Hii ni tafsiri ya maendeleo kutoka Kwa lazern muisraeli aliyeishi sana Cameroon,

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
"watu duni kifikra hudhani ujenzi wa miundombinu ni maendeleo, yaani barabara, reli, madaraja, hayo sio maendeleo ni mahitaji ya eneo husika tu"
Hayo hapo juu ni maneno ya rafiki yangu mmoja kutoka moja ya nchi zilizoendelea na katika maongezi aliendelea kueleza yafuatayo.
Mtazamo wa maendeleo hutofautiana pia kulingana na mazingira, Kwa mfano nchi ili iendelee lazima iwe inauwezo wa kufanya gunduzi mbalimbali ikiwamo gunduzi za huduma ambapo zile huduma zitategemewa na kuingiza kipato cha fedha ya kigeni,
Maendeleo ni uwezo wa kuzalisha bidhaa na uweze kuwauzia wengine ili wewe upate pesa, akasema hata elimu za nchi maskini bado zinafifisha fikra na kua duni,
Niliwaza kumbe Kwa karne ya leo kusimama unasema umejenga barabara, madaraja, matundu ya vyoo kuna watu huko duniani wanakua wanakucheka bila wewe kufahamu,
 
Zanzibar tunafanya Marekebisho ya Elimu na Ubunifu. Tulieni muone maajabu
 
Hapo kwenye elimu amenigusa. Ndio maana huwa nasema hakuna umuhimu wowote wa kulipa mamilioni ili mwanao asome English Medium shule ya msingi kwa sababu hiyo elimu inayo tolewa haina thamani inayo endana na hiyo hela.
 
Mfumo wa elimu yetu bado hadi leo watoto wanafundishwa majimaji war utegemee tuendelee, innovation ndio maendeleo yamelala huko lakini bado hatuoni
 
Reactions: I M
Mfumo wa elimu yetu bado hadi leo watoto wanafundishwa majimaji war utegemee tuendelee, innovation ndio maendeleo yamelala huko lakini bado hatuoni
Kabisa ndio maana hakuna sababu yoyote ile kulipa mamilioni kwa ajili ya shule za English Mediums
 
Hapo kwenye elimu amenigusa. Ndio maana huwa nasema hakuna umuhimu wowote wa kulipa mamilioni ili mwanao asome English Medium shule ya msingi kwa sababu hiyo elimu inayo tolewa haina thamani inayo endana na hiyo hela.
Kivip mkuu unasema elimu inayotolewa haina thamani ya hiyo hela
 
Hapo kwenye elimu amenigusa. Ndio maana huwa nasema hakuna umuhimu wowote wa kulipa mamilioni ili mwanao asome English Medium shule ya msingi kwa sababu hiyo elimu inayo tolewa haina thamani inayo endana na hiyo hela.
Dogo hili swala la English medium umelikomalia humu. Vipi binti yako wa miaka 16 anaendeleaje? Mzima? Bado unamwachiaga aende kwa boyfriend wake kuomba vitabu vya kujisomea?
 
Atakae kupinga hana akili tena hana akili

Huwezi kutaka kuendelea bila kua nahayo majambo hayo uloyataja na mfano wake

Ukiwa na hayo mambo by nature yatafanya maendeleo yaje yatarahisisha usafiri nk

Wao wenyewe huko kwenye hii miundo mbinu wapo vizuri ila wanataka kutuaminisha sisi kua sio maendeleo

Halaf kuna watu wanamuona jamaa kaongea yamaana kumbe mwamba kaongea unafiq tuuu
 
Ukitaka kujua miundombinu ni maendeleo ishi sehemu ambayo imekosekana
 
Ni sawa na mtu kujenga nyumba ya kuishi sio maendeleo
 
Are We Serious??? Yani Mpaka leo baso tunalalamika tu kuwa hatuendelei kisa kikiwa ni Wazungu. Yani tangu tupate Uhuru ni Miaka takribani 63 Bado tunalalamika juu ya Ukoloni Mamboleo.

