Hii picha imenihuzunisha sana, nani wa kulaumiwa?

Dah, kazalishwa na watu 4 na yeye kaona aende kupanga foleni? Haki ya nani aisee.
 
Sasa watoto wanashida gani?
 
Huyo baba bado ana utoto hajakomaa akili..

Kama unajua kuwa mwanao ana ndugu zake wa4 anaishi nao, kuwanunulia wote vitu wakafurahi kwa pamoja ni moja ya njia ya kufanya maisha yawe ya amani kwao,, Yaani hapo tayari ameshamtengenezea mtoto kamtimanyongo yeye na wenzake..

Pamoja na yote maisha ni connectionn na undugu wa mama una nguvu kuliko wa baba.. Hatujui yajayo, tuishi kwa kuitengeneza kesho ..
 
Hii picha nilliona zamani sana, wala sio ngeni na ilikuwa na Habari tofauti na hii ya kusema mama alizaa na washikaji kibao

Waswahili wawekee picha tu

Mwakani ataileta mwingine na kusoma Mtoto wa kigogo kaenda kuomba kura na mwanae kijijini
 
Watoto si wake awanunuie ili iweje, kosa ni la huyo Mama kuzaa na vibaka na ndilo kosa kubwa ufanywa na wanawake wengi hapa mjini. Mtu anajizalia tu bila hata kufikiri maisha ya huyo mwanae yatakuwa vipi wakati mwanamme aliyezaa naye anaonekana kabisa si ridhiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…