Hii picha inaongea mengi kuhusu Africa.
Ina maana zaidi ya mia moja.
Kila msomaji wa hii picha anaipa maelezo yake kulingana na mazingira na ufahamu wake.
View attachment 2767847
Angalia picha ambazo hunipa
tumaini jipya kuhusu Africa.👇
Hiki ni kilimo Cha future.
No greenhouse no irrigation
No fertilizer no trecta non of bullshits you ever known.
Inaitwa syntropic farming
Hapa kilimo Cha umwagiliaji bila maji.
Migomba hutumika kama matenki ya maji ( Kwa kuitandaza shambani) , Mikaratusi hutumika kama mbolea.
Mavuno ni miezi miwili baada ya kupanda na forever unavuna
Mazingira ya mkulima ni rafiki Sababu kivuli ni Cha kutosha.
Gharama kubwa huwa ni mwanzo kwani inahitaji mbegu aina nyingi na idadi kubwa na vyote unapanda mara Moja na kuvuna forever.
Elimu ya kujua mimea ni lazima pia.
Panda mimea yote kuanzia na inayotambaa(tembele,viazi)vichaka ( mbaazi) matunda, mbao(Mikaratusi/eucalyptus)mwavuli(Nazi)penda kivuli (ndizi,kahawa,) biashara (korosho)
Vyote Kwa pamoja wewe ni kuvuna mpaka wajukuu.
Jembe halitumiki sana au Kwa nadra ,
Hapa panga TU linatosha au chainsaw na mashine ya kufyeka,kama una hekari nyingi.
Hiki ni kilimo Cha kuona mbali miaka 20 mbele ( mbao,mkaa n.k )unavuna TU.
Kanuni zake:
1. Panda Kwa mistari
2. Mistari ielekee North to South
3. Funika ardhi muda wote kama hakuna zao basi nyasi/mulch/majani
Ardhi wazi ni kama kidonda
4. Lima udongo SI Mazao.
Ardhi Bora Mazao Bora
6. Kuna mimea mingi inavyowezekana
7. Pruni miti na mimea baadhi ni kuongeza speed ya ukuzaji wa mimea jirani
8. Hakuna mbolea kutoka nnje ya shamba
9. Migomba na Mikaratusi ni King na Queen,visikose shambani.
10. Usiwe mtumwa wa Shamba
Mwanzilishi Ernst Gotsch ni mswiss anayefanya kilimo hiki Brazil baada ya kupewa heka kama 300 za jangwa na kuzibadilisha kuwa sehemu ambayo the cocoa duniani inatoka bila mbolea ya chumvi au dawa ya wadudu.
Hiki ni techniques ni Bado mpya hata Europe ndio kwanza inangia ila Kenya Kuna wakulima wameanza na hata wa5 hawafiki.