Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
TAARIFA KUHUSU BIMA ZA WAGOJWA KUKATAA KUWA AUTHORISED KWENYE MFUMO

Utaratibu wa mfuko wa NHIF umebadilika ili kuzuia polyvisit za wagonjwa pamoja na polyservices zingine za wagonjwa wetu

Kuanzia sasa mteja atakua na nafasi ya VISIT 3 TU KWA MWEZI kwa kituo husika na mteja hawezi kujiamulia kuhama Kituo cha kutolea huduma(Hosp,H/na disp) moja kwenda nyingine kwa kujiamulia, mfano mgonjwa akianza kutibiwa Kituo X basi atakua wa X tu mpaka pale X tutakapo amua sisi mrefer mgonjwa kwenda sehemu nyingine la sivyo mgonjwa hataweza kwenda sehemu nyingine , kama kuna emergency kutakuwa kuna utaratibu kwenye mfumo wa kuruhusu huduma ziendelee

Aidha mfuko utaweka pia utaratibu wa wale wagonjwa ambao ni wa refill ili kama amekuja kwa ajili ya refill asiweze kuchomekea kitu kingine cha kimatibabu

Kwa huduma za physio, meno kutawekwa utaratibu maalumu ili huduma kama hizo ziendelee

Mfuko unataka kubana wale wa watu wanaozunguka kila kituo kufanya vipimo, kuona madaktari na kulinganisha huduma za madaktari

Ni hayo tu ndugu zangu,muwe ka kazi njema.

Watu wa mapokezi mutakua munawaelekeza kwa upole wateja ambao kadi zao zimepata changamoto hizo.

NHIF.
 
Habari za mchana wapendwa.

Habari za kusikitisha - NHIF wamebadilisha mifumo yao ya matumizi ya card.

1- Tegemezi wengi wameondolewa,

2- Card itumike x 3 tu kwa mwezi.

3- Kama umetibiwa Jana au juzi, ukienda hospitali nyingine utatakiwa uende na Referral toka hiyo hospitali ulikotibiwa mara ya mwisho.

Makorokoro kibao yamebadilika. Tunaendelea kuwasikiliza. Ni shida tupu.


HII SIO HAKI MTU ANACHANGIA AFU HUDUMA ANAPANGIWA ATIBIWE KTK KITUO KIMOJA TU KWA MWEZI NA NA MARA TATU TU KWA MWEZ HII SIO HAKI. BASI WATUMISHI WARUHUSIWE KUJIUNGA NA MIFUKO MINGINE ISIWE LAZIMA NHIF ILI AFUATE HUDUMA SEHEMU ANAYOONA INAFAA
 
... kero ni nyingi sana kwenye huu mfuko. Unakatwa mshahara wako kwa lazima kulipia NHIF ila kama huna mtoto wa kumzaa huruhusiwi kuweka ndugu (mfano unayemlea); nafasi zako 4 (kama ungekuwa na watoto) zinakuwa zimekwenda bure faida kwa mfuko. Ukiuguliwa na huyo ndugu itakubidi kuingia gharama za matibabu yake ilhali kwenye mfuko una nafasi ambazo hutakiwi kumsajili.

Pili, watoto wote uliokuwa umewasajili wameshavuka 18/21; kwanini mwanachama huyu asipate nafuu ya makato? Badala yake makato yake yanabaki yaleyale. Tatu, badhi ya huduma muhimu zimepunguzwa; ukosefu wa baadhi ya dawa hivyo mhusika kulazimika kuingia mfukoni, n.k.
 
Kwa hilo napinga Tena napinga kwa asilimia zote hi sio haki...NI heri wanitoe kwenye mfuko wao hela yangu iingie kwenye take home.nianze mazoezi na kunywa maji waone Kama nitakwenda hospitali zao..huu NI uzembe Sana na uonevu
 
Imeanza lini mkuu, maana juzi nilienda dispensary nikatibiwa, sikuridhika na matibabu, Jana nikaenda Aghakan nikatibiwa fresh Tu wala hawakudoubt kama nimeshatibiwa within 24hrs
 
Kuna official public announcement kwenye hili?
Kama kuna ukweli au urongo, ni Bora mfuko ujitokeze kutoa ufafanuzi na kutoa naelekea ili isilete sintofahamu kwa wagonjwa.
Kuna baadhi polycyclic ziko karibu na makazi ya wagonjwa na zinafanya kazi mchana na usiku zinafunga, vip kama mtu anaugua usiku na anahitaji kwenda kwenye polyclinic ambayo inatoa saa 24?

Au ndio wanataka kuwa na CHF ambayo mtu akitoka ndani ya Wilaya haifanyi kazi?
What if mtu akasafiri nje ya eneo kazoea kutibiwa na akaugua??
 
Nashangaa viongozi wetu wanajipangia maamuzi yasio natija kabisa leo, eti limetoka tamko kwamba wenye bima wanatakiwa kutibiwa mara tatu tu kwa mwezi. Huu ni upungufu wa akili. Acheni ujinga. Unampangia Mungu mtu kuumwa vip kuhusu wale wenye celebral palsy CP vip kuhusu wale wenye matatizo ya Figo.
 
Back
Top Bottom