Hii ni aibu, tunatakiwa kubadilika. Msaada wa Waziri Wang Yi ni fedheha

Hii ni aibu, tunatakiwa kubadilika. Msaada wa Waziri Wang Yi ni fedheha

Bado sijasikia kubwa aliloafikiana kuhusu maslahi ya nchi. Nadhani ametoa hiyo hela ndogo kama sehemu ya kupunguza joto la sura za kutaka msaada wa ujenzi wa SGR na SG. Ni makubaliano gani yenye tija kaingia kwenye hiyo safari yake? Maana China ya sasa sio ya enzi za Mao, japo awamu hii wanadhani China hii ni ya kijamaa.
Nasikia kuna fununu, mchina kujenga Sgr,Isaka to Mwanza.
 
Taifa ombaomba haliwezi kuwa na sustainable development hata siku moja,hizo kauli za sisi ni matajiri nizakijinga sana.
 
Sidhani kama kuna mtu kakatazwa kuchangia, so long as kuna nafasi ya kufanya hivyo changia tu.
 
Bado sijasikia kubwa aliloafikiana kuhusu maslahi ya nchi. Nadhani ametoa hiyo hela ndogo kama sehemu ya kupunguza joto la sura za kutaka msaada wa ujenzi wa SGR na SG. Ni makubaliano gani yenye tija kaingia kwenye hiyo safari yake? Maana China ya sasa sio ya enzi za Mao, japo awamu hii wanadhani China hii ni ya kijamaa.
Dogo tulia soon utakuwa unatoka Dar mpaka Mza kwa treni la umeme.
 
Jamani imefikia wakati kama watanzania tunatakiwa tubadilike.

Kupokea msaada wa milioni 380 ni aibu kwa taifa tajiri kama hili.

Milioni 380 iliyotolewa na waziri wa Mambo ya nje wa China ni fedheha kwetu.

Hii pesa ilipaswa kuchangwa na wafanyabiashara wa dhahabu Katoro na kuikabidhi kwa Veta Chato, sio kutolewa kama msaada na waziri wa taifa kubwa kama China.

Tusipende kudhalilishwa kwa misaada midogo kama hii. Hata kama unatakiwa usichague cha kupewa,lakini inatakiwa tufikie hatua tuchague.

My take; Tuwe makini sana juu ya misaada kama hii,ikumbukwe huko nyuma babu yetu Sultan Mangungo alishawahi kubugi na ikawa fedheha kwa watanzania.
Misaada wanatowaga wazungu sio wachina ni wabahili kweli kweli. Mchina anatoaga mikopo sio misaada
 
Chadema ndio maana Mimi niliapa kuwa sikubali mshinde niko tayari hata kukimbia na box la kura msaada ni msaada huwezi mpangia tajiri akupe nini hivi nyie chadema mlishatoa hata mlo mmoja kulisha walemavu?
Ahahahaaaa [emoji3][emoji23][emoji1787][emoji85]. Kumbe ndiyo mliokimbia na mabox . Wachawi wa usiku hujitaja mchana
 
Chadema ndio maana Mimi niliapa kuwa sikubali mshinde niko tayari hata kukimbia na box la kura msaada ni msaada huwezi mpangia tajiri akupe nini hivi nyie chadema mlishatoa hata mlo mmoja kulisha walemavu?
Usiwe lofa..nyie ndo malofa aliyewasema RIP Ben.

Kisa msaada tu basi unyooshe mkono hata kama ni wa dharau?

Hivi unajua msafara wa Rais unagharim kiasi gani kwa siku?

300m kitu gani kwa Taifa lenye utajiri wa kila kitu.

2Trillion kwa mwezi,afu 300m iwe habari.
 
JNHP itakuwa imekamilika,unaposema hakuna tatizo la usafiri una maana gani? Mbona unatia aibu?

JNHP itakuwa imekamilika, una uhakika gani wakati ni pesa ya mkopo? Kuna shida gani ya usafiri kati ya Mwanza, maana mabasi ya kumwaga.
 
JNHP itakuwa imekamilika, una uhakika gani wakati ni pesa ya mkopo? Kuna shida gani ya usafiri kati ya Mwanza, maana mabasi ya kumwaga.
Dogo mbona unatia aibu vijana wako wa ufipa? Umesahau wewe ni kamanda mkuu? Sababu kuna mabasi kibao ndio watu wa Mza hawahitaji gharama nafuu? Hujui cement kwa sasa ni karibu elfu 20 kwa mikoa ya kanda ya ziwa? Hujui treni itapunguza gharama za usafiri na kupoza bei za bidhaa?
 
Nyie lopolopo mno hadi hamjui mnachotetea, endeleeni tu kulamba kwato za beberu huku mkizuga pesa za ndani!
 
Back
Top Bottom