Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Huu uzi ni feki kabisa...

dogo juzi tu kahitimu chuo 2021

kaanza kutuma maombi ya chuo mpaka 2022 hajapata Job..

hapa kaja na uzi kafukuzwa kazi katengwa na kila mtu mpaka chawa wamemkimbia😅

Halafu anatupanga kirahisi tu eti kanunua shamba heka 50, mara anunue trekta which is not less than 30mil dadek..

dogo hebu mrudishe mkeo shule mjenge familia mkiwa wote na akili mingi

Baba yangu alifariki wakati nikiwa Mtoto mchanga hivyo nililelewa na Mama tu naye hakuwa na uwezo Hivyo nilisomeshwa na wasamaria wema. Mtu pekee Aliyekuwa na uwezo wa kiuchumi Ni dada aliyeolewa na yeye hakutaka mazoea kabisa.

Kwa jinsi maisha yalivyokuwa magumu, nilipofika Chuo nikawa natumia boom(mkopo wa elimu ya juu) kumtunza mama. Imagine mtu nilikuwa nalipwa laki tano na kumi na kupaswa niitumie kwa miezi miwili lakini nilikuwa najibana kwa kadiri iwezekanavyo nitumie mama Kati ya elfu 60 na 100,000.

Nilipomaliza chuo nikarudi nyumbani, hakuna ajira na Sina mtaji wa biashara au kilimo, nikawa nashinda ndani kwa mawazo au siku nikibahatisha kibarua Cha zege au kumsafishia mtu shamba naifanya kwa nidhamu, napata hela ya bundle la muendelezo wa kusaka ajira.

Ajabu ya karne; Mama mzazi alianza kunisimangia chakula na kunilaumu kuwa nilitumia vibaya mkopo wa Chuo nilikuwa nawapa makahaba wa mjini na kwamba ningekuwa na akili ningetambua kuwa mimi ni Mtoto yatima na ningetunza akiba ili nimalizapo chuo nifungue kioski!

Mungu siyo Shetani, baada ya miaka miwili ya ukosoefu wa ajira, nikapata kazi nzuri Sana kwenye moja ya taasisi za Kimataifa, nimeanza kusahau yale maisha magumu. Nimewekeza katika ardhi, nimenunua ekari 50, nimenunua viwanja viwili Arusha mjini na kimoja Kibaha. Kwa Sasa nawaza kununua power tiller(KUBOTA) ili inisaidie kwenye kilimo ambacho nitakianza mwakani rasmi.

Sasa nikikumbuka vituko vya mama, na Ndugu kuwatumia hela napata taswira ya yale maneno yale masimango. Naghairisha.

Yule dada Aliyekuwa na uwezo wa kunisomesha akagoma, Benki imewafilisi, wakaachana na mumewe. Amebaki kunipigia simu eti "nilikuwa nakusalimu" wakati kipindi nipo down hakuwahi kunipigia na nikimpigia hapokei simu, nikimpigia kwa number ngeni akishafahamu Ni mimi, anakata.

Maisha ya hapa Duniani ni fumbo
Wasamehe wote. Ukifanikiwa kuwasamehe basi utaishi vizuri zaidi ya sasa
 
Iko hivi hao wote walikutesa wakati unashida ujue nao walipitia maisha magumu walivyopata wakaona ndo mda wakuwatesa na kuwanyanyasa wasionacho.
.
Kama ulivyosema kuwa dunia ni fumbo bas bado unafumbo mbele yako, hujui kesho utakuwa nani pengine kesho ndo anguko lako kubwa kuwahi kutokea maishani mwako.
.
Nachokushauli samehe sahau, saidia watu kadri uwezavyo, sometimes Mungu hukupa ridhiki kama mlango na wengne kubarikiwa kupitia wewe kwaiyo nakushauri tu saidia watu kadri utakavyojaliwa na utazidishiwa ulichonacho lkn kwa roho mbaya jiandae kurudi kwenye ufukara kwa mara nyingne
 
Kwani wao wakati nawahitaji hawakujua haya maneno.
Maisha yaleyale walioishi na Mimi nami nitaishi nao hivyohivyo.

