Tetesi: Hii ndio sababu ya kiroho kwanini watu wanaookota chupa za plastiki wengi huwa wanaishia kuwa wendawazimu

Hamna kitu kama hicho.....hayo makopo yanapopelekwa huko viwandani kwa tani za kutosha...si wafanyakazi na wamiliki wangeishaisha kabisa kwa kugeuka vichaa
..
Tuheshimu kazi za watu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Watafutie neno stahiki, Ujasiriamali linamaana bora kuliko hii uliyotumia wewe. Mjasiriamali anaishia kuwa mwehu??????? du
 
The same old question. Nikikujibu roho ni nini utaniomba reference Nami nitakwambia nimeitoa kwenye kamusi then utaniuliza " kamusi " nini? So it will be like a child play.

# Ur so predictable

# Ngoja nikae kimya
Hujajibu swali langu, na hapo hapo umenitungia maswali zaidi.

Roho ni nini?

Unaweza kuthibitisha ipo na si hadithi ya uongo ya kutungwa na watu tu?
 
[emoji1787][emoji1787] Kwenye ubora wako babu yangu Kiranga
Watu wanapenda sana kurukia ghorofa ya kumi wakati hata msingi hawajatueleza ukoje.

Katika majadiliano ya watu wanaojali mambo kwa kina, kabla ya kujadili kuhusu roho, inabidi kuweka definition.

Kwa sababu, kwa mfano, katika Kiingereza, neno "spirit" linaweza kumaanisha roho, na neno hilo hilo linaweza kumaanisha kinywaji kikali cha pombe.

Sasa, ukiniambia spirit ni kinywaji kikali cha pombe, siwezi kukubishia kipo.

Lakini ukiniambia spirit ni roho, hapo itabidi tuelezane zaidi.

Ndiyo maana nikauliza, kabla ya kwenda zaidi kimepanda kimeshuka...

Roho ni nini? Naweza kuthibitishiwa kwamba roho ipo na si hadithi za uongo za watu tu?

Mpaka sasa sijaona jibu.
 
Roho ni umbile la pekee lisiloonekana ambalo linasadikiwa kuwemo pamoja na mwili katika binadamu

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hapo utaniuliza babu yangu binadamu ni niniii unawea kuthibitisha sio kuambiwa na watu [emoji125][emoji125]
 
Roho ni umbile la pekee lisiloonekana ambalo linasadikiwa kuwemo pamoja na mwili katika binadamu

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hapo utaniuliza babu yangu utaniuliza binadamu ni niniii unawea kuthibitisha sio kuambiwa na watu [emoji125][emoji125]
Ukinitungia swali nitakalouliza hapo nakuja kama Magu nakwambia "Mimi sipangiwi".

Hata kama nilitaka kuuliza hilo nabadili.

But on the real, jokes aside, hilo la binadamu, licha ya kuwa ni uzushi mtupu (hakuna binadamu) sitakuuliza hilo, maana hilo linaweza kuanzisha thread nyingine.

Sasa umesema roho haionekani, katika kujaribu kujibu roho ni nini.

Lakini hujajibu swali langu lingine, unajuaje roho ipo na si hadithi ya uongo tu?

Kama roho haionekani unajuaje ipo na si hadithi ya uongo tu?
 
I think hii mada ina ukweli flani hivi, kuna jamaa hapa kitaa na wajua kabisaa na hata tuliwahi cheza mpira back in the days pamoja walikuwa wazima kabisaa ila wakaanza kuokota makopo na hizi mabaki ya vitu vya plastik
amini nakwambia hawako vyema kabisa upstairs kwa sasa, kwanza naona wamekuwa walevi mbwa, kuna mda wanajiongelesha
kwa ufupi kuna tatizo ukianza okota hizi kopo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si Kweli.

Binafsi nadhani sababu kubwa ni:

- Chronic Deppression ( Mtu hana Tumaini tena )

PLUS,

- Kudharauliwa na jamii ikiwemo familia zao.

TANZANIA.

- Hata ukiwa Mlinzi ( Kama mimi ), House Girl, Dancer, Mnenguaji Kwenye Mabendi, Kondakta, Mfanya Usafi Makosoni, Maofisini

Kama huna nguvu ya Self Respect & Psychology ya namna utajiweka sawa. Unapotea mazima

Jambo la msingi ni namna ya kurasmisha hizi kazi ili kila mtu apate heshima.

Ulaya na US wamerasmisha kila kitu mpaka STRIPPING na PORN INDUSTRY na hatuoni mtu anakuwa chizi.

Hizi kazi unazoona ni mbaya ndizo wabeba box ulaya wanafanya tena mpaka za KULEA WAZEE ( Tena vizee vingine vikorofi vinaweza kukutemea mpaka MAKOHOZI ) lakini mpaka immigrants wenye Masters wanafanya ukiachilia mbali kusafisha MAJIJI
 
Hujajibu swali langu, na hapo hapo umenitungia maswali zaidi.

Roho ni nini?

Unaweza kuthibitisha ipo na si hadithi ya uongo ya kutungwa na watu tu?
Roho ni nguvu ya uhai ya mwanadamu au kiumbe chochote kilicho na uhai. Ile nguvu ya uhai " force of life " ya mwanadamu au kiumbe hicho ndio inayo itwa roho.
 
Wabeba box hawa hawa ambao wamechanganyikiwa mpaka hawaamini Mungu kama Kiranga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…