Hii ni Yanga sio Simba, maana ya Kikosi kipana ndio hii! Hakuna Pacome, Aucho na Yao, unatoa sare na Mamelodi iliyokamilika kila idara

Hii ni Yanga sio Simba, maana ya Kikosi kipana ndio hii! Hakuna Pacome, Aucho na Yao, unatoa sare na Mamelodi iliyokamilika kila idara

Mamelody wenyewe wameogopa walichokiona na vile wanajua goli lolote la yanga ndani ya Pretoria kwao ni maumivu basi hofu inapanda ila yote kwa yote Yanga anaenda semi tena kirahisi sana
 
Mkuu mpira unakusumbua possession waliyoipata mamelodi ni kipa kumpa pass nyingi beki Kekana mara unaenda kwa Moosa Lebusa unarudi kwa kipa Williams ulitaka hapo Yanga wafanyeje watu wanamiliki mpira ndani ya zone yao wakitegemea pass za kupenyeza ambazo nyingi waliblock wakina Bacca...Yanga wamejituma sana jana wacha waende wakapambane tena huko SA...
Usitumie nguvu nyingi kumuelimisha aaiyetaka elimu hiyo. Ni hivi Yanga sc anavuka hatua hii mtake msitake. Tunza hii comment mwanakwetu achana na hao Simbilisi waliojaa choyo na wivu kwa Wananchi tz
 
Sasa mnajisifia nini wakati mmecheza mpira wa hovyo namna hiyo.
Mpira wa hovyo wakati kipa wa Mamelod ndio anaongoza kwa kufanya saves nyingi?
Mpira wa hovyo wakati Yanga imeongoza kwa shots on target?
Jana ilikuwa imechezwa mpira wa mbinu, pamoja na Mamelod kuumiliki sana mpira kakini wamelazimishwa mipira mingi wachezee eneo lao.
Yanga wamefaulu kupata clean sheet kuruhusu goli la ugenini ni msala kwa hatua hii.

N B
Timu zote hazijaruhusu goli la ugenini kwenye first leg kasoro Simba peke yake.
Yanga 0 Mamelod 0
Tp Mazembe 0 Petro Luanda 0
Es Tunis 0 Asec 0
 
Weka akiba ya maneno. Kucheka na kulia vyote vimeumbwa
Nyie hamkuweka akiba ya maneno mpaka mkasahau mechi yenu na kushadia mechi ya Yanga lwamba anapigwa,mkijipa matumaini Al Ahly kaisha eti mnamjua na mlivyo pangia kuanzia viongozi wenu mpaka mashabiki walio alikwa waliruka na kushangilia au mlisahau kuweka akiba za maneno. Ila mlicho kutana nacho mlikiona na pale Al Ahly key player watatu majeruhi.
 
Sasa mnajisifia nini wakati mmecheza mpira wa hovyo namna hiyo.
Tumecheza mpira wa ovyo wewe uliyecheza mpira mzuri ulifunga ngapi dhidi ya Aly ahly? Unafikiri hii ni group stage kwamba ni marathoni? Hizi hatua za robo fainali zinachezwa kwa akili na sio kimihemko, mbinu ndizo zinatawala na sio chenga twawala kufurahisha mashabiki ndio maana mmekuwa mwakarobo mechi za mtoano mnacheza Kama mnacheza ligi ovyo kabisa!
 
Narudia tena weka akiba ya maneno. Sote tumeangalia mechi zote, droo yenu Yanga isiwape jeuri kiivyo ni bad game plan ya Mamelod tu ingawa bado ukiniambia kati ya Mamelod na Al Ahly kwenye michuano hii, Al Ahly wako juu.
Nyie leo ndio mnaijua akiba,sasa hapa mlipo shangilia baada ya kupangiwa na Al Ahly mlikuwa hamna hiyo akiba ya maneno?

View: https://m.youtube.com/watch?v=bwBTWSJNSjU&t=304s
Baada ya hapo mkaanza matusi kwa Yanga,mtazani mshafuzu.
 
Makolo ndo timu pekee iliyokandwa hatua ya kwanza robo fainali...wanatia aibu kwakweli.
 