Kwa kifupi sisi Waafrika na hao Viomgozi ndio tuna Matatizo. Tujiulize, Wachina waliwezaje Kujikwamua? India Waliwezaje kujikwamua? Ok hata North Korea naye anapambana hatujifunzi kwake?

Kwakifupi Sheria za kidemokrasia ndio zimetufikisha hapa. Ni wakati wa kibadili Mfumo wa Uongozi Afrika. Demokrasia hatuiwezi kwetu. Pia tuweke Sheria Ngumu kama ya Kunyongwa Kwa Wahujumu Uchumi/Mafisadi hapo ndio tutafanikiwa, hata kama Taifa litakuwa linaishi Kwa kutegemea misaada.

Hiyo misaada itafumika vizuri naadeni yatalipwa vizuri.

Libya lilikuwa Taifa Pekee Afika lililowahi kuwepo bila Madeni ya Wamagharibi kipindi cha Muamar Gaddafi, hatujiulizi Waliwezaje?

Inasikitisha kiukweli....
 
Kabisa hao majamaa wakikwambia sasa hivi mchana toka nje ukahakikishe kama kweli

Majamaa wanafiq waongo wazushi waharibifu na umesema kweli jamaa nlitaka kumwambia kwakua kasema mweupe ndio anasema ukweli

Watu weupe kiukweli ilitakiwa hata huko kwetu tuwafukuze wanafiq wauaji washenzi haswaaaa
 
1. Maendeleo ya Kiuchumi na Miundombinu ya kiuchumi
2. Maendeleo ya Kisiasa
3. Maendeleo ya kijamii na huduma za kijamii

Miundombinu kama madaraja, majengo NI sehemu ya maendeleo katika uchumi.
 
Si kila mwisrael aaminiwe kwa kila aongeacho hata kama ni utumbo, Waisrael wengine ni weupe tupu kushinda hata wabongo wa bonyokwa

Huyo jamaa yako kaongea pumba tupu

Maendeleo ili yaje, yanahitaji kiwezeshi cha kutafikia

Mfano mzuri ni namna Mungu alivyoanza kuumba ili kuja kumweka mwanadamu aishi kwenye miundombinu iliyokuwa wezeshi kwake

Kulihitajika kuwepo na miti ili ije imsapoti kufikia lengo la yeye kuishi kwa raha duniani, kulihitajika kuwepo maji, kuwepo jua, kuwepo aridhi, kuwepo samaki n.k

Hiyo yoote ni miundombinu wezeshi kwa mwanadamu

Na huo ndio mwelekeo sahihi na kichocheo cha kuendelea (Maendeleo)
.
JPM yule alikuwa akili kubwa!

Huyo jamaa mwisrael na wote wanaomuunga mkono ni wajinga tupu!

Hatuwezi kuwa na Elimu bora bila ya kuwepo miundombinu bora wezeshi

Kwa maana nyingine ni kwamba, Miundombinu ndiyo maendeleo ya Kweli
 
Umesoma ukaelewa views tofauti ya maendeleo kulingana na karne hii na karne ya zamani au zilizopita, na nini dunia Kwa sasa inakimbia nacho, au hata hauelewi kwamba tafiti za mars kama kutakua na maisha au lah huelewi zina maana gani?
 
Nichoona hapa kuna watoto vichwa maji sana
 
Hapo kwenye elimu amenigusa. Ndio maana huwa nasema hakuna umuhimu wowote wa kulipa mamilioni ili mwanao asome English Medium shule ya msingi kwa sababu hiyo elimu inayo tolewa haina thamani inayo endana na hiyo hela.
Ukiwaambia huu ukweli wanakua wakali sana. Imekua fashion tu. Mbaya zaidi wazazi wengi uwezo huo hawana ila wanajibana sana mpaka kukopa ili mtoto asome huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…