Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Hii ndiyo sababu ya mimi kutokuwa na huruma na Ndugu

Baba yangu alifariki wakati nikiwa Mtoto mchanga hivyo nililelewa na Mama tu naye hakuwa na uwezo Hivyo nilisomeshwa na wasamaria wema. Mtu pekee Aliyekuwa na uwezo wa kiuchumi Ni dada aliyeolewa na yeye hakutaka mazoea kabisa.

Kwa jinsi maisha yalivyokuwa magumu, nilipofika Chuo nikawa natumia boom(mkopo wa elimu ya juu) kumtunza mama. Imagine mtu nilikuwa nalipwa laki tano na kumi na kupaswa niitumie kwa miezi miwili lakini nilikuwa najibana kwa kadiri iwezekanavyo nitumie mama Kati ya elfu 60 na 100,000.

Nilipomaliza chuo nikarudi nyumbani, hakuna ajira na Sina mtaji wa biashara au kilimo, nikawa nashinda ndani kwa mawazo au siku nikibahatisha kibarua Cha zege au kumsafishia mtu shamba naifanya kwa nidhamu, napata hela ya bundle la muendelezo wa kusaka ajira.

Ajabu ya karne; Mama mzazi alianza kunisimangia chakula na kunilaumu kuwa nilitumia vibaya mkopo wa Chuo nilikuwa nawapa makahaba wa mjini na kwamba ningekuwa na akili ningetambua kuwa mimi ni Mtoto yatima na ningetunza akiba ili nimalizapo chuo nifungue kioski!

Mungu siyo Shetani, baada ya miaka miwili ya ukosoefu wa ajira, nikapata kazi nzuri Sana kwenye moja ya taasisi za Kimataifa, nimeanza kusahau yale maisha magumu. Nimewekeza katika ardhi, nimenunua ekari 50, nimenunua viwanja viwili Arusha mjini na kimoja Kibaha. Kwa Sasa nawaza kununua power tiller(KUBOTA) ili inisaidie kwenye kilimo ambacho nitakianza mwakani rasmi.

Sasa nikikumbuka vituko vya mama, na Ndugu kuwatumia hela napata taswira ya yale maneno yale masimango. Naghairisha.

Yule dada Aliyekuwa na uwezo wa kunisomesha akagoma, Benki imewafilisi, wakaachana na mumewe. Amebaki kunipigia simu eti "nilikuwa nakusalimu" wakati kipindi nipo down hakuwahi kunipigia na nikimpigia hapokei simu, nikimpigia kwa number ngeni akishafahamu Ni mimi, anakata.

Maisha ya hapa Duniani ni fumbo
Nimependa hapo ilipomalizia hakika Maisha ni Fumbo hapa Duniani na mwenye majibu ni Mwenyezi Mungu.
 
Um
Maisha ya hapa duniani ni fumbo..
Usimlipie kwa ubaya nawala usimuambie lolote kuhusu aliofanya yeye. ..if you can msaidie ukiona huhitaji mpemakavu ajijue why humpi hii kuoeneana aibu ndio uadui unazidi mpemakavu
 
Wazazi hawalipizwi Kisasi ingawaje wanakosea, endelea kumsaidia Mama kulingana na moyo wako utakavyo.

Saudia pia na Ndugu zako Ila usiwaweke karibu yako. Saidia kulingana na uwezo wako lakini hakikisha hawawi karibu na wewe.
 
kitu ambacho hukijui wazazi na jamii wanahisi chuo tunapewa mamilioni kila mwezi hivyo wakat unampa elfu 60-100 alikuwa anajua unatunza m1 kwa mwezi
kitendo cha kuja huna hata mia, akatafsiri ulikuwa unakula bata tu hivyo akazungumza kwa hasira julisha stress za maisha

ajabu la karne: ni kuona wewe umeyabeba yale maneno ya hasira na stress

kumsaidia mama hatukuombi hili ni lazima, maana amehangaika na wewe na anaweza sema lolote likakukuta (kiimani)

sasa leta ujauaji wako na elimu yako utaona video, naona umemfanya muumba nduguyo kwamba utakuwa na fedha maisha yako yote.
 
All in all chuki, kisasi, roho mbaya, makasiriko humchoma aliye ihifadhi moyoni....😊😊

Niliwai kuishi kama sipo duniani.........Mm ukini negative motivation NDIO ume uwasha moto wa kufanikisha kile nacho kipambania....

