Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Mufindi kuna viwanda vya Mbao,Pareto, Chai......mchina amejaa tele kwenye mbao saizi pale
Kweli kabisa sasa hivi mufindi Kuna viwanda vingi vya mchina kwa vijana wanaotafuta maisha bila kujali ugumu wa kazi njoo mufindi hakika hautojuta
 
tunduru inaizidi Arusha, hebu acheni uchawi basi, mlogage kwengine
 
Wewe unajua kuchambua data na wawekezaji wote wana sifa hii. Sio wengine wanafyatuka na mitaji kwenda kujilipua
 
Kutoka mjini kwenda wapi wewe mbususu..Njombe to Makambako ni km 80 hizo km 100 ni kuelekea wapi wakati unajua Mji unazungukwa na Halmashauri za Vijijini

Visingizio kibao wakati unajua fika kwamba Makambako ni kijiji kikubwa ndio kwanza kinaanza kutambaa
 
Uzi wa maana sana kwa wenye kujua ya maana. Kudos mkuu.

Wenye kutu ya SIASA vichwani mwao huu uzi hutakuwa na msaada kwao...sana sana wataishia kuuharibu tu.
Inasaidia hata serikali yenyewe kujua wapi iongeze nguvu kuibua na kusaidia maeneo maskini huku iliyapromote haya yenye unafuu
 
Mimi mwenyew nashangaa.
Hadi wilaya ya misenyi yenye viwanda kama kagera sugar,kilimo cha vanilla,mpaka wa mutukula na Ranchi kibao inazidiwa na wilaya ya muleba iliyojaa migomba na kahawa
Hiyo migomba na Kahawa ndio vinagusa raia mmja mmja directly kuliko manamba na vibarua wa viwandani mnaowalipa 130,000 per month
 
Kweli kabisa sasa hivi mufindi Kuna viwanda vingi vya mchina kwa vijana wanaotafuta maisha bila kujali ugumu wa kazi njoo mufindi hakika hautojuta
Yeah niliona hapo nilikuwepo kama week hivi
 
TUNAPOPIKA DATA TUWE TUNATUMIA UBONGO SIO MAKALIO.
HIVI DODOMA INAWEZA KUIZIDI MWANZA AU ARUSHA KWA MAPATO???
Pole mkuu ,upike kusaidia nini labda au umesoma mada na attachment yake?

Kubali tuu mkuu kutangulia sio kufika huo ndio ukweli wenyewe na bado mtalia sana
 
Kigoma Ujiji Mc na Kyela dc wanakwama wapi wote wana maziwa makubwa ya uvuvi, wote wanalima mawese na mazao mengine ya kibiashara, wote pia wana advantage kubwa ya kuwa mpakani kabisa na nchi jirani, shida inakuwa wapi
Sijui shida iko wapi hasa Kigoma japo kwa Kigoma inaonekana kuna urasimu Sana unawekwa na Serikali kufanya biashara na DRC huwa naona wafanyabiashara wanalalamika Sana.

Mji na mkoa kama Kigoma ilifaa wawe wanachangia Sana mapato nchi hii
 
Ni kweli ukizigawa moja moja Dom inazipita vizuri tuu,nakumbuka ule mwaka juzi Dom waliuza Sana viwanja wakapiga bil.73 ndio iliongoza kwa Halmashauri moja moja watu wakapagawa.

Dom unakuja Kazi Sana na viwanda vinajengwa Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…