Hii picha inatuambia nini? Kwamba Tanzania is full of nepotism? Rais na mkwe wake wanaweka jiwe la msingi!

Hii picha inatuambia nini? Kwamba Tanzania is full of nepotism? Rais na mkwe wake wanaweka jiwe la msingi!

Hii ni michawa kama kawaida ndiyo inamsifu Rais kwa kujenga barabara wakati anatumia kodi za wananchi kujenga hiyo barabara. Nchi hii ina mijitu ya ajabu sana aisee!
Kwa hiyo ulitaka ajenge barabara kwa kutumia majani? Kama anatumia kodi zetu kujenga barabara na kukamilisha vizuri kwanini tusimpongeze kwa kutumia vizuri kodi zetu kwa ustawi wa Taifa letu?
 
Hakuna upendeleo hapo.Mh mchengerwa ni mchapa kazi sana tena sana na ndio maana alipotolewaga utumishi uliona namna watumishi wa umma walivyo bubujikwa machozi ya uchungu ,kwa kuwa ni wakati wake ambapo watumishi wa umma walikuwa wanasikilizwa sana na kutendewa haki na kutatuliwa kero zao kwa haraka sana.
Mkuu usitetee utwana na uzandiki kwa sababu ya maslahi yako binafsi ghairi ya maslahi ya taifa. Kuwa mzalendo kwa taifa lako na adabu kwa raia wenzako.
 
Mkuu usitetee utwana na uzandiki kwa sababu ya maslahi yako binafsi ghairi ya maslahi ya taifa. Kuwa mzalendo kwa taifa lako na adabu kwa raia wenzako.
Narudia kusema kuwa kama mtu ni mchapa kazi kama mh mchengerwa sisi watanzania tunamhitaji sana katika serikali yetu ili atusaidie watanzania kama ambavyo mh mchengerwa amekuwa akitusaidia kila eneo ambalo amekuwa akipewa na kuaminiwa kuongoza wizara. Uhusiano wake na mh Rais kindugu haumnyimi nafasi ya kulitumikia Taifa lake
 
Kwa hiyo ulitaka ajenge barabara kwa kutumia majani? Kama anatumia kodi zetu kujenga barabara na kukamilisha vizuri kwanini tusimpongeze kwa kutumia vizuri kodi zetu kwa ustawi wa Taifa letu?
Elewa ninachokisema mkuu. Rais hazifiwi kwa kujenga barabara bali machawa (kama wewe) humsifia kwa kutoa hela za kujengea; utadhani hizo hela anazitoa mfukoni mwake.
 
Elewa ninachokisema mkuu. Rais hazifiwi kwa kujenga barabara bali machawa (kama wewe) humsifia kwa kutoa hela za kujengea; utadhani hizo hela anazitoa mfukoni mwake.
Lazima apongezwe na kusifiwa maana kuna wengine wakikusanya hata kuzitoa tu hawezi na badala yake abaziweka tu benki kana kwamba ni mali yake.mwingine anaanza hadi kuzitapanya hovyo hivyo kwa matumizi yasiyo na tija wala matokeo chanya katika maisha ya watanzania.wengine anafanya kama alivyofanya mobuti seseseko kujenga majumba ya kifahari Ufaransa ambayo aliyaacha yote baada ya kufariki
 
Vitu vingine vidogo vidogo kama hivi sioni hata sababu ya kuvidiscuss humu jf !
Kwani kuwa na Mkwe au mtoto au mume katika shughuli yeyote ya kijamii au ya kitaifa unayoifanya kuna kosa gani hapo ??!
Yupo Rais humu Africa alimteua mke wake kuwa makamu wa Rais 😅🙏
Huyo mkuu nyankurungu2020 ni masalia ya sera za JPM, atatafuta chochote kinachoiponda awamu hii na kuiweka juu ile ya hayati.
 
Vitu vingine vidogo vidogo kama hivi sioni hata sababu ya kuvidiscuss humu jf !
Kwani kuwa na Mkwe au mtoto au mume katika shughuli yeyote ya kijamii au ya kitaifa unayoifanya kuna kosa gani hapo ??!
Yupo Rais humu Africa alimteua mke wake kuwa makamu wa Rais 😅🙏
Na mwingine kateua watoto wake wawili ni mawaziri,sio tatizo, shida ni kuwa hivi vyeo vinapatikana kwa kujuana wala sio kwa uwezo wa mhusika, kingekuwepo chombo cha mchujo wa hawa watu sidhani kama wangebahatika kupata hizo nafasi.Mfano unajua unajua tuanalisha wanaukoo wangapi wa familia ya kikwete na Mwinyi?
 
Nepotism ilikuwa ya Dotto James na JPM Ilikuwa ni ile ya kujaza watoto wa wajomba na wa kaka zako kwenye halmashauri za nchi hii.

Nepotism ilikuwa ni ile ya kumuweka Paul Makonda kuwa RC wa Dar, kijana mdogo aliyekosa busara na hekima ya kuongea mbele ya watu.

Afrika yetu hii na hata huko USA huwezi kuikwepa nepotism. Cha muhimu ni huyo anayepewa kuendesha nchi awe anaifanya kazi yenye matokeo yanayoonekana,
 
Back
Top Bottom