Msiache kuongea_Mwana FA Ft Lady jay de....
Huu wimbo ulikua una nipa inspirational words sana kwenye hustle za kujitafutaa.....

Wasalaam

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Unaanzajr kumpiga chini mama. Kuna muda unaacha mengine unaangalia tu yale mazuri mama ni mama maana al8kuwa naye wakati wa dhiki
Alipomsimang sababu ya chakula na kwamba alichezea boom alikuwa siyo mama?Pig chini tu
 
Alipomsimang sababu ya chakula na kwamba alichezea boom alikuwa siyo mama?Pig chini tu
Bado mimi ningemhudumia japo inauma lakini sio kiasi cha kumtelekeza maana mama kama mama mpaka sasa atakuwa ametumia zaidi ya miaka 20 kumtunza jamaa
 
Baba yangu alifariki wakati nikiwa Mtoto mchanga hivyo nililelewa na Mama tu naye hakuwa na uwezo Hivyo nilisomeshwa na wasamaria wema. Mtu pekee Aliyekuwa na uwezo wa kiuchumi Ni dada aliyeolewa na yeye hakutaka mazoea kabisa.

Kwa jinsi maisha yalivyokuwa magumu, nilipofika Chuo nikawa natumia boom(mkopo wa elimu ya juu) kumtunza mama. Imagine mtu nilikuwa nalipwa laki tano na kumi na kupaswa niitumie kwa miezi miwili lakini nilikuwa najibana kwa kadiri iwezekanavyo nitumie mama Kati ya elfu 60 na 100,000.

Nilipomaliza chuo nikarudi nyumbani, hakuna ajira na Sina mtaji wa biashara au kilimo, nikawa nashinda ndani kwa mawazo au siku nikibahatisha kibarua Cha zege au kumsafishia mtu shamba naifanya kwa nidhamu, napata hela ya bundle la muendelezo wa kusaka ajira.

Ajabu ya karne; Mama mzazi alianza kunisimangia chakula na kunilaumu kuwa nilitumia vibaya mkopo wa Chuo nilikuwa nawapa makahaba wa mjini na kwamba ningekuwa na akili ningetambua kuwa mimi ni Mtoto yatima na ningetunza akiba ili nimalizapo chuo nifungue kioski!

Mungu siyo Shetani, baada ya miaka miwili ya ukosoefu wa ajira, nikapata kazi nzuri Sana kwenye moja ya taasisi za Kimataifa, nimeanza kusahau yale maisha magumu. Nimewekeza katika ardhi, nimenunua ekari 50, nimenunua viwanja viwili Arusha mjini na kimoja Kibaha. Kwa Sasa nawaza kununua power tiller(KUBOTA) ili inisaidie kwenye kilimo ambacho nitakianza mwakani rasmi.

Sasa nikikumbuka vituko vya mama, na Ndugu kuwatumia hela napata taswira ya yale maneno yale masimango. Naghairisha.

Yule dada Aliyekuwa na uwezo wa kunisomesha akagoma, Benki imewafilisi, wakaachana na mumewe. Amebaki kunipigia simu eti "nilikuwa nakusalimu" wakati kipindi nipo down hakuwahi kunipigia na nikimpigia hapokei simu, nikimpigia kwa number ngeni akishafahamu Ni mimi, anakata.

Maisha ya hapa Duniani ni fumbo
Hupaswi kulipa kisasi hasa kwa mama yako, mpe huduma bila kuwa na kinyongo naamini utafanikiwa zaidi.
 
Kwa hiyo usiwachukie sana ndg zako,mradi umesha wajua rohoo zao,basi wwe ishii nao kwa akili maana huwezi jua kesho yako hata kama tayari uko vizuri kiuuchumi, Maisha saa yoyote ile yanabadilika,na siyo Kiuchumi tu,hata kiafya!!
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app

Kwani wao wakati nawahitaji hawakujua haya maneno.
Maisha yaleyale walioishi na Mimi nami nitaishi nao hivyohivyo.

#YNWA
 
Jenga moyo wa kusamehe, usieke kinyongo moyoni ama mawazoni mwako, focus kwenye majukumu Yako, ka umchamungu basi 20/50k mtumie mama Kila mwezi,

Ujana unapita tuu. Nawe siku moja utaitwa baby mwenye hekima na maarifa
Kipimo kilekile ulinichonipimia nami nitakupimia.
Nilikuhitaji nikiwa na shida na hukutokea.
Hivyo wakati huu ukiwa na shida usitegemee kuniona.

#YNWA
 
Back
Top Bottom