Hii picha imenihuzunisha sana, nani wa kulaumiwa?

Hii picha imenihuzunisha sana, nani wa kulaumiwa?

Huyo mtoto mwenyewe ndo mchoyo,aombe Mungu babake aondoke naye,endapo atamuacha hapo hayo makwenzi atakayopata,siku nyingine akiletewa atawagawia nakwambia.
ndo maana methali inasema ''asiyefunzwa na babaye,hufunzwa na ulimwengu''

Mtoto WA Baba mwenye uchumi Mkubwa Kuliko wengine uliona wapi akipigwa makonzi?
 
Jamaa amemtembelea mwanae ambae Mamake amezaa na wanaume watano tofauti, kamnunulia vitamu yeye peke yake huku wengine wakila kwa macho.

View attachment 3295696
Binafsi kama mwanaume/Baba naona jamaa hajafanya sahihi, ni heri angewanunulia wote au angemchukua mwanae akakae nae sehemu afanye yote anayojisikia kumfanyia mtoto kisha amrudishe kwa wenzake kuliko kuwasulubisha kwa makosa yasiokuwa yao

Ni nani wa kulaumiwa hapa?

Hao watoto Baba Zao nao waende wakatoe zawadi kwa watoto wao.

Huyo Baba yupo Sahihi Sana.
 
Huyo dogo janja unamtwisha msalaba mzito sana mkuu
Watoto siyo wachoyo kama hawajafundishwa uchoyo.

Wakulaumiwa ni mama yao seems kuna wakati huwa anawafanyia hivyo ikitokea baba wa mmoja wao amempa mahitaji yake kwa kauli kama “nyie subirini na baba yenu aje awanunulie” akijua anawakomoa waliomzalisha kumbe anawatenganisha watoto,mbaya kabisa hii na mwanamke kwanini anazaa kama mbwa?watoto watano kila mmoja baba yake?
 
Hahaha umesema kwel mkuu

Yaani mtoto wako asile vizuri Kisa ujamaa?

Huyo Mamaake kama anawaonea huruma watoto wake awanunulie chakula

Kama alitaka umoja angezaa na mwanaume Mmoja.
Hakunaga umoja katika Jambo kama Hilo.
Hapo wanasubiri wakue kila Mmoja aende kwenye ukoo wake.
 
Ujamaa ni njia ya kipumbavu sana katika kufanikiwa ,yani wewe ulaze akili mimi nitumike ili wewe ufaidi🤔
 
Ujamaa ni njia ya kipumbavu sana katika kufanikiwa ,yani wewe ulaze akili mimi nitumike ili wewe ufaidi🤔

Uteseke wewe tule wote. Acha uchoyo wewe!

Mtoto aache kujivinjari na Babaake Kisa watoto wenzake?
Au Baba aache kufurahia na mtoto wake kisa Kuwafurahisha watoto wa mwanaume Mwenzake.

Matokeo ya Umalaya lazima yasapotiwe ili iwe funzo
 
Ningekua raisi ningepiga marufuku watu kuzaa kama hawana kipato , hii ni mbaya kwa muskakabadhi wa maisha ya mtoto baadae🤔
 
Ningekua raisi ningepiga marufuku watu kuzaa kama hawana kipato , hii ni mbaya kwa muskakabadhi wa maisha ya mtoto baadae🤔

Ukose nguvu Kazi ya kuitumia?

Hao Maskini wanaozaa ndio tunapata cheap Labour Mkuu.

Ukiona serikali haiingiilii Jambo ujue inanufaika aidha direct or indirect
 
Back
Top Bottom