Hii ndiyo hasa tafsiri ya Nabii Katika Agano Jipya

karama zote za nabii, mwalimu, na mchungaji zilikuwepo ndani yake, lakini zinatoka kwenye asili yake ya kipekee ya kimungu.
Mimi nakuelewa,

Labda niiweke hivi,

Kwa kuwa hapatatokea nabii yeyote baada ya Yohana Mbatizaji kuleta unabii tofauti na INJILI YA KUZALIWA, KUFA, KUZIKWA NA KUFUFUKA KWA YESU KRISTO, INJILI YA WOKOVU KUPITIA MSALABA.

Na kwa kuwa unabii wote lazima umkiri Yesu kuwa ndiye MUNGU,

Conclusion ni kuwa Unabii wote unatimilika Katika Yesu, ndiye:

NABII WA MANABII.

Mfalme wa wafalme,

Mungu wa miungu,

BWANA wa mabwana.

Mfalme wa MILELE wa wafalme wote.

Aamen
 
Mimi nakuelewa,

Labda niiweke hivi,

Kwa kuwa hapatatokea nabii yeyote baada ya Yohana Mbatizaji kuleta unabii tofauti na INJILI YA KUZALIWA, KUFA, KUZIKWA NA KUFUFUKA KWA YESU KRISTO, INJILI YA WOKOVU KUPITIA MSALABA.

Na kwa kuwa unabii wote lazima umkiri Yesu kuwa ndiye MUNGU,

Conclusion ni kuwa Unabii wote unatimilika Katika Yesu, ndiye NABII WA MANABII.

Mfalme wa wafalme,

Mungu wa miungu,

BWANA wa mabwana.

Mfalme wa MILELE.

Aamen
Amen Amen.

Hapo tunakwenda sawa.
 
Salaam, Shalom!

Palikuwepo manabii wengi Katika agano la kale, mfano Adam, Nuhu, Musa, Elia, Nehemiah, Daniel nk nk.

NABII katika Agano la kale na kuishia kwa Yohana Mbatizaji,waliishi maporini kujitenga na UOVU kuepuka kuona, kusikia UOVU Katika mikusanyiko ya watu, ingawa SI wote, manabii hawakuoa ingawa baadhi walioa, hawakujenga au kuanzisha makanisa kama sasa, ukiona mtu anajenga nyumba ya ibada na kuhudumia watu, huyo ni mchungaji mwenye karama ya unabii, Mungu akimwita nabii akafungue kanisa, huyo ni mchungaji lakini ndani ana karama ya unabii.

TAFSIRI YA NABII.

Nabii ni mtu aliyeteuliwa na Mungu , mtu huyo, kinywa chake, Mungu hukitumia kunena yatokayo kwa Mungu, kuelekea nchi na JAMII husika.

Nabii Musa kwa Mfano, aliongea na Mungu direct, au kwa maono au kupitia ndoto Kisha akaja kuleta ujumbe wa Mungu kwa watu wa Mungu.

Uandishi pia wa Biblia, wote, ni manabii walipokea neno kwa njia ya kusikia,maono au ndoto Kisha wakaandika walichosikia Katika gombo na vitabu mbalimbali ambavyo ndivyo vilivyokusanywa kupata Biblia.

NABII WA MWISHO NI NANI.

Yesu Kristo ameweka wazi, nabii wa Mwisho ni Elia/ Yohana Mbatizaji, na hakuna mwingine baada yake kwa sababu baada ya Yesu kuja, akazaliwa, kufa na kufufuka, hapatatokea nabii mwingine yoyote atakayeleta unabii wowote kinyume na INJILI YA AGANO JIPYA YA KUZALIWA ,KUFA, KUZIKWA NA KUFUFUKA KWAKE YESU KRISTO.

Hivyo ukisikia nabii mwingine yeyote amekuja na kuleta habari tofauti na injili ya ufalme ya YESU KRISTO aliyezaliwa,aliyekufa,akazikwa na kufufuka, huyo ni nabii wa uongo aongozwaye na Roho ya mpinga Kristo.

TAFSIRI YA NABII KATIKA AGANO JIPYA.

