Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Hivi serikalini huwa wanakata asilimia (%) kwenda NHIF maana bima ya afya kwa watumishi wa serikali inatibu magonjwa mengi kuliko hizi bima za vifurushi kama wanavyoziita na ukute mtu amelipia 600,000 (laki 6), huwa najiuliza serikalini huwa wanalipa zaidi kiasi kwamba hizi za vifurushi zinapewa hadhi ya chini
 
Kingekuwa na vyama huru na kweli vya wafanyakazi, hii kitu ingeondolewa mara moja. Mfanyakazi anakatwa asilimia tatu ya mshahara wake kuchangia NHIF hzlafu unampangia idadi ya siku za kuugua kwa mwezi? Nikatwe maelfu kila mwezi kisha nikalipie matibabu kisa tu kwa,mwezi huo tayari nimeenda hospitali mara tatu! Fikiria mtu ameenda hospitali anaambiwa apime vipimo na kwa kuwa amekula asubuhi basi siku hiyo hawezi kupimwa vipimo fulani hivyo aje kesho; siko inayofuata anakuja na kupimwa anaambiwa aje kuchukua vipimo siku inayofuata, akija siku ya tatu na kuchukua majibu na akimwona daktari anakuwa amemaliza siku tatu anazoruhusiwa kutu.mia bima yake anayokatwa pesa kila mwezi; hivyo kama asipopata nafuu hawezi kurudi tena hospitali baada ya siku chache katika mwezi huo huo upuuzi ulioje? Mtu huyo huyo akisafiri nje ya mji anapoishi kama likio@ kikazi na akaugua huko alikoenda hawezi kutibiwa na bima yake anayokatwa kila mwezi.

Ufumbuzi ni kuwa sheria ya ku.lazimisha mfanyakazi kuchangia NHIF ifutwe na wafanyakazi waruhusiwe kuchagua bima inayowafaa na kujiunga.

NHIF wana.pangia mwanachama siku za kuugua kwa mwezi!
 
Hali ni mbaya sanaa kila kiongozi anamua anachotaka, kule mafuta, pale tozo,huku mitandao na sasa hawa wapuuzi tena, nchi haina kiongozi mkuu inakwenda kwenda tu.
 
... nadhani kutokana na wigo wa wateja kuwa mdogo ndio maana za vifurushi ni ghali. Ila huenda za serikali zisingekuwa LAZIMA badhi ya wafanyakazi wange-opt za vifurushi hivyo kuongeza wigo hence reduced cost.
 
Mkuu kumbe nssf ni mara tatu tu kwa mwezi? Nilikuwa sijajua hili, niko nao mwaka wa tatu sasa,20 tu kila mwez
 
Watawala nyie mtaiharibu nchi hii.Watu wanaugua.
 
Bado wale wa mabando, wanajiona miungu watu
 
Wacha tukachague hospital zenye hadhi basi ili wawe wanapapaswa vizuri hamna kwenda kule kwa wakulima.

Hapa gongo la mboto nafanya utafiti kati ya rugambwa au kitonka nikite kambi wapi.
Kitonka ni ya mtu binafsi nasikia, na halipi vizuri wafanyakazi. Rugambwa ni ya dini, wala huhitaji hata kufaulu chekechea kujua wapi pa kukomaliza for the better future
 
na mtu anayemaliza mwaka bila kuugua wanamfidishia vipi?
 
Taarifa kwa umma
 
Tayari asali tamu wamejisahau kuwa watu wanakatwa mishahara.asali tamu.wakitimuliwa wakuu kama watatu utaona ufanisi
 
Baada ya taharuki kwa wanachama,wizara ya afya imeweka zuio kwa utaratibu huu mpya uliowekwa na NHIF
 
Mbona NSSF siku zote tuliambiwa kuchagua hospitali moja tu katika eneo unaloishi utakako tibiwa, na tuliendelea hivyo unless unakiwa referred hospitali nyingine na haijawa tatizo?
 
Mbona NSSF siku zote tuliambiwa kuchagua hospitali moja tu katika eneo unaloishi utakako tibiwa, na tuliendelea hivyo unless unakiwa referred hospitali nyingine na haijawa tatizo?
Watu hapa wanaongelea NHIF (mfuko wa taifa wa Bima) unaochangiwa hela kutoka kwenye mishahara ya wafanyakazi na sio NSSF ambayo wameamua kutoa zawadi ya bima ya matibabu kwa wanachama wao (ukipewa zawadi huwezi kuchagua/kudai); ila ukilipia huduma, unahaki ya kushirikishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…