Ryan Holiday
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 2,026
- 4,450
Peace be upon you Wana JF
Hakuna kitu kizuri kama kushukuru, kusifu na kukubali karama waliyonayo wenzako. Naongea hili Kwa maana ni tatizo kubwa hapa kwetu nikimaanisha kwenye tasnia mbalimbali kwenye uandishi, michezo, muziki na nyinginezo.
Leo hii ndugu zangu tupo hapa tulipo kutokana na kukosa uwezo kushukuru, kusifu na kukubali kipawa na uwezo wa mtu fulani kwenye elimu, uandishi, uimbaji, uchoraji na fani nyingine.
Ntatoa mifano michache kwa wenzetu walioendelea :-
Kylian Mbappe - Football⚽ hadi viongozi wa France wanamkubali na kumpenda kwa kipaji chake na uwezo wake.
Rafael Nadal - Tennis🎾 nyumbani kwao Spain wanamkubali na kumpenda kama tunu ya Taifa.
Shakira - Music🎤 nyumbani kwao Columbia - Bogota ni the same story.
Tyson Fury - Boxing🥊 kwao Uingereza the same story wanamkubali na kumpenda kwenye up's and down's
Lakini ukija kwetu Afrika ni different story mtu akiwa blessed na kipawa fulani akaanza kuonyesha ujuzi wake au fani yake na kuanza kuinuka tunatafuta means yoyote ya kukizima alichonacho. Iwe kazini, maofisini, kwenye siasa, michezo, hata hapa Jukwaani n.k.
Basi Mimi nikaona nisiwe mchoyo wa fadhila bila kushukuru, kusifu, na kukubali vipaji vya uwezo wao wa uandishi na uchanganuaji mambo hapa JF.
1. Da'vinci🏆 🥇🏅🎖️- amekuwa mmoja kati ya watu ambao wameniinspire sana kwa namna ya uandishi wake na uwezo wake wa kuunganisha kati ya science staff na mambo ya dini (Theology), mbali na hayo ni muhumini mzuri wa Ancient stories, Movies (Sci-fi) pamoja na mambo Saikolojia. Thanks Pal'✌️.
Criston Cole
2. Mshana Jr🏆🥈🎖️ - Ni brother mmoja very humble, cool, wise and smarter in the brain. Yeye amejikita sana kwenye siasa, jamii issues na spiritual world. Hakika amekuwa msaada kwangu pindi napokumbana na spiritual issues + mambo ya kijamii hakika naipenda sana hekima yake. Thanks mkuu and Almighty God be upon you 🙏.
3. Mr Excel🥉🎖️ - ni kijana matata niliyesoma bandiko lake kwenye The Story Of Change, likiwa na title ya "Muonekano hutengeneza Uwezekano" na hili ni moja kati ya mabandiko bora kuwai kutokea hapa JF. Asante kwa bandiko zuri na Mungu akubariki sana.
Napenda kuwashukuru pia Wana JF member wote ambao tulidiscuss na kuchanganua mambo mbalimbali kwa namna ya utofauti ambayo yamekuwa very productive kwetu. Napenda kuwatakia heri ya sherehe za krismasi pamoja na mwaka mpya.
Mwenyezi Mungu awabariki sana🙏
Je, tatu bora yako ni ipi? Funguka usikae nalo moyoni!