..Lissu ametetea WANANCHI dhidi ya serikali na makampuni ya madini.
..harakati hizo ndizo zilizomtia ktk matatizo na serikali za Mkapa, Kikwete, Magufuli, pamoja na makampuni ya madini.
..kwenye " mgogoro " wa Barrick / Accacia na Magufuli, na uwasilishaji wa ripoti za uchunguzi, Lissu alitetea UKWELI.
..Mtu yeyote aliyeshughulisha akili zake asingeshindwa kuona kwamba ripoti na taarifa za serikali zilijaa UPOTOSHAJI /PROPAGANDA.
..Lissu alionya kwamba taarifa zile sio za kweli na tukichukua hatua kwa kuzifuata NCHI itaingia gharama kubwa kwa kushindwa kesi.
..UKWELI umeanza kujulikana kwa jinsi serikali inavyoshindwa kesi moja baada ya nyingine.
..Watu kama Prof.Mruma, ambao Magufuli aliwaamini mpaka akawapa vyeti vya utendaji wa kizalendo, wamekwenda mbele ya mahakama za kimataifa na kushindwa kutetea nchi.
..Kwenye kutetea rasilimali ni wachache ambao mchango wao unajulikana na WANANCHI / WENYEJI wa maeneo husika.
..Wenyeji wa maeneo ya Bulyankulu, Nzega, Geita, North Mara, wanamtambua Lissu kama mtetezi wao. Hahitaji kujisafisha machoni mwa jamii hizo.