Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

We Kuna kitu unakuTafuta sio bure, yaan unamuhukumu mama yako kisa umepata heka 50 na kiajira , huo upumbv ulisomea kbsa maana sio kwa kiwango Hiko,

Mama ni mama acha ujinga mpe pesa hata za kuzidi stupid wew [emoji57][emoji57][emoji57]
 
Nakumbuka kusoma story kama hii siku za Nyuma wakati UN inafanya kazi Arusha pale AICC ambapo wafanyakazi walipata hela nyingi.
Kama ni tofauti, saidia mama yako halafu, nakushauri kwa dhati kabisa, wasaidie na hao ndugu zako Kama unauwezo wape mitaji midogo midogo kwa masharti kuwa umewakopesha hata kama rohoni unajua umewapa.
Kuwakopesha ni ili waiangalie vizuri. Hii itasaidia kutoa funzo kwenye familia na hizo dharau hazitatokea tena kwa mwingine Ndugu zako ni ndugu zako tu,
Watu hesema; mtoto akijisaidia kwenye mkono wako, hauukati badala yake unauosha na maisha yanaendelea
 
Kwa Sasa nafikiri kununua KUBOTA....... ,Uko vizuri
 
Kama ni Mimi mama ningepiga chini
 
Nimekuelewa vizuri Sana mkuu
 
Anyway ndiyo changamoto na mitihani ya maisha , ili nafsi yako iwe huru wasaidie unavyo weza tu ila kaa nao mbali, mengine mwachie MUNGU!!!
 
Sidhani kama kuna mama anaweza msimangia mwanae chakula, toto hata kama tukutu namna gani atamfichia msos wakat mzee analeta nongwa
 
Nimeelewa kwanini wenzetu wazungu hawaendekezi huu undugu undugu ,kila mtu apambane na life lake , undugu undugu ni unafiki tu. Hasa hizi ngozi nyeusi zilizolaaniwa
 
Kama ungekuwa unaamini ktk Mungu ningekushauri usamehe na anza kuwasaidia. Mungu ananjia nyingi. Huenda kama usingepitishwa kwenye moto na ndg zako, ungebweteka na usingesoma kwa bidii.
 
Yametupata sana hayo Wenzio. Hao wengine wooooote, waache hapo pembeni. Usiwasemeshe. Wakiwa na shida, wasaidie KWA KIASI. Mama usimwache kamwe na usimkumbushe matendo yake kwako. Huwezi jua walimwengu walimwambia nini kuhusu wewe ulipokuwa chuoni. Nunua zawadi nzuri kabisa, mpelekee Mama, mtandike na bima moja ya afya yenye scheme matata kabisa, hakisha anavaa, anakula vizuri. Utabarikiwa sana na Utakuja kunishukuru mbele za Mungu na mataifa.
 
Wewe utakuwa na tofauti gani na wao?

Au tu wao walianza wewe unamaliza.

Wasaidie pale unapoona unahitajika msaada wa kibinadamu, siyo kwa sababu wamekutendea mema, la hasha. Kwa sababu ya ubinadamu.

Saidia wengine hata ambao siyo ndugu zako, ambao wapo kama wewe wa enzi zile....


Tizama ridhiki ilipitishwa kwao wakaitumia kama fimbo, imehamishiwa kwako uwe baraka kwa watu wote, Mungu asijute kukupa.
 
Nikisoma nyuzi kama hizi kisha nikumbuke marehemu mama yangu alivyoteseka kutulea, huwa natamani afufuke hata siku moja nimtunze kisha aage dunia tena, maana aliaga dunia kipindi naanza kupata visenti, sikupata fursa ya kumlipa chochote.
Aisei yule ningemsamehe hata kama angenisimanga kivipi, jameni mna bahati nyie ambao mama zenu bado wako hai.
 
Mkuu upo sahihi kwa uamuzi wako
Katika maisha ndugu yako wa kwanza ni mama yako katika hali yoyote ile kama alikukosea ni lazima umsamehe
Hao wengine watajua wenyewe..
 
Umenena vyema mkuu, Hawa wazazi hubadilika kabisa
 
Well said....samehe Kaa nae mbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…