Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Kama itakuwa ya kweli, kwa mtazamo wangu itakuwa na mapungufu makubwa kwani watakuwa wamejiamulia bila kuwashirikisha wadau muhimu hasa wafanyakazi ambapo ndio wanaoendesha mfuko kwa michango yao. Suala linalo husu Afya/maisha ya watu, linahitaji mjadala makini bila kuweka faida ya mapato mbele.
Ilikua ya kweli
 
TAARIFA KUHUSU BIMA ZA WAGOJWA KUKATAA KUWA AUTHORISED KWENYE MFUMO

Utaratibu wa mfuko wa NHIF umebadilika ili kuzuia polyvisit za wagonjwa pamoja na polyservices zingine za wagonjwa wetu

Kuanzia sasa mteja atakua na nafasi ya VISIT 3 TU KWA MWEZI kwa kituo husika na mteja hawezi kujiamulia kuhama Kituo cha kutolea huduma(Hosp,H/na disp) moja kwenda nyingine kwa kujiamulia, mfano mgonjwa akianza kutibiwa Kituo X basi atakua wa X tu mpaka pale X tutakapo amua sisi mrefer mgonjwa kwenda sehemu nyingine la sivyo mgonjwa hataweza kwenda sehemu nyingine , kama kuna emergency kutakuwa kuna utaratibu kwenye mfumo wa kuruhusu huduma ziendelee

Aidha mfuko utaweka pia utaratibu wa wale wagonjwa ambao ni wa refill ili kama amekuja kwa ajili ya refill asiweze kuchomekea kitu kingine cha kimatibabu

Kwa huduma za physio, meno kutawekwa utaratibu maalumu ili huduma kama hizo ziendelee

Mfuko unataka kubana wale wa watu wanaozunguka kila kituo kufanya vipimo, kuona madaktari na kulinganisha huduma za madaktari

Ni hayo tu ndugu zangu,muwe ka kazi njema.

Watu wa mapokezi mutakua munawaelekeza kwa upole wateja ambao kadi zao zimepata changamoto hizo.

NHIF.
Ushauri wangu ni kwamba baada ya nhif kusitisha matumizi ya fomu 2C ambao ilikuwa uamuzi mzito na drastic, wangejipa muda walau kipindi cha miezi 6 ili kutathmini matokeo yake kabla ya kuibuka na mageuzi mapya haraka.
Ushauri wa pili ni kwa nhif kuweka mgumo wa kielectronic kuwawezesha madokta kutambua matumizi mabaya ya huduma zao hasa madawa. Kwa mfano mgonjwa akipewa dawa za panadol leo iwe ni rahisi kutambua iwapo kesho yake ataenda hospitali nyingine kwa tatizo linalohitaji dawa ya panadol.
Kama nhif wana kitengo cha IT ni budi wawatumie vijana wao vizuri badala ya kutuletea sera mbovu kwawagonjwa wasio na kosa.
 
Sawa kuna fraud
Ila heri mngeweka watu/task force ya ku'confirm na wagonjwa kama kweli walitumia huduma flani kuliko kunyima watu huduma

Ukiweka utaratibu wa kuconfirm kila claim or atleast on a sample basis kuendana na risk za kituo then utajua tu wapi kuna loophole afu utadeal na wahusika

Ile strategy ya msg nayo ni nzuri sana
 
Ushauri wangu ni kwamba baada ya nhif kusitisha matumizi ya fomu 2C ambao ilikuwa uamuzi mzito na drastic, wangejipa muda walau kipindi cha miezi 6 ili kutathmini matokeo yake kabla ya kuibuka na mageuzi mapya haraka.
Ushauri wa pili ni kwa nhif kuweka mgumo wa kielectronic kuwawezesha madokta kutambua matumizi mabaya ya huduma zao hasa madawa. Kwa mfano mgonjwa akipewa dawa za panadol leo iwe ni rahisi kutambua iwapo kesho yake ataenda hospitali nyingine kwa tatizo linalohitaji dawa ya panadol.
Kama nhif wana kitengo cha IT ni budi wawatumie vijana wao vizuri badala ya kutuletea sera mbovu kwawagonjwa wasio na kosa.
Yees
Data analytics zitawaonyesha vitu flani
Mbona CAG aliona wanaume wana operation za uzazi😅
 
Hii je?
FB_IMG_1659536586630.jpg
 
Imeanza lini mkuu, maana juzi nilienda dispensary nikatibiwa, sikuridhika na matibabu, Jana nikaenda Aghakan nikatibiwa fresh Tu wala hawakudoubt kama nimeshatibiwa within 24hrs
Aga Khan wanapokea NHIF standard au unatumia supplementary?
 
