Hii tabia ya kukata pesa pembeni, inaharibu pesa zetu, tuiacheni jamani

Mimi naomba niwe tofauti kidogo.

Siyo vizuri kuchana noti, ila chuma ulete nina amini ipo na imenitokea.

Mimi ninafanya kazi kwenye Idara ya Fedha. Sikuwa nina amini chuma ulete; nilikuwa mbishi sana.

Kuna siku nilienda kukusanya hela. Ajabu, nilipoenda kuzihesabu, niligundua pesa kiasi cha shilingi elfu 10 hamna. Lakini, nikakumbuka, kuna dogo mmoja ghafla aliniomba chenji ya elfu 10 wakati ninakusanya hela. Huyo dogo ninakumbuka hakuwa na kazi yeyote ile yaani ni wale watu wakuzurura maeneo ya biashara za watu na kusimama simama kijiweni.

Kwa hiyo nikahusisha moja kwa moja kwamba pale nilipigwa changa la macho, inawezekana aidha nilipewa hela ndogo ila mazingaumbwe yakanifanya nione elfu 10, ama nilizidisha chenji kupitia kiini macho.

Nilipewa dawa ya kuzuia chuma ulete ambayo ni mkaa na ndimu. Unaweka kwenye mfuko wa hela. Toka wakati huo sijapoteza hela kimazingara.
Hayo ndo mambo siamini,inakuwaje nizidishe ela,mzee nini nahesabu ela mara mbili mbili,tena nahesabu moja moja kwa ufasaha
 
Hii ya kuchana noti ni mpya aisee.

Ila wakumbuke tu kuwa nasikia ni Kosa kisheria kuharibu fedha kwa makusudi
 
Mimi naomba niwe tofauti kidogo.

Siyo vizuri kuchana noti, ila chuma ulete nina amini ipo na imenitokea.

Mimi ninafanya kazi kwenye Idara ya Fedha. Sikuwa nina amini chuma ulete; nilikuwa mbishi sana.

Kuna siku nilienda kukusanya hela. Ajabu, nilipoenda kuzihesabu, niligundua pesa kiasi cha shilingi elfu 10 hamna. Lakini, nikakumbuka, kuna dogo mmoja ghafla aliniomba chenji ya elfu 10 wakati ninakusanya hela. Huyo dogo ninakumbuka hakuwa na kazi yeyote ile yaani ni wale watu wakuzurura maeneo ya biashara za watu na kusimama simama kijiweni.

Kwa hiyo nikahusisha moja kwa moja kwamba pale nilipigwa changa la macho, inawezekana aidha nilipewa hela ndogo ila mazingaumbwe yakanifanya nione elfu 10, ama nilizidisha chenji kupitia kiini macho.

Nilipewa dawa ya kuzuia chuma ulete ambayo ni mkaa na ndimu. Unaweka kwenye