Nabii katika Agano jipya ni mtumishi wa Mungu anayehubiri Neno la Mungu kwa nguvu za Roho mtakatifu. Ni aliletaye neno kutoka kuandikika, likatamkika na kuwa hai na kuleta matokeo halisi.

Nabii katika Agano jipya ni yule anayeliamini neno na kuhubiri injili kwa Imani na watu wanaamini na kupokea nguvu na neema ya wokovu.

Kwa Tafsiri hiyo, nabii anaweza kuwa Mchungaji kwa maana, kuhubiri injili kwa kuongozwa na Roho mtakatifu ni sharti kwanza usikie sauti iliyo ndani ya neno la Mungu lililoandikwa, Kisha uipokee Katika Roho Kisha uilete kuwa neno ambalo utalitamka kwa kinywa Kisha likasikiwa na watu kwa sikio la Roho na likapokelewa kwa Imani.

Nabii na unabii Katika Agano jipya ni mtu ndani ya kanisa aliye chini ya mchungaji aliyepewa karama ya unabii, na kama nilivyoeleza hapo juu,

Nabii mwenye karama ya unabii( prophecy) ataena kwa lugha, Mungu atatumia kinywa chake kunena injili na ufunuo juu ya Injili, Kisha atatafsiri alichokisema kwa lugha aliyonena kama ni lugha ya malaika au lugha za wanadamu Ili kulijenga kanisa.

TAFSIRI POTOFU YA NABII KATIKA AGANO JIPYA.

Kuna watu wanapotosha nabii na tafsiri ya Nabii kwa kuchanganya na kitu kiitwacho " Jicho/mwonaji" au "macho ya kinabii/ mwonaji".

Ukisikia mtu anawaambia watu akiwaambia Jana ulikula Nini, au kesho utaenda wapi, au ulizaliwa sehemu Fulani, Umesoma Shule Fulani, au jina la mama yako ni Fulani bila kumwambia, huyo SI nabii, ni sehemu tu ya office ya unabii iitwayo uonaji./ Mwonaji./ Macho ya Roho, sasa huyo SI nabii kamili.

PROPHECY:Is to preach the Gospel with power of The Holly spirit/ spirit of JESUS.

Note: WEWE pia unisomaye Katika thread hii ni nabii ikiwa tu Umeokoka, unaye Roho mtakatifu,na unahubiri injili kwa nguvu za Roho mtakatifu.

Mungu awabariki.

Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako fuatisha sala hii:

Ee Mungu katika jina la Yesu Kristo, nina kukiri wewe kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu, ninatubu dhambi zangu zote, ninaomba unisamehe, ulifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uliandike jina langu katika kitabu cha uzima, nipe uwezo wa kuishi maisha matakatifu, dhambi isinishinde, uovu usinishinde, ulevi usinishinde, uzinzi usinishinde, uchawi usinishinde, ninaomba hayo kupitia jina la Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Aamin
Nabii ni neno la kiarabu likimanisha aliyetumwa na Mungu na ujumbe mpya na kwa Kiislamu wapo wanne tuu .
 
Nabii wa mwisho ni Elia/ Yohana Mbatizaji.

Baada ya kutengeneza njia ya Agano jipya, injili ya ufalme,injili ya wokovu KUPITIA MSALABA na damu ya Yesu,

Hakuna Tena unabii mpya au unabii mpya nje Ya kuzaliwa, kufa,KUZIkwa na kufufuka kwa Yesu.

Nje ya hapo , unabii mpya ni ule utikao kwa mpinga Kristo.
 
Nipo mtumishi humu JF.

Kila nipatapo ujumbe wa Mungu, huja kushare na wana wa Mungu.
Amina, inapendeza sana. HATA Mimi nakuona huku jf, lkn nakutafuta ndugu yngu ktk Ufalme wa Mbinguni, Una group la NENO tofauti na JF?
 
Sina group mtumishi,

Mimi ni mtumishi mdogo tu, humu JF ndipo sehemu pekee ambayo huwa napata kibali kushare injili Kila nipatapo ujumbe.