Ushauri wangu ni kwamba baada ya nhif kusitisha matumizi ya fomu 2C ambao ilikuwa uamuzi mzito na drastic, wangejipa muda walau kipindi cha miezi 6 ili kutathmini matokeo yake kabla ya kuibuka na mageuzi mapya haraka.
Ushauri wa pili ni kwa nhif kuweka mgumo wa kielectronic kuwawezesha madokta kutambua matumizi mabaya ya huduma zao hasa madawa. Kwa mfano mgonjwa akipewa dawa za panadol leo iwe ni rahisi kutambua iwapo kesho yake ataenda hospitali nyingine kwa tatizo linalohitaji dawa ya panadol.
Kama nhif wana kitengo cha IT ni budi wawatumie vijana wao vizuri badala ya kutuletea sera mbovu kwawagonjwa wasio na kosa.

Kwa mtazamo wangu,
kama watu wanafanya hivyo inamaana kunatakiwa research; namaanisha kama kweli from Doct A to Doct B kuna majibu mengi yasiyo endana/yaliyokinyume, basi kuna tatizo mahala pengine kwenye vipimo nk wanatakiwa walifanyie kazi; Ila kama majibu angalau 85% yanaendana, wanachama wanahitaji kuelimishwa
 
Kwan si ilikua ukitunia kad huwez tena kpaka ipite masaa 24.
Vip kwa mfano nimetumia kadi katika hospital specialises katika dental tu? Na ndan ya muda huo nikaugua ikanibid niende katika hospital ambayo inatoa huduma za OP je italazamika kwenda hospital ya dental pekee ndan ya miez hio m3?
 
Hawana majibu
 
Bora iwe ya kughushi maana kama ni kweli tutaandamana
Hamna uwezo wa kuandamana kwani hamko hivyo tangu huko nyuma. Shukuru tu "siasa" zimeshalipoza jambo lenyewe ila kiuhalisia NHIF wataendelea nalo baada ya kimya kupita kidogo. Nchi hii ina vigego ni balaa!
 
Huna hoja kwa kuwa leo nipo morogoro na najisikia kuumwa niitaebda hospital hapo morogoro. Baada ya wiki nikasafiri kwenda Dodoma nikajiskia kuumwa nitaenda tena hospital, baada ya wiki mbili nikaenda dar na nikajiskia kuumwa si ntaenda tena hospital?

Sio haja ya kuweka limit, kwa kuwa so far nachojua wanaotibiwa ni wachache kuliko ambao hawatibiwi. Kuna watu wana miaka minne hawajui hospitali ipoje. Huyo nae utasema arudishiwe oesa yake ya miaka minne?
[emoji23][emoji23][emoji23] acha utani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli wewe ni nyumbu uliolamba asali ukashiba. Fikiria kwa kichwa sio makalio. Wafikirie watu ambao wana CP na matatizo ya figo ambao wanatakiwa kwenda kuhudhuria clinic mara 3 na zaidi. Kuna hospitali zingine huduma zao ni mbaya hazikizi mahitaji utaenda hapo hapo tu? Muhimbili yenyewe rubbish huduma yake ni chini ya kiwango. Kama wewe umezikuta kwa Baba ako na Mama ako wengine atujazikuta tunafight kwa nguvu zetu.
Ndugu unataka utest dialysis kila hospitali [emoji23][emoji23][emoji23] sasa hiyo ni shopping

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi ni ya kifala kabisa huu upoyoyo huyu mother f ndio kauleta yani mambo yanaendea kifala kweli.
Huyu waziri ndo tatizo kila siku matamko kama chiriku yeye anajua labda kila mtu anatembezwa na VX kama yeye
 
Yani bora ummy kajitahidii... nape anaambia vifurushi vimepanda sana anasema GHARAMA ZA MAISHA LAZIMA ZIPANDE.
 
Back
Top Bottom