Ndugu Masamila, je unajua kusoma? Nilisema wapi kitu kuhusu CIA?
Nimeleta chanzo chenyewe,
taarifa rasmi ya serikali ya Uganda kuhusu sensa ya 2014. Milioni 34 waliulizwa maswali na pale wanaulizwa pia dini (tofauti na TZ). Maana
asili ya data ni wananchi wenyewe jinsi wanavyojibu. Na
takriban asilimia 14 walijibu "Mwislamu". Je unataka kusema pale Uganda Waislamu wengi sana ni waoga wanaoficha dini yao na kujiita Wakristo?
Halafu kama ungesoma kweli tovuti
www.muslimpopulation.com ungeona mawili tofauti:
1. makadirio ya 30+% ni namba ya mufti aliyehisi walikuwa na Waislamu milioni 6 mwaka 2002. (fungua "reference" katika jedwali) Hakuonyesha chanzo yaani wapi alichota idadi hii. Kumbe miaka 18 badaye ni milioni 4 tu wanaojitambulisha kuwa Waislamu katika taifa lililokua. Je hii tofauti ya milioni mbili walikufa bila kuzaa, wamekuwa Wakristo, wamesahau Uislamu wao? Uwezekano mkubwa ni shehe alihisi tu bila uhakika.
2. Halafu soma tovuti ileile hapa
:
"According to the National Census 2002 Islam is practiced by 12.1 percent of the population "
Kumbe ni tovuti ambyo si makini kuhusu namba. Maana sehemu moja wanataja asilimia 30+, penginepo wanataja asilimia 12.
Nakushauri utafute vyanzo halisi, usiamini mambo unayokuta kwa sababu unapenda habari fulani, lakini chungulia kwa akili ya ukosoaji. Lakini ni Shauri lako!