Huko kwingine labda baadae nikipata maelekezo kufanya hivyo.
 
Waukweli anakuwajeM
Nabii wa kweli anakidhi yote yaliondikwa kwenye biblia,hapingani na maandiko

Branham ni nabii wa uongo kwasababu 👇 👇

1. Alijitangaza kuwa nabii wa Malaki 4:5-6 na Ufunuo 10:7, jambo ambalo haliko sawa na mafundisho ya Biblia.

2. Alifundisha kuwa Hawa alifanya zinaa na nyoka (the Serpent Seed doctrine) – mafundisho yasiyo na msingi wa Biblia.

3. Alikataa fundisho la Utatu (Trinity), akasema ni la shetani, kinyume na mafundisho ya Wakristo wengi.

4. Alidai picha yake ilionekana na “nuru ya kipepo/ malaika” juu ya kichwa chake, jambo lisilo na uthibitisho wa kibiblia.

5. Alitabiri kuwa ulimwengu ungekoma mwaka 1977, lakini haikutokea (Kumb. 18:22 inasema nabii akitabiri na halitokei, huyo ni wa uongo).

6. Alijitangaza kuwa ndiye “mjumbe wa mwisho” wa kanisa la mwisho (Laodikia), akijiweka kwenye nafasi ya kipekee isiyoandikwa.

7. Alisema mtu yeyote asiyemkubali yeye hana Roho wa Mungu, jambo ambalo ni la kujitukuza binafsi.

8. Alivuruga mafundisho ya ubatizo, akisema lazima iwe “kwa jina la Yesu pekee” na siyo “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19).

9. Aliwafundisha wafuasi wake wamfuate yeye zaidi ya Kristo, jambo lililosababisha “Branhamism” badala ya Ukristo.

10. Wafuasi wake walimwinua kama mtu asiyekosea, jambo linalopingana na Biblia (Warumi 3:23: “wote wametenda dhambi”).
 
Nabii wa mwisho ni Elia/ Yohana Mbatizaji.

Baada ya kutengeneza njia ya Agano jipya, injili ya ufalme,injili ya wokovu KUPITIA MSALABA na damu ya Yesu,

Hakuna Tena unabii mpya au unabii mpya nje Ya kuzaliwa, kufa,KUZIkwa na kufufuka kwa Yesu.

Nje ya hapo , unabii mpya ni ule utikao kwa mpinga Kristo.
Kaka ,mbona kama unapingana na maandiko ?Unajua hata kitabu cha matendo ya mitume Kuna manabii waliendelea kuwepo

Unajua Utabiri wa manabii wa uongo wa Yesu, unamaanisha waukweli watakuwepo ila tujihadhari na wauongo kama Hawa kina MWAMPOSA, muhamad,n.k

Yohana Mbatizaji alitabiri kuhusu Yesu na alipata karama ya unabii kwa ajili ya muda wake (Luka 1:76-77).

Baada yake, unabii uliendelea kupitia manabii wengine na pia kupitia Roho Mtakatifu baada ya kuanzishwa kwa Kanisa la Kristo (Matendo 2:17-18).

Yesu pia aliahidi kwamba Roho Mtakatifu atawapa wafuasi wake nguvu ya unabii (Matayo 10:41, Luka 24:49, Matendo 1:8).

Kwa ufupi
👉 Yohana hakukoma kuwa nabii, lakini karama ya unabii iliendelea kwa wafuasi wa Kristo na manabii wengine.
 
Umenena vyema,

Unabii upo, manabii wapo hata baada ya Yohana Mbatizaji.

Kusema Yohana Mbatizaji/Elia ni nabii wa mwisho,

Tafsiri yake ni kuwa, hapatatokea nabii mwingine wa kuja na unabii mpya tofauti na injili ya ufalme ya YESU KRISTO kuzaliwa, kufa KUZIkwa na kufufuka siku ya tatu.

Unabii na manabii wote wa kweli waliopo wanatabiri KUPITIA Roho wa Yesu ( Roho mtakatifu)

Hapatatokea nabii wa kutabiri nje ya Roho wa Yesu Roho mtakatifu,

Akitabiri kinyume na INJILI, nje ya Roho wa Yesu Roho mtakatifu, ni nabii wa uongo.