#YNWA
Muheshimu mzazi wako Ili usife mapema....
Wanasema wahenga.....Mzazi hakosei 😊
🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
#ASAP
 
Umesomeshwa na wasamalia wema ila wewe umeshindwa kuwa msamalia mwema.

Kituko Cha karne.
 
Maisha ya Hapa Duniani ni Fumbo "Ukishalijua hilo basi huna hata haja ya kuwa na kisasi na choyo.Kama unao uwezo wa kuwasaidia basi unawasaidia.Maana unaweza kuwa unaandaa wema kwa ajili yako.
 
Iko hivi hao wote walikutesa wakati unashida ujue nao walipitia maisha magumu walivyopata wakaona ndo mda wakuwatesa na kuwanyanyasa wasionacho.
.
Kama ulivyosema kuwa dunia ni fumbo bas bado unafumbo mbele yako, hujui kesho utakuwa nani pengine kesho ndo anguko lako kubwa kuwahi kutokea maishani mwako.
.
Nachokushauli samehe sahau, saidia watu kadri uwezavyo, sometimes Mungu hukupa ridhiki kama mlango na wengne kubarikiwa kupitia wewe kwaiyo nakushauri tu saidia watu kadri utakavyojaliwa na utazidishiwa ulichonacho lkn kwa roho mbaya jiandae kurudi kwenye ufukara kwa mara nyingne
Watu wengi wanapenda kua karib na UWARIDI....

Ukiwa masikini hauta tafutwa 😃😊 pambana sana yaan Mm kitu naogopa kurudi kwenye dimbwi la UMASKINI na mwomba sana Mungu.......

Umaskini unachosha for sure OGOPA umaskini utakimbiwa na Kila mtu MKE.....

sure 😄😊 ukiwa maskini huto tafutwa na yeyote maana kapuku maana yake ni burden...
 
Unachokosea ni kumnanga Mama Yako.

Kumbuka mama ni mzazi,
Na mzazi huwa hakosei,
Na hata akikosea huwa asemwi.

Mama ni Mungu wa Pili.
Kwa lolote Baya atakalolifanya haliondoi mazuri mengi aliyokupambania.

Huwezi kupima upendo WA mama Kwa kauli yake moja yenye hasira ndani yake.

Kuhusu ndugu nakubaliana na ww, Kwa Nchi za ulimwengu wa Tatu hasa hizi Nchi za Kiafrika ndugu wengi ni watu wanafiki mno.

Binafsi naamini katika kujipambania mwenyewe Kwanza, kuwaza kuwa eti Una ndugu ambae anaweza kukupush ni hatua ya mwanzo ya kufeli mipango yako.

Kamwe usipende kuweka matarajio yako Kwa watu wengine. Matumaini yangu utampambania mama kwa Hali yoyote Ila hao wengine achana nao.
 
Alipomsimang sababu ya chakula na kwamba alichezea boom alikuwa siyo mama?Pig chini tu
Mkuu,Kuambiwa ukweli sio masimango.Mama alikuwa na uchungu na ilikuwana lazima akwambia maneno yatakayokurudisha kwenye reli hata kama yanaumiza.Unafikiri alifurahia kwamba huna kazi na umesoma.Huyu mleta mada anaoneka ni mtu mwenye roho mbaya ila sasa nafsi inamsuta inabidi ajipe moyo.

Katika maisha yalipita si Ndwele watu wana ganga yajayo.Kama unao uwezo wa kuwapa msaada wape ila usifikiri kwamba watakulipa fadhila na wala usifikri kwamba wangukutendea vyema ungewajali.

Pia hata hao watu baki waliokusaidia naona hata huna time now.So Face IT an BE GOOD.

DO GOOD FOR YOUR OWN GOOD
 
Baba yangu alifariki wakati nikiwa Mtoto mchanga hivyo nililelewa na Mama tu naye hakuwa na uwezo Hivyo nilisomeshwa na wasamaria wema. Mtu pekee Aliyekuwa na uwezo wa kiuchumi Ni dada aliyeolewa na yeye hakutaka mazoea kabisa.

