Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Ishu naona ni TAARIFA za mapema.

Ukitaka kwenda kusalimia au kumtembelea Ndugu hakikisha unatuma taarifa.

Ila ndugu wengi wanapanda Bus, wakiwa njiani ndio wanakwambia tunakuja.

Muda huo hujafanya any pre arrangements zozote, na bahat mbaya haupo sawa mfukoni au tyr una mgeni mwingine.
 
Kwa kweli mke Ni pambooo...mume wangu aliwahi washushuaa ndugu zakee kuhusu mavazi yanguu...siwezagi kuvaa matenge Mimi nikiwaa home ni mwendo wa pensi na simple dress..sasa waoo mkewwee kashindikannaaa😄😄😄😄aliwasuuzaa
 
Atakuwa anakaa porini kweli, wale wa masaki hawanaga nongwa hizo
 
Ila kuna watu wana roho ngumu sana kuhusiana na hawa ndugu wanaokuja pasi na kutoa taarifa. Jamaa anawauliza " Je, mlisikia mimi naumwa?" "Hapana tumekukumbuka sana ndo maana tumekuja kukusalimia". "Ok, kwa vile sasa mmekuja na mmeniona nipo mzima, basi kesho asubuhi na mapema mjiandae kurudi mlikotoka".
 
Tuwe wanyenyekevu tunapopata mafaniko tusione wengine ni takataka hawafai.
Ukifa ndio watamfariji mkeo na watoto wako
Huu ujinga tu yaani nife halaf ndugu wamfariji mke na wtt uliona wapi!? Kitu pekee cha kuwafariji mke na wtt wake ni kuwaachia msingi mzuri wa miasha tu

Sent from my PRA-LA1 using JamiiForums mobile app
 
Kirimu wageni toka mkoa ndugu yangu acha ubahili.
 
Mimi nimewahi wakataria kaka zangu wawili ambao tunashibana sana,na wana mchangu mkubwa sana kwangu kufika hapa nilipo,mmoja anawatoto 7 na bado anazaa nikimuuliza unazaa watoto wanini ilihali hawa waliopo huwapi mahitaji muhimu!?,oooh nimlete Fulani aje asomee huko,Mimi hapana maana watoto wanaweza tugombanisha,kama ni msaada nitawasaidia wakiwa huko,maana hata huko kuna shule.

Siwezi na haitatokea,na nilishaambia ndugu zangu ,jamani tuleleane watoto ikiwa hatupo,yaani kifo,ikiwa sote tu wazima wa afya kila mmoja apambane na mzigo wake.

Nimeona kwa watu wengi sana hapa hasa walimu wenzangu wameishia kuvurugana na ndugu zao kisa watoto waliowachukua kuwalea.

Hatari saana
 
Ukishindwa kuwa muwazi kwa watu matokeo yake ndiyo haya. Watu wanatakiwa wakuelewe msimamo wako, unatakiwa uwaeleze kabla bila kumung'unya mung'unya maneno, waujue msimamo wako kabla hawajaanza kufanya haya yote mnayolalamikia hapa.

Usipokuwa muwazi ukawaachia, matokeo yake ndiyo haya unaanza kuja kulalama humu kwenye mitandoa. Kwanza haya maswala ni too private katika hali ya kawaida mtu hatakiwi kuyaleta humu
 
Jamaa una majivuno 😂, dsm tu mzee unavimba,, vipi ungeishi London?
Sifurahii tabia ya mtu kukustukiza,, ila cjapenda ulitambaa na mistari,, saidia tu upate baraka,,
 
Dah! Binadamu tunasahau mapema sana yaani mtu amesomeshwa na mjomba wake na alikuwa analala jikoni kwa mjomba ake leo Mungu amemuinua, hatak ndugu uzuri ndugu wenyewe huwa hawaji mikono mitupu wamekuja na ndizi, mchele, unga maharage kuja kusalimia wapendwa wao na kusafisha macho na kubadili mazingira kidogo, tunawaona wasumbufu, hilo la taarifa ni changamoto isifanye umzimie ndugu yako simu dah! Mungu atusaidie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…