TFF yampa onyo kali Rais wa Yanga Hersi Said
TFF imeipa onyo kali klabu ya Yanga kutokana na kitendo cha viongozi wake akiwemo Rais wake Hersi Said kuingia uwanjani na kupiga zogo na wachezaji wa Singida Black Stars baada ya mechi iliyochezwa hivi karibuni baina ya timu hizo mbili.

Kitendo hicho kilichofanywa na viongozi hao wa Yanga kinaleta tafsiri na viashiria vya upangaji wa matokeo na ukaribu unaohatarisha ushindani wa kweli wa timu shiriki katika ligi ya NBC.

View attachment 3247012

Hivi kwa nini TFF wamekuwa wanaipa tu onyo timu ya Yanga na kushindwa kupata tafsiri sahihi ya matendo haya ya Yanga ili kuchukua maamuzi sahihi?

Miezi michache iliyopita waliipa onyo kama hili klabu ya Yanga kutokana na kitendo cha Mkurugenzi wao wa Ufundi kukaa kwenye benchi kwa mechi 3 kinyume cha kanuni. Yanga ilipombadilishia kazi na kuwa kocha msaidizi ndiyo TFF ikawapa onyo wakati wameshachelewa.

Na hivi onyo ni adhabu?
Kwenye maelezo yako umetaja habari ya upangaji wa matokeo! Cha kushangaza kwenye maelezo ya TFF, wametoa sababu nyingine kabisa.
 
Maelezo ya mweka mada na maelezo ya TFF ni tofauti kabisa!, kwa kuzingatia uhuru na ukweli wa habari nashauri huu uzi ufutwe ama urekebishwe kutokana na kile kilichoandikwa!.

kwenu moderators JamiiForums Active
 
Kwenye maelezo yako umetaja habari ya upangaji wa matokeo! Cha kushangaza kwenye maelezo ya TFF, wametoa sababu nyingine kabisa.

Maelezo ya mweka mada na maelezo ya TFF ni tofauti kabisa!, kwa kuzingatia uhuru na ukweli wa habari nashauri huu uzi ufutwe ama urekebishwe kutokana na kile kilichoandikwa!.

kwenu moderators JamiiForums Active
Para ya kwanza nimetoa taarifa nikaambatanisha na chanzo cha taarifa halafu nikatoa na maoni yangu. Kwani siruhusiwi kutoa maoni yangu kisa nimeleta taarifa?

1000054574.jpg
 
Viongozi wa Yanga walikuwa wakiingia uwanjani ndo maana 5imba alofungwa mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imewapa onyo kali Viongozi wa klabu ya Yanga kwa kosa la kuingia kwenye eneo la kuchezea (pitch area) katika mchezo uliowakutanisha Yanga dhidi ya Singida BS baada ya mchezo kukamilika.

Viongozi hao wa klabu ya Yanga walioingia uwanjani walisababisha kukosekana kwa utulivu wakati wa mahojiano ya mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga.

Chanzo Taarifa: mpenjatv

Najua mnawaogopa kwakuwa kuanzia TFF na nyie TPLB 99% yenu mpo katika Payroll ya GSM na mnaneemeka nao sana.
 
Back
Top Bottom