SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
TFF imeipa onyo kali klabu ya Yanga kutokana na kitendo cha viongozi wake akiwemo Rais wake Hersi Said kuingia uwanjani na kupiga zogo na wachezaji wa Singida Black Stars baada ya mechi iliyochezwa hivi karibuni baina ya timu hizo mbili.
Kitendo hicho kilichofanywa na viongozi hao wa Yanga kinaleta tafsiri na viashiria vya upangaji wa matokeo na ukaribu unaohatarisha ushindani wa kweli wa timu shiriki katika ligi ya NBC.
Hivi kwa nini TFF wamekuwa wanaipa tu onyo timu ya Yanga na kushindwa kupata tafsiri sahihi ya matendo haya ya Yanga ili kuchukua maamuzi sahihi?
Miezi michache iliyopita waliipa onyo kama hili klabu ya Yanga kutokana na kitendo cha Mkurugenzi wao wa Ufundi kukaa kwenye benchi kwa mechi 3 kinyume cha kanuni. Yanga ilipombadilishia kazi na kuwa kocha msaidizi ndiyo TFF ikawapa onyo wakati wameshachelewa.
Na hivi onyo ni adhabu?