tuko pamoja mkuu,ila kama ntakua sijakosea kuna reply moja ulisema atuwezi kulinganisha uchumi wa mafuta na mkonge,,baada ya mimi kuuliza miaka ya 60's tulikua uchumi sawa na Dubai?,
ila wewe ukaleta jibu moja la msingi ambalo nimeelielewa,kwamba sisi atuna matumizi mazuri ya akili.hapo tuko sawa kabisa wala atujatofautiana mkuu.
Naam,
Kuna mambo mawili hapa ambayo yote yako sawa na kwa juujuu ukiyaangalia, hususan kwa sababu mazungumzo yetu mwengi yanakuwa ubishi wa identity politics badala ya kuangalia facts, inawezekana mtu akaona kama kuna kujichanganya, lakini haya mambo mawili hayana kujichanganya, na hayana contradiction.
1. Ni kweli kwamba si sawa, si haki na hakuna mantiki ya kulinganisha uchumi wa katani na uchumi wa mafuta.
Kanuni moja ya muhimu ya kulinganisha vitu ni kulinganisha vitu vilivyo katika kushabihiana kiasi fulani. Waingereza wanasema "Do not compare apples to oranges". Ndiyo maana hata kwenye mashindano ya michezo kuna ligi tofauti, kwenye ndondi watu wa uzito tofauti hawapambanishwi, etc.
2.Lakini pia, hata baada ya kujua kwamba hatutakiwi kujilinganisha na uchumi wa mafuta, ni muhimu pia tujitathmini, hata kwa rasilimali zetu, yani bila hata kujilinganisha na mtu mwingine, je uchumi wetu unatakiwa kuwa hapa ulipo? Jibu ni hapana. Ndiyo maana nikasema tuna matatizo ya akili, kwa sababu tungekuwa na akili leo hii uchumi huu huu wa katani tungeweza kujiongeza tukatengenez ainternet parks vijana wakapata kazi online.
Huku nchi zilizoendelea kuna kazi hizi low paying jobs mtu hakosi $1000 kwa mwezi, inachohitajika ni internet, nidhamu ya kazi, kuwa smart katika kujifunza mabo mapya na kujua Kiingereza tu, mengine watakufundisha wenyewe. Sasa Tanzania umeme wa manati, internet ya kibatari, hata ku recommend watu inakuwa tabu. Kwa sababu watu hawajui hayo matatizo.
Tungeweza kutatua matatizo hayo tu kuna vijana wengi wangepata ajira mitandaoni.
Lakini pia serikali yenyewe imejikita kukata kodi kabla watu hawajafanikisha biashara zao, na inaweka vikwazo vingi. Mfanyabiashara wa Tanzania hata kama analipwa hela kutoka nje kupata online platform ya kumlipa ni tabu, kwa sababu ya sheria zetu.
Hao waarabu washajua kwamba uchumi wa mafuta unaisha, wanajiandaa kuingia katika "knowledge economy".
Nimeona washaanza kutengeneza parks za wanyama wa Africa. Sisi tunashangaa waarabu wanakuja kuchukua wanyama Africa, wanafanya nini? Utashangaa baada ya miaka michache badala ya watalii kuja Africa, utasikia wanaishia Dubai.
Sisi hata huo uchumi wa mazao umetushinda, na huko kwenye knowledge economy ndiyo kabisaaa, hatujaanza hata kuamka.