Halafu kuna mtu mmoja asiyejua mpira anajiita Danielmwasi anamkosea heshima huyu kocha.
Huyo jamaa -Dany- laiti ingetokea tungefungwa jana, basi leo angekuja kufungua nyuzi kibao za kukanyagia na angepata wafuasi.

Cha ajabu mpaka muda huu sijasoma hata comment yake moja kutoka kwenye post yoyote ile.

Hiyo maana yake yupo kwenye kukosoa tu, huyo ni shabiki mpuuzi.
 
Ndio ball possession iwe 75 kwa 25 kweli?
Mbumbumbu Kuna kazi pale mangungu anatakiwa aifanye sio bure, ball possession Haina maana yoyote Kama auna madhara kwa mpinzani wako, Mamelod pamoja na kuwa na ball possession kubwa akuna madhara yoyote waliyoyafanya kwenye lango la yanga, short on target yanga alikuwa na 4 wao 2, njia zao zote zilifungwa, ikiwa na maana yanga ndio walikuwa na nafasi kubwa kuibuka na ushindi, mechi hizi za mtoano zinachezwa kwa akili na sio mihemko ndio maana mkapigwa na Aly ahly Kisha wakawaachia mpira mlipokuwa mnavuka mstari wa kati mnakosa option wanakabia kwenye low block mnakwama mnarudi kuchezea mpira kwenye zone yenu kitu ambacho akikuwa na madhara kwao, na Mamelod walifanya Ivyo ivyo mipira mingi wamecheza kwenye zone yao maana walishindwa namna ya kuipenya ngome ya yanga iliyokuwa inakaba mpaka kivuli!
 
Labda tuwakumbushe haya mashindano ni mtoano hivyo ulitakiwe utunze AKIBA ya maneno mpaka mmemaliza mechi ya nyumbani na ugenini.
Uliwaona mamelody walikuwa Kama wako mazoezini, wao ndio walikuwa wanaamua yanga wacheze namna gani?
 
Huyo jamaa -Dany- laiti ingetokea tungefungwa jana, basi leo angekuja kufungua nyuzi kibao za kukanyagia na angepata wafuasi.

Cha ajabu mpaka muda huu sijasoma hata comment yake moja kutoka kwenye post yoyote ile.

Hiyo maana yake yupo kwenye kukosoa tu, huyo ni shabiki mpuuzi.
Anaishia kusoma comments tu, jamaa ana chuki mbaya sana dhidi ya Gamondi sijui ni mshabiki wa timu pinzani hivyo kaona ni kikwazo au sijui ni kipi anachogombea dhidi ya Gamondi
 
Anaishia kusoma comments tu, jamaa ana chuki mbaya sana dhidi ya Gamondi sijui ni mshabiki wa timu pinzani hivyo kaona ni kikwazo au sijui ni kipi anachogombea dhidi ya Gamondi
Gamondi kawa bingwa na Mamelodi miaka ya 2006 huko nianze kumsoma mtu asiejua mpira hata chembe kisa ana Tecno pop 2 anaweza kuingia JF...
 
Labda tuwakumbushe haya mashindano ni mtoano hivyo ulitakiwe utunze AKIBA ya maneno mpaka mmemaliza mechi ya nyumbani na ugenini.
Uliwaona mamelody walikuwa Kama wako mazoezini, wao ndio walikuwa wanaamua yanga wacheze namna gani?
Awakucheza Kama wako mazoezini kwa kutaka walilazimishwa wacheze vile muwe na heshima na mbinu za makocha, wewe kwa uelewa wako uliona vile but master gamond alizifunga njia zao kwa mbinu, Mamelod ubora wao na nguvu yao ipo katikakati kwa viungo wao, ivyo gamond aliweka lock ya maana na walishindwa kupitia kati kati wakawa wanafanya kuwavuta yanga kwao ili wapige mipira mirefu iwakute kina shalulile yanga wakiwa wamevutika kushambulia, lakini yanga awakuingia kwenye mtego wao wakabaki kucheza pasi nyingi kwao ambazo azikuwa na faida yoyote Wala madhara kwa yanga, wamemiliki mpira lakini wamemiliki asilimia kubwa kwenye zone yao awakuwa na option ya kuleta madhara kwenye lango la yanga, short on target yanga 4 wao 2 so what???
 
Back
Top Bottom