Hii picha kuna kitu hakiko sawa: Mzee George Mkuchika amesimama vijana wamekaa

Si alikuwa waziri asiye na wizara maalum,huenda wenye viti ni ni wenye kazi maalum🙂
mi ndo maana naona ukifikisha umri wa kustaafu ni bora ustaafu ili kulinda heshima yako.
 
Inaonekana mzee ni mnyenyekevu kwake ameona kusimama si shida,
Ila waliokaa wote hawana adabu au walijisajau
 
Mnadhimu Mkuu Lukuvi. Iko sahihi picha.🙏🙏🙏
 
Baraza lijalo inafaa wakina mama wapewe wizara nyingi zaidi za kuongoza.
 
Lakini kuna kipindi Raisi Samia alisema Vijana tuwapishe wazee kwenye viti hasa kwenye usafiri wa umma. Imekaaje hapo mbona vijana hawajampisha Mzee Mkuchika kukalia kiti?

Au ile kauli ilitulenga sisi vijana tusio kuwa viongozi wa Chama na Serikali?
Mzee Mkuchik.a ni askari mkakamavu msimuomee huruma
 
Hicho sio kikao cha ukoo hapo wamekaa kulingana na vyeo vyao sijui ulitaka akae kwa nani hapo?
Wengi hawamfahamu mzee George Mkuchika.
Ni mzee, kwanza alianzia kazi ya ualimu na baadaye kwenye siasa.
Nilimfahamu kupitia Mwalimu wangu aliyeitwa Chiwile ambaye sasa ni marehemu,
Mzee Mkuchika hana makuu,
Miaka yote hana scandal,
Hana kujikweza pamoja na utumishi wake ulio tukuka,
Aliwahi kuwaonya watu wenye madaraka wawe na kiasi,
Mzee Mkuchika ni mcha Mungu

Hao vijana waliokaa sasa .......

Kuna wenye fleet za mabasi,
Kuna wennye maghorofa kadhaa nchini,
Kuna weneye wake wengi kama mfalme Daudi,
Kuna wenye ukwasi wa kutisha pamoja na kwamba ni awamu zao za kwanza uwaziri.

Neno linasema;

Ayubu 12 : 12
12 Wazee ndio walio na hekima, Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.


Wananchi tuna wafahamu viongozi wetu.
 
mwalimu ni babake, yeye alikuwa mjeda aliwahi kuwa PEO wetu pale Ruvu jkt, he was a very smart guy
 
Sio kwenye picha tuu, na CCM kuna vitu havipo sawa, serikalini kuna vitu havipo sawa, kinchi kuna vitu havipo sawa na kitaifa pia kuna vitu havipo sawa.
 
Hao hawafai kukaa katika viti wote wanabidi wakae katika mkeka au nyasi hakuna wanachofanya hapo
 
Raia wa nchi gani? kuna mpaka Waarabu na Wahindi(ambao ni raia) kwenye mfumo.
 
Kwa huo mkao ni itifaki imezingatiwa na siyo suala la Mkuchika kuwa wa siku nyingi Ikulu. Hapo ni mpangilio wa kiitifaki tu na siyo blah blah unayotaka kutuchafulia bongo zetu hapa.
 
Mleta uzi acha blah blah, huo mkao ni wa kiitifaki (umezingatia seniority order ya kimadaraka kulia na kushoto mwa Mhe. Rais Samia).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…