life...
Nimeandika kitabu kizima kueleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hakuna aliyenipinga toka kitabu kitoke 1998.
Soma hapo chini:
Saku Kondo Saku Kondo,
Prof. Haroub Othman akimpenda sana Mwalimu.
Hili likijulikana na wengi.
Lakini alipomaliza kukisoma kitabu cha Abdul Sykes alitoka na mshtuko mkubwa kwa yale aliyokutananayo.
Prof. Haroub akazungumza na mimi na akanieleza kuwa amemuomba Mwalimu aandike historia ya maisha yake ili na yeye asikike.
Akamwambia Mwalimu kuwa kitabu cha Abdul Sykes kimebadilisha historia yake Nyerere mwenyewe na historia nzima ya jinsi uhuru wa Tanganyika ulivyopatikana na akamfahamisha kuwa "legacy" yake yote sasa si kama ilivyokuwa ikiaminika kuwa.
Kitabu kimebadili mambo mengi sana.
Prof. Haroub akamwongezea kuwa halikadhalika kitabu cha Sheikh Ali Muhsin Barwani, "Conflict and Harmony in Zanzibar," (1979), kimeeleza mengi kuhusu yeye ambayo hayakuwa yakifahamika.
Hapakupatapo kutokea katika maisha ya Nyerere kukabiliana na hali kama ile ya yeye kutiliwa shaka katika sifa zake na khasa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Historia ya Baba wa Taifa ilikuwa imeingia dosari kubwa kutokana na vitabu hivi viwili na anaeweza kuiondoa dosari ile kama itawezekana ni yeye mwenyewe kwa kauli yake.
Hili halikufanyika hadi Mwalimu anafariki mwaka wa 1999.
Waingereza wanasema "the rest is history."
Hali ikoje hivi sasa?
Kitabu cha Abdul Sykes kikafanyiwa "review" katika Cambridge Journal of African History na mabingwa wa Historia ya Afrika: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan (1989).
Kleist Sykes na wanawe Abdul, Ally na Abbas wakatiwa katika Dictionary of African Biography (2011) wakiandikwa kama wazalendo wapigania uhuru wa Tanganyika.
Katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika serikali ya Tanzania ikawapa Abdul na Ally Sykes Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa kutambua mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hawa ni watu ambao walikuwa karibu sana na Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru na watu ambao Nyerere alikataa kuwatambua hadi anaingia kaburini.
Kitu gani kilisababisha hali hii?
Hakika Saku umesema kweli hakuna kama Mwalimu katika historia ya Afrika.
Mwalimu alisahau ni kituo gani alipanda basi la safari yake.
Mwalimu hakutegemea kuwa itaandikwa historia ya maisha yake katika uhai wake na ukweli wa kila kitu utafahamika.
Nahitimisha kwa kusema kuwa nimeondoa katika kitabu cha Abdul Sykes sura niliyoipa jina, "Kinyang'anyiro Cha Nyaraka za TAA na TANU."
Hii sura inaeleza mvutano uliotokea katika miaka ya 1970 baina ya Mwalimu Nyerere Rais wa TANU na Ally Sykes juu ya nani mwenye haki ya kutunza baadhi ya Nyaraka za TANU za wakati wa kupigania uhuru.
Mwalimu aliomba nyaraka zote za TAA na TANU zilizokuwa mikononi mwa Sykes zikabidhiwe kwake.
Ally Sykes alikataa kwa madai kuwa nyaraka zile zilikuwa za marehemu kaka yake Abdul Sykes.
Yako mengi yalifuatia baada ya mkwamo huu.