Hiyo ndiyo tafsiri ya kusema Yohana Mbatizaji/ Eliya ni nabii wa mwisho.

Akija nabii Leo au kesho akasema Yesu amezalliwa Kenya au Ureno, kwamba amekuja kuukomboa ulimwengu ni nabiii wa uongo huyo.

Sijui umenielewa?
 
Kama ni hivo upo sawa kabisa

🙏🙏
 
Kama ni hivo upo sawa kabisa

🙏🙏
Ni hivyo ,

Unabii wa AGANO JIPYA ni shart nabii ajazwe na Roho mtakatifu.

Akitumia Roho ingine kutabiri au kutenda miujiza, akaacha Msingi wa kuwahubiri watu injili ya MSALABA, juu ya kuacha DHAMBI,

Hiyo ni Roho ya mpinga Kristo.

Ubarikiwe kama umeelewa.
 
Utajuaje huyu kajazwa roho mtakatifu?
 
Utajuaje huyu kajazwa roho mtakatifu?
Shart atabiri yaliyo ndani ya Biblia,

Lazima awe na atende na kutabiri sawa sawa na maagizo ya YESU.

Mfano,

1. akiombea mgonjwa hatodai malipo, ni Bure, mgonjwa akishukuru sawa, asipotoa chochote sawa.

2. Shart Aishi MAISHA MATAKATIFU, ukisikia tuhuma za uzinzi, huyo SI nabii wa kweli.

3. Upendo, asiwe na kiburi na majivuno, lazima ahurumie maskini. Sadaka zirudi kusaidia wajane na yatima, asijilimbikizie utajiri utokanao na sadaka.

4. Shart awakataze watu UOVU na kuwaambia watubu na kuacha DHAMBI, ukiona wanawake wanavaa nusu uchi kanisani kwa nabii na hakemei, ni wa uongo huyo. Nk nk nk
 
Umenena vema
 
Yesu aliposema maandiko haya yametimia mbele yenu mnapotasikia pia watu walikataa kwa sababu alikuwa anajionyesha kama mtu alieandikiwa andiko.

Ubatizo mzima hakuna aliewahi kubatizwa kwajina la baba mwana na roho mtakatifu kama unalo ilo andiko lilete.

Hawa hakula tunda io ni kweli hiblia inasema mungu aliumna miti yote ifaayo kwa kula kutoka arrdhini kisha ikasema kisha mti waujuzi wa mema na mabaya, soma biblia utaona haikutoka chini ya ardhi,na walipokula walijua wapo uchi na mwanamke akalaaniwa sehem za siri, hata watoto waliozaliwa walikuwa mmoja anatabia ya kiungu mwingine ya kishetani.

Malaki 4 imesema wazi kuwa mungu atatuma roho ya eliya kabla dunia kuchomwa moto, na io ni lazima itimie.

Na nabii wa kweli anasehem yake kwenye maandiko,yanamtambua.

Branham hakuwahi kusema mwisho wadunia ni 1977 usigoogle, pia kinatofaut kati ya unabii na bashiri

Maandiko hamna sehem yanasema mungu ananafsi 3 ila biblia inasema mungu ananafsi moja.

Fatilia vzr,hayo makanisa makubwa ndio yameandika izo ulizoleta kwakuwa ni kinyume na taratibu zao za tangu kale,

Na nabii yoyote wa kweli usizani atapendwa hajwahi kuwepo mmoja, mwanzo wa huduma ya yesu alipendwa sana, ila.mwisho alipoanza kusema mimi na baba ni kimoja ndo wakamkasirikia.

