Lee Van free
JF-Expert Member
- Aug 14, 2024
- 2,833
- 8,777
Tukiwaambiaga hamna akili nyinyi Pro Ukraine msiseme tumewatukana.Siku NATO watatia guu pale Ukraine sidhani kama Urusi itaweza kusimama hata siku moja ikiwa mpaka leo inahenyeshwa na kainchi jirani Ukraine
Ila Pro USA mnashangaza sana.Hii aibu ni kwa Iran, China na Russia
Mbona Trump alikuwa akiyasema sana mkuu au haufuatilii?Hayo ni malengo yako wala sio ya marekani.
Maelezo meeengi yasiyo na maana yoyoteIla Pro USA mnashangaza sana.
Naona haka katukio ni kama vile kamewapa nafasi ya kupumulia kwa jinsi mnavyokashabikia,na hapa itapigwa propaganda kubwa kweli kuonesha kua USA ni mahili sana.
Sasa hapa sijaona uhusika wa Urusi na china katika kitukio hiki maana hii vita sio ya Urusi wala china,of course Nina uhakika Urusi na china wanaisaidia Iran kwa mambo mengi lkn hawajaingiza askari wao kupigana,na wala hawapigani wao.
Sasa sijui aibu hiyo inatoka wapi.
Ni vema ungetuambia hayo mawazo yako ni namna Gani Urusi na china zimepata aibu katika hi hichi kitukio Cha uokoaji ili tuone kama mawazo yako ni sahihi au umewaza pumba TU.
Nyie Pro USA naona mnavyofurahi utadhani huo uokoaji ndio ilikua malengo ya vita hii yote kwa ujumla.
Yaani Sasa sio Tena kuizuia Iran isiwe na nyukilia,
Sio Tena Regime change,
Sio Tena kuzuia Iran isiwe na ballistic missiles,Bali sasa lengo limekua ni kumuokoa rubani.
Wakati katika vita Kuna matukio mengi na makubwa,mengine tunayasikia na mengine hatuyasukii kutoka kwa pande zote.
Kwa uelewa wangu huyo rubani hakuwa tayari amekamatwa na askari wa Iran,alikua amejificha na Kwa kawaida ya marubani wa majeshi makubwa yenye vifaa Bora kabisa alikua ana kifaa Cha mawasiliano ambacho Kiko connected na command center ambacho hakina mafungamano na maadui.
Hivyo waokoaji walikua wanajua location alipo na wanajeshi wa Iran wakishirikiana na raia hawakujua alipo zaidi ya kumtafuta kienyeji.
Laiti kama angekamatwa na Iran ingekua kazi sana kummkomboa na kama wangeweza kumkomboa wangepata maiti.
Hata hivyo uokoaji huo umekua na hasara kubwa badala ya faida kwa sababu ni lazima Kuna askari wa USA waliokufa na Haina ubishi Marekani imepoteza ndege na Helkopta muhimu pamoja na vsilaha nyingine ikiwa picha za mabaki ya ndege tunazoziona ni za kweli..
Hii ni vita ya Iran sio ya Urusi wala china.
Kama ingekua vita ya Urusi na china dhidi ya USA ,USA wala asingejisumbua kuingia ndani ya ardhi ya Urusi ama china kujaribu kutaka kuokoa mtu wao.wangehusisha diplomasia.
Na hata Iran,bahati Yao USA waliwahi kufikia eneo la tukio,laiti wangechelewa kidogo TU, uokoaji usingefanikiwa.
Sas hebu tuangalie hasara,je USA imepata faida au hasara kwa maana ya vifaa ilivyopoyeza na je hakuna hata mwanajeshi mmojabwa USA aliekufa ?
Navyojua uokoaji kama huo hufanywa na makomando sio wanajeshi wa kawaida. Je kupoteza commando mmoja kwa kwa ajili ya kuokoa rubani mmoja Kuna faida au hasara? Maana kumtrain special forces mmoja wa USA navy seal au delta force,au us Marine hakuna tofauti kubwa sana na kumtrain rubani.
Tuangalie kabla ya rubani ndege yake kushambuliwa ndege ngapi ziliangushwa na Irani,
pia tuangalie katika zoezi la uokoaji ndege ngapi zilitumika na ngapi zilipigwa.
Je jumla ya ndege zote katika kadhia hii ni ngapi jumla zilizopigwa?
Maelezo meeengi yasiyo na maana yoyote
Ni upumbavu kuamini Iran inanguvu kijeshi na ulinzi kwa nchi yake ilihali imepoteza viongozi wote wa juu kwa mpigo na bila upinzani wowote na wao wasiweze kuuwa hata balozi wa nyumb
Wewe unaakili kisoda mkuuKwanza nilikupuuza kwa sababu niliona uko mtupu kichwani na huna elimu,lkn nikaona nikikuacha hivihivi utawapata wengi mazuzu kama wewe.
Iko hivi sera ya Iran sio kuua Viongozi wa nchi nyingine,lkn sera ya Israel na USA ni kuua Viongozi wa nchi nyingine.
Usidhani kuwavizia na kuwaua Viongozi wa nchi nyingine ni kazi sana hapana.imawezekana TU.
Rais wa USA JF Kennedy na Waziri Mkuu wa Israel Shimon Perez waliwahi kuuliwa Kwa risas na wahuni TU,kwa hiyo watu wakipanga inawezekani.
Sio Siri kwa miaka mingi Israel iliwekeza katika kuua Viongozi wa maadui zake.
Iran haikuwekeza huko Bali iliwekeza katika kujilinda.
Kumbuka kuua Viongozi wa n chi nyingine sio sifa nzuri,lkn ma komando au majasusi wa Israel wakiua Viongozi wa nchi nyingine West,wewe na wajinga wenzako mtasifia sana na kusema ni kitendo Cha mafanikio Cha majasusi wa Israel au USA,
lkn ikitokea majasusi au makomando wa Palestine, Hizbola au Iran au nchi yoyote msioipenda wakiwaua Viongozi wa nchi nyingine wewe na wajinga wenzako mtaita ni tukio la kigaidi.
Hivi wewe kwa akili zako huoni hata aibu kua nchi mbili kubwa kabisa hapa duniani katika medani za vita na hata uchumi kwa pamoja zinapigana na nchi moja TU halafu wewe unaiona nchi hiyo ni dhaifu?
Hivi kama ingetokea zikapigana nchi mbili TU Israel na Iran, Israel ingetoboa kweli?
Ikiwa USA TU analalamika kua Dunia imemuacha peke yake,NATO hawataki kumsaidia,je Israel inaweza peke yake?
Hivi unajua USA kabla ya vita hii iliwadanganya Iran kua siku tatu zijazo mazungumzo yataendelea,Hali hiyo ilimfanya Ayatollah na wenzake wakawa na amani kua tuko kwenye mazungumzo waka relax ndipo USA na Israel wakavamia na kuwaua?
Huoni katika diplomasia huo ni uhuni?
Kwa kifupi kama Iran au taifa lolote wakiamua nao kuogopa kuitwq magaidi na kuwekeza kuua Viongozi wa wenzao haitashindikana.
Kama unajua kua magaidi walivamia USA wakateka ndege Tano za abiria wakazibamiza kwenye majengo muhimu ya Marekani pamoja na Pentagon na kufanikiwa kuua makamanda wa jeshi wengi TU.
Je inashindikana Nini?
Ok USA na Israel walipoanza vita TU wakamuua Ayatollah na wenzake je Nini wamefanikiwa?
regime change imetokea?
Tafakari.