Hii sasa dharau, yaani mimi wa kunialika mahafali ya mtoto wa chekechea? Kweli?

Huwezi jua ndio ukawa sherehe yake kwanza na mwisho.....maisha yanaenda mbio...zama hizi nenda tu mfanyie kama ni wako au mjukuu..
Huyu bwana NIMEONA aseme tu kama hana hela, na hasira za kukosa hela anajidai zimetokana na kualikwa kwenye sherehe ya mwanachekechea kumaliza uchekechea wake..!! Hivi ingekuwa yanafanyika hayo, si tungekuwa wote tunasubiria ile degree ya mwisho ndo tufanye sherehe..!!??? Maana kila level kuna ya juu yake ambayo ina mambo yasiyopatikana kwenye hii ya chini..!!
 
Mimi kwangu sherehe ni upumbavu kwani HATA HARUSI YA KAKA YANGU WA DAMU SIKWENDA leo naambiwa mchango wa get together kazini nikitoa waniite mbwa
Sherehe ni upotevu wA rasilimali mda na pesa tu,, hazinaga maana😁
 
Nimenuniwa na Shoga angu kisa sikwenda kwenye Graduu ya Mtoto wake alimaliza Chekechea,

Na mie namwambia nuna upasuke sikua na muda wa kupoteza [emoji57]
 
Huu ujinga ndo maana tunashindwa hata kuwa inventive,angekuwa amebuni mbinu ya kutengeneza umeme kwa kutumia matawi ya miti hapo ikulu popo ingekuwa mashiko,wtz ni hope the opposite
 
Sherehe ni upotevu wA rasilimali mda na pesa tu,, hazinaga maana😁
Kuna mjeda aliefukuzwa Kazi kafanya harusi ya m26,mimi hapo nikatamani nione fuso Barabarani,ila haya maisha ya foma ya ajabu sana
 
Na Leo graduation zilikuwa nyingi πŸ˜‚πŸ˜‚
Mimi Sina mtoto wa kugraduate ila wazazi wa shule nzima tulialikwa, ni vile tu NIMEONA una ajenda zako ila ni RAHA sana ukiwaangalia watoto kwenye functions kama hizi.
Mungu akupe wepesi
Amiina, labda nitaelewa
 
Jamaa yangu ameambiwa achangie mchango wa 30000 kwa ajili ya sherehe ya mtoto kamaliza chekechea.
Na wanaohangaika na huo ujinga wengi ni wanawake.
Kabisa, wanahangaikia kweli hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…