matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 9,514
- 23,523
Kumuamini Mungu ndio risk (kujihatarisha) kikubwa kuliko vyote KWA mwanadamu wa kawaida.
Unamuamini Mungu kupitia maneno ya BIBLIA (wakristo). Na hautakiwi KUWA na ushahidi mwingine wowote wa hicho unachokiamini isipokuwa maneno hayo peke yake.
Mfano.
Ukisema huogopi, ushahidi wako uwe ni mstari ( Hatukupewa ROHO ya hofu). Huu ndio unatakiwa uusimamie kama ushahidi hata kama mtu anapasua kichwa chako na panga.
Hii ni hata kwenye magonjwa. Ushahidi wa kupona kwako sio unafuu, au kuona maumivu yanapoa. Hata kama unaona unakata ROHO na hakuna uwezekano kabisa wa kupona. Amini utapona na ushahidi wa kupona kwako ni ( KWA kupigwa kwake (Yesu) sisi tumepona).
Kama maisha yako unasubiri mifumo yako ya fahamu ( kunusa, kuhisi, kugusa, kuona, kuonya) kama ushahidi wa imani yako, huna imani maana ushahidi wa imani KWA Mungu ni sentensi za Mungu na Sio Hali unayopitia.
Kama hauamini hivi Bado humuamini Mungu unaamini kuhusu Mungu na Sio Mungu.
Ni hayo tu
Mtumishi Matunduizi