Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Hapo kwa mama umebugi mzee maneno yake makali sio masimango ni msongo aliokuwa nao tu !isitoshe mama halipiziwi kisasi ,huwezi jua hiyo miaka hana kitu ukute hadi alidanga kwa ajili yako then umletee unyoko!
Huyo dada ishia kumpa msosi tu tena akikutembelea sio aje kukaa kwako
Na nimemuambia amsamehe mama.
 
Fanya mambo yako usiwakaribishe Wala kiwashirikisha mambo yko watakuharibia,wale waliokuwa wanakunyanyasa wakat huna ndio roho zao halisi,hawa wa sasa ni feki.Na ukija kuowa jipange mkeo na watoto kuchukiwa kwamba wanafaid hela zako.
Kweli kabisa
 
Kwahiyo unajiona hapo umemaliza yaninkuwa na Viwanja viwili na mshahara WA milion 2 unaona ni hela nyingi.

Saidia watu kijana Acha kulipiza visasi kila MTU duniani ana nafasi yake awe masikini au Tajiri. Ndio maana hata Bakhrresa anamtegemea masikini awe mteja wake WA bidhaa. Usiishi Kwa visasi. Hizo Mali ulizonazo ni ndogo Sana na chache usitake kujiona umefika kuanza kuwadharau watu. Kwanza Mali zenyewe sio Cash inflow kwako means siku ukivuruga kazini ukapigwa chini utauza hizo Viwanja ....


Wewe ndio inabidi uwe mwanzo WA tabia mpya kwenye familia. Vunja roho za visasi
Ila msimlazimishe kusamehe. Mshaurini asamehe na si kumlazimisha.
 
Huyo dada amkatae ila sio Mama, kisa tuualitoa lugha ya masimango, ilhali kashasema mama maisha aliyoyapitia, unaona kabisa mategemeo yake kwa mwanafunzi wa chuo yalikuwa yapi, sometime mabimkuwa ni stress, umri, na ugumu wa maisha ndio huwafanya yote hayo.
Hakika
 
Baba yangu alifariki wakati nikiwa Mtoto mchanga hivyo nililelewa na Mama tu naye hakuwa na uwezo Hivyo nilisomeshwa na wasamaria wema. Mtu pekee Aliyekuwa na uwezo wa kiuchumi Ni dada aliyeolewa na yeye hakutaka mazoea kabisa.

Kwa jinsi maisha yalivyokuwa magumu, nilipofika Chuo nikawa natumia boom(mkopo wa elimu ya juu) kumtunza mama. Imagine mtu nilikuwa nalipwa laki tano na kumi na kupaswa niitumie kwa miezi miwili lakini nilikuwa najibana kwa kadiri iwezekanavyo nitumie mama Kati ya elfu 60 na 100,000.

Nilipomaliza chuo nikarudi nyumbani, hakuna ajira na Sina mtaji wa biashara au kilimo, nikawa nashinda ndani kwa mawazo au siku nikibahatisha kibarua Cha zege au kumsafishia mtu shamba naifanya kwa nidhamu, napata hela ya bundle la muendelezo wa kusaka ajira.

Ajabu ya karne; Mama mzazi alianza kunisimangia chakula na kunilaumu kuwa nilitumia vibaya mkopo wa Chuo nilikuwa nawapa makahaba wa mjini na kwamba ningekuwa na akili ningetambua kuwa mimi ni Mtoto yatima na ningetunza akiba ili nimalizapo chuo nifungue kioski!

Mungu siyo Shetani, baada ya miaka miwili ya ukosoefu wa ajira, nikapata kazi nzuri Sana kwenye moja ya taasisi za Kimataifa, nimeanza kusahau yale maisha magumu. Nimewekeza katika ardhi, nimenunua ekari 50, nimenunua viwanja viwili Arusha mjini na kimoja Kibaha. Kwa Sasa nawaza kununua power tiller(KUBOTA) ili inisaidie kwenye kilimo ambacho nitakianza mwakani rasmi.

Sasa nikikumbuka vituko vya mama, na Ndugu kuwatumia hela napata taswira ya yale maneno yale masimango. Naghairisha.

Yule dada Aliyekuwa na uwezo wa kunisomesha akagoma, Benki imewafilisi, wakaachana na mumewe. Amebaki kunipigia simu eti "nilikuwa nakusalimu" wakati kipindi nipo down hakuwahi kunipigia na nikimpigia hapokei simu, nikimpigia kwa number ngeni akishafahamu Ni mimi, anakata.

Maisha ya hapa Duniani ni fumbo
Unamtenga mpaka mama yako mzazi . Mama yako ndio aliekusomesha mkumbuke
 
Pomoja na hayo yote kutokea mkuu nakushauri usiache kumhudumia mama yako,siku zote yalipe mabaya kwa mema na Mungu atakubariki Sana.
 
Mleta mada kama vile Malaika yani tangu azaliwe hadi sasa hivi hajawahi kumkosea Mtu yeyote duniani.

Mama ni Mama utake usitake ipo siku hatakuwepo duniani na utatamani sana kumwomba msamaha ila utakuwa ushachelewa.

Kuna faida gani sasa ukiwa unatumia pesa bila ya damu yako kunufaika nazo?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kwani wao wakati nawahitaji hawakujua haya maneno.
Maisha yaleyale walioishi na Mimi nami nitaishi nao hivyohivyo.

#YNWA
Hata Kama unataka kuliipiza,tumia njia nzuri ya kuwachomolea huku mnacheka,usioneshe beef live! Kua Kama Mkwere Mzee wa Msoga,anacheka huku ana lake moyoni!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom