Wala sio hivyo, Magufuli sio chaguo la Kikwete lakini amekuwa Rais. Hata Magufuli mwenyewe hakuwahi kuamini kama yeye ndiye Rais hadi amekufa.
CCM ina machinery yake ambayo is so powerful. Hata Rais wa nchi hana uwezo wa kuidhibiti. Ukiikorofisha itakukorofisha wewe kwanza kabla hujaanza kuikorofisha. Kuna jamaa mmoja alikuwa anataka kujaribu kuondoa ukomo wa urais kwenye Katiba, weee!! hakuamini kilichompata yeye na jamaa zake.
CCM sio chama cha siasa, it is a system inayojiendesha yenyewe ambayo haina kabila, dini, jinsia wala ukanda. Ni system ambayo inazingatia amani na utulivu wa watu kwanza na mengine yooote yatafuata. Yaani barometer yao inapima kiwango cha amani na utulivu nchini tu baasi. Mifumo yote ya nchi (serikali, bunge na mahakama) inasomana katika kuhakikisha amani na utulivu wa nchi.
Mtu kama Nchimbi amekulia ndani ya CCM, anaujua huu mfumo lakini amefanya makusudi tu kuukorofisha. Anafahamu namna mfumo ulivyowakorofisha watu maarufu kuliko yeye kama akina Kambona, Bibi Titi, Mzee Aboud Jumbe, Hamad Sharif, Lyatonga, Kingunge, Lowassa, Sumaye, Njelu, Kolimba, Komba, Melecela, Polepole, Msindai, Membe, nk. Ukiangalia haya majina ya hawa watu utagundua kuwa ni watu wa makabila, dini, umri, uzoefu, na jinsia tofautitofauti.
Huwezi kuwa na janaba yako halafu ukatishe moja kwa moja kwenda Ikulu mfumo ukuangalie tu kiboya.