Tetesi: Hii ndio kazi inayofuata atakayopewa Makonda na Rais Magufuli

Mimi nawe tupo kundi moja mkuu
 
Umemjibu vizuri, jitu na akili linamshabikia Makonda, for what good has he done and even if so, under what situation! Muogope mtu anayejikomba ili apate cheo. Aliyoyafanya kwa Warioba yanatosha to disqualify him in every aspect!
Huwa simpendi huyo kiumbe
 
Mimi ningwshauri Kama Rais amelazimika sana Kumpa Kitu huyu Kunguni, Basi ampe Ukuu wa Mkoa wa Dodoma, Akimpa Dar, Navyomjua Huko Mitaani Watu wasiomjua Magufuri wakimwona Makonda watadhani Ndiye Rais. Mtu Ukuu wa Mkoa tu anazunguka na Mpolisi Kila Mahali Akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar si Ndio atazunguka na Majeshi ya Anga, Wanamaji, FFU Zimamoto na Bila Kusahau Mgambo. Si Mnajua Anavyojifanya! eh Kweli Tulivyokuwa shule ya Msingi tulikuwa tunasema, anavyojitia-tia
 
Namuomba mungu nisikutane naye viwanja
 
Makonda ni kiongozi mzuri sana wa mazingira ya sasa hana yale mambo ya mazoea anaamini ukweli hata kama ni kigogo mzee amuleta figisu figisu anapewa vipande vyake....makonda,zitto,kafulila wako vizuri sana.makonda anakela kitu kimoja tu kuwa shabiki wa ccm kupindukia.cha msingi awe kama rais wetu ni mwanaccm ila siyo shabiki wa ccm
 
CV yake ipi?
Haya anayoyafanya Dar ndio CV yake ya kisiasa!
Au unataka kuona achievements za darasani ndio u judge uwezo wake wa kisiasa?
Nadhani hiyo issue ya academic haina maana sana kwa sasa!
Si kila kitu kinaweza kufanywa kwa CV za mwonekano vingine vinahitaji taalum. Tunaomba taaluma ya mteule huyu wa rais kama mnayo.
 
Mkuu wa mkoa wa arusha au kilimanjaro


Ingawaje Rais Magufuli ameonesha hadharani kuwa ameridhishwa na utendaji wa DC wa Kinondoni Makonda hakutamka kuwa Makonda atakuwa Mkuu wa Mkoa katika hao atakaowateua bali alisema kuwa ""alijihakikishia nafasi katika serkali yake na hata angepandishwa cheo watu wasijewakaona ajabu".

Tamko la Rais halikusema kwa uhakika [ definetive] kuwa atakuwa mkuu wa mkoa !! Rais kumpamdisha Makonda kuwa mkuu wa mkoa upesi upesi namna hiyo hata bado hajapata uzoefu wa kuongoza wilaya sio kumpendelea bali ni kumpa adhabu kwani ukuu wa mkoa ni kazi inayohitaji ukomavu na utulivu ambao huyu kijana hana na hivyo atapata taabu sana katika kazi yake. Kama ameonesha potential ya kuwa kiongozi mzuri Magufuli amuache kwanza akomae kidogo ili apate uzoefu na hapo baadae akipanda hata yeye mwenyewe atafurahia kazi yake, kwani tumeona wakuu wa mikoa wengi ambao walizawadiwa hizo nafasi wakipata taabu kuongoza mikoa yao ukifananisha na wale wenye experience!! Ni ushauri tu msijekuanza kusema ni wivu la hasha.
 
Mzuri kwa kumpiga warioba. Watanzania wepesi wa kusahau.
 
Kwasababu ni kazi za kupeana tu ampe cheo chochote hata ukatibu mkuu kiongozi
 
Kwasababu ni kazi za kupeana tu ampe cheo chochote hata ukatibu mkuu kiongozi
Huenda akapewa Ubunge na kuwa naibu Waziri wa mambo ya ndani ili aweze kutumika kuwakomoa wapinzani kama wafanyavyo Uganda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…