Nabii wa kweli anakidhi yote yaliondikwa kwenye biblia,hapingani na maandiko

Branham ni nabii wa uongo kwasababu 👇 👇

1. Alijitangaza kuwa nabii wa Malaki 4:5-6 na Ufunuo 10:7, jambo ambalo haliko sawa na mafundisho ya Biblia.

2. Alifundisha kuwa Hawa alifanya zinaa na nyoka (the Serpent Seed doctrine) – mafundisho yasiyo na msingi wa Biblia.

3. Alikataa fundisho la Utatu (Trinity), akasema ni la shetani, kinyume na mafundisho ya Wakristo wengi.

4. Alidai picha yake ilionekana na “nuru ya kipepo/ malaika” juu ya kichwa chake, jambo lisilo na uthibitisho wa kibiblia.

5. Alitabiri kuwa ulimwengu ungekoma mwaka 1977, lakini haikutokea (Kumb. 18:22 inasema nabii akitabiri na halitokei, huyo ni wa uongo).

6. Alijitangaza kuwa ndiye “mjumbe wa mwisho” wa kanisa la mwisho (Laodikia), akijiweka kwenye nafasi ya kipekee isiyoandikwa.

7. Alisema mtu yeyote asiyemkubali yeye hana Roho wa Mungu, jambo ambalo ni la kujitukuza binafsi.

8. Alivuruga mafundisho ya ubatizo, akisema lazima iwe “kwa jina la Yesu pekee” na siyo “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19).

9. Aliwafundisha wafuasi wake wamfuate yeye zaidi ya Kristo, jambo lililosababisha “Branhamism” badala ya Ukristo.

10. Wafuasi wake walimwinua kama mtu asiyekosea, jambo linalopingana na Biblia (Warumi 3:23: “wote wametenda dhambi”).
 
Nabii wa kweli anakidhi yote yaliondikwa kwenye biblia,hapingani na maandiko

Branham ni nabii wa uongo kwasababu 👇 👇

1. Alijitangaza kuwa nabii wa Malaki 4:5-6 na Ufunuo 10:7, jambo ambalo haliko sawa na mafundisho ya Biblia.

2. Alifundisha kuwa Hawa alifanya zinaa na nyoka (the Serpent Seed doctrine) – mafundisho yasiyo na msingi wa Biblia.

3. Alikataa fundisho la Utatu (Trinity), akasema ni la shetani, kinyume na mafundisho ya Wakristo wengi.

4. Alidai picha yake ilionekana na “nuru ya kipepo/ malaika” juu ya kichwa chake, jambo lisilo na uthibitisho wa kibiblia.

5. Alitabiri kuwa ulimwengu ungekoma mwaka 1977, lakini haikutokea (Kumb. 18:22 inasema nabii akitabiri na halitokei, huyo ni wa uongo).

6. Alijitangaza kuwa ndiye “mjumbe wa mwisho” wa kanisa la mwisho (Laodikia), akijiweka kwenye nafasi ya kipekee isiyoandikwa.

7. Alisema mtu yeyote asiyemkubali yeye hana Roho wa Mungu, jambo ambalo ni la kujitukuza binafsi.

8. Alivuruga mafundisho ya ubatizo, akisema lazima iwe “kwa jina la Yesu pekee” na siyo “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19).

9. Aliwafundisha wafuasi wake wamfuate yeye zaidi ya Kristo, jambo lililosababisha “Branhamism” badala ya Ukristo.

10. Wafuasi wake walimwinua kama mtu asiyekosea, jambo linalopingana na Biblia (Warumi 3:23: “wote wametenda dhambi”).
Unaweza kuniambia hao wajumbe ni wakina nani ambao biblia imewaandika,
Wajumbe wa nyakati saba,

Ufunuo wa Yohana 10:7
[7]isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.
 
Ufunuo 10:7 inasema “watumishi wake manabii” ni wale waliokuwa wakihubiri na kushuhudia ujio wa Ufalme wa Mungu katika historia, si majina maalum ya watu binafsi.,Na hapa ndipo matapeli wamejipenyeza na kusema ni wao .

Kwa maneno mengine, hii si listi ya wajumbe wa karne ya 20 au mtu fulani aliyechaguliwa kuwakilisha malaika wa saba., kama Branham alivyojipachika

Ikiwa Biblia haijataja majina, kwa msingi gani Branham au mtu yeyote tapeli anaweza kudai kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe hao?
 
Back
Top Bottom