Kwa jinsi maisha yalivyokuwa magumu, nilipofika Chuo nikawa natumia boom(mkopo wa elimu ya juu) kumtunza mama. Imagine mtu nilikuwa nalipwa laki tano na kumi na kupaswa niitumie kwa miezi miwili lakini nilikuwa najibana kwa kadiri iwezekanavyo nitumie mama Kati ya elfu 60 na 100,000.

Nilipomaliza chuo nikarudi nyumbani, hakuna ajira na Sina mtaji wa biashara au kilimo, nikawa nashinda ndani kwa mawazo au siku nikibahatisha kibarua Cha zege au kumsafishia mtu shamba naifanya kwa nidhamu, napata hela ya bundle la muendelezo wa kusaka ajira.

Ajabu ya karne; Mama mzazi alianza kunisimangia chakula na kunilaumu kuwa nilitumia vibaya mkopo wa Chuo nilikuwa nawapa makahaba wa mjini na kwamba ningekuwa na akili ningetambua kuwa mimi ni Mtoto yatima na ningetunza akiba ili nimalizapo chuo nifungue kioski!

Mungu siyo Shetani, baada ya miaka miwili ya ukosoefu wa ajira, nikapata kazi nzuri Sana kwenye moja ya taasisi za Kimataifa, nimeanza kusahau yale maisha magumu. Nimewekeza katika ardhi, nimenunua ekari 50, nimenunua viwanja viwili Arusha mjini na kimoja Kibaha. Kwa Sasa nawaza kununua power tiller(KUBOTA) ili inisaidie kwenye kilimo ambacho nitakianza mwakani rasmi.

Sasa nikikumbuka vituko vya mama, na Ndugu kuwatumia hela napata taswira ya yale maneno yale masimango. Naghairisha.

Yule dada Aliyekuwa na uwezo wa kunisomesha akagoma, Benki imewafilisi, wakaachana na mumewe. Amebaki kunipigia simu eti "nilikuwa nakusalimu" wakati kipindi nipo down hakuwahi kunipigia na nikimpigia hapokei simu, nikimpigia kwa number ngeni akishafahamu Ni mimi, anakata.

Maisha ya hapa Duniani ni fumbo
Ila mama usimkazie hafamu chochote
 
KIJANA POLE KWA YALIYOKUKUTA. LEO NIMEAMINI KUWA SI KILA MAMA WA KUKUZAA ANAWEZA KUWA MWEMA AU KUKUPENDA KWA DHATI. MAMA WA KUKUZAA ANAWEZA KUKUPENDA KINAFIKI PIA KAMA RAFIKI AU MTU BAKI TU!. NA HAO AKINA MAMA WA AINA HIYO WAPO.

HILO MOSI, PILI KUSAMEHE AU KUTOSAMEHE NI HIYARI YAKO NA ASITOKEE YEYOTE WA KUKULAZIMISHA USAMEHE, HAKULA LAANA YOYOTE KWA WEWE KUTOSAMEHE, ILA BINAFSI KWA UTASHI WANGU NAKUOMBA UMSAMEHE MAMA ILA USIWE NAYE KARIBU TENA KWA KUMUAMBIA MICHONGO YAKO WALA KUISHI NAYE. HUYO DADA YAKO ENDELEA NAYE KIBABE HIVYO HIVYO.

NB: NI HIYARI YAKO KUSAMEHE, SI LAZIMA. WASITOKEE WACHUNGAJI KOKO KUKUTISHA. SI DHAMBI USIPOSAMEHE PIA SI DHAMBI UKISAMEHE. USIKILIZE MOYO WAKO/NAFSI YAKO.
 
Endelea na maisha yako kimya kimya.. wasiyajue itasaidia na Mama yako asikulilie kuhusu wenzako.. usiringie lolote jionyeshe kama huna unapokwenda.. utaishi kwa Amani kubwa sana
 
Back
Top Bottom