Hii ni moja ya picha ambazo Waingereza hawapendi kuziona

Hii ni moja ya picha ambazo Waingereza hawapendi kuziona

Idd Amin alikua mbabe, mwenye kiburi na majivuni, lakini bado akaitwa Dada...



Cc: mahondaw
 
Aliitisha mkutano wa wafanya biashara na maofisa wa ubalozi wa Uingereza. Akaamrisha wambebe
Hii si kweli hata kidogo. Tamasha hii ilipangwa na Bob Astles. Astles alikuwa Mwingereza aliyebaki Uganda baada ya ukoloni akashiriki na serikali ya Obote na kuendesha biashara zake. Alimwoa Mganda kutoka ukoo wa kifalme. Alikuwa na shamba la mananasi. Amin aliposhika utawala 1971 akamtupa gerezani, akamwachisha baadaye. 1975 Amin alimtaka mshauri kwa mawasiliano na nchi za nje akamchagua Astles. Astles alijitahidi sana kumbembeleza Amin kwa kila namna.

Wakati Amin alichaguliwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (aibu juu ya madikteta wote wa Afrika waliompa kura!) kulikuwa na party. Kwenye nafasi hii Astles alitisha wafanyabiashara Waingereza walioishi Uganda wambebe Amin mbele ya wageni wa Umoja wa Afrika. Baadaye aliamuru idadi ya Waingereza waliokuwa wafanyabiashara Uganda wapige magoti mbele ya Amin. (kwa nini waliitikia? ).

Astles alikuwa hodari kumbembeleza Amin. Alihukumiwa naye hadi mauti mara nne lakini alifaulu kila safari kumbembeleza tena. Baada ya uvamizi wa Tanzania pale Uganda na kurudishwa kwa Obote Astles alitupwa tena jela kwa miaka 4 au 5, hatimaye aliachishwa akarudi Uingereza....

Kuhusu siku zile ambako Astles alipowalazimisha Waingereza wenzake kumbeba Amin, askofu Mwanglikana Mganda Festo Kivengere aliandika: "At the very moment the heads of state were meeting in the conference hall, talking about the lack of human rights in southern Africa, three blocks away, in Amin torture chambers, my countrymen's heads were being smashed with sledge hammers and their legs being chopped off with axes."
Bado unataka kusheherekea picha hii???

(halafu: si kweli Waingereza hawataki kuona picha hii jinsi unavyodai kwenye kichwa cha habari. Bila shaka ilionyeshwa zaidi huko kuliko Tanzania)
 
1129522
 
1129523

Mafanikio mengine ya Bob Astles yaliyomsaidia kuhifadhi kichwa chake (Amin alipenda kuamuru vichwa vijunjwe kwa nyundo)
(na hao waliopiga magoti kuendelea na biashara zao pale Uganda kwa miezi kadhaa - pesa ni hamasisho kali)
Menginevyo si kweli Amin aliwafanya madiplomat Waingereza kupiga magoti - lkn alifaulu kuwalazimisha watambae... Alimhukumu kifo mwalimu mmoja Mwingereza wa Makerere; London walituma wawakilishi kumwona Amin. Amin aliwapokea katika kibanda waliponyeshwa tu mlango wa chini kiasi walilazimishwa kuingia kwa kutambaa. Walikubali kwa sababu walikuwa na amri kumrudisha raia wao akiwa hai. Amin aliona ni ushindi mkubwa!
Kweli?
 
Kuna zilizoongezwa chumvi lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa jamaa huyu alikuwa mtata.

Ipo interview yake mwenyewe anaelezea jinsi atakavyoipiga Israel..sasa mwenyewe waweza kupata picha alikuwa Mtu wa aina gani.
Kwani kuelezea kuipiga Israel kuna ubaya gani?!
...America kila siku wanaelezea jinsi watakavyoiipiga Iran mbona haujalalama...au ndio mabwana zenu Israel hawapigiki ?!
 
Hio Cip yake ilimuudhi wakwanza mzee mnafik Nyerere kwasbb alijikomba saana kwa waingereza,***** Iddi Amin alikuwa mwanaume lkn kwa unafik wa kamzee mchonga wakaanza kumpakazia “Oohh dikteta’” Oohh anaua wananchi wake “ohh anatawala kimabavu
Hakujuona yeye Huyo mzee mchonga alitawala miaka mingapi Tz[emoji38]hadi kakaambiwa mzee achia vingenevyo,,,,[emoji3]
Wakati Amini hakutawala hata miaka mi5
Papo hapo kamzee mchonga hakakujiona kalivotaifisha mali za wananchi wake na kuidudimiza uchumi wa nchi yake kwa kuwatuhumu watu wake wahujumu wa uchumi
Tena kawashkuru hao wazungu vingenevyo vita vya Uganda maji yalikua shingoni[emoji3]kalishazidiwa saana lkn mabeberu A,k,A Wahisani wakampiga tafu[emoji3]
 
Hio Cip yake ilimuudhi wakwanza mzee mnafik Nyerere kwasbb alijikomba saana kwa waingereza,***** Iddi Amin alikuwa mwanaume lkn kwa unafik wa kamzee mchonga wakaanza kumpakazia “Oohh dikteta’” Oohh anaua wananchi wake “ohh anatawala kimabavu
Hakujuona yeye Huyo mzee mchonga alitawala miaka mingapi Tz[emoji38]hadi kakaambiwa mzee achia vingenevyo,,,,[emoji3]
Wakati Amini hakutawala hata miaka mi5
Papo hapo kamzee mchonga hakakujiona kalivotaifisha mali za wananchi wake na kuidudimiza uchumi wa nchi yake kwa kuwatuhumu watu wake wahujumu wa uchumi
Tena kawashkuru hao wazungu vingenevyo vita vya Uganda maji yalikua shingoni[emoji3]kalishazidiwa saana lkn mabeberu A,k,A Wahisani wakampiga tafu[emoji3]
Amin alitawala miaka nane Uganda. Si uongo Amin aliua wapinzani na watu waliokuwa tishio kwake.

Mjomba wa rafiki yangu alikuwa masomoni Uingereza wakati Amin anaingia madarakani. Baba yule alisoma PhD ya Horticulture. Alipo rudi alikuwa mmoja wa maofisa waandamizi wizara ya kilimo.

Siku moja kwenye kikao aipishana na rais kwenye sera za kilimo. Baada ya kikao akiwa anarudi nyumbani. Kilichomuokoa ni kuwa mtoto wa dada wa mkewe alikuwa usala was taifa. Alimwambia mama yake mdogo amkimbize Baba mdogo mara moja nje ya nchi anauwawa usiku wa Leo.

Mama mdogo alikodi tax mumewe akiwa kwenye booth ya gari mpaka wanavuka mpaka wa Kenya.
Walikimbilia Uingereza ambako yule Baba alipata kazi Trinidad.
 
Back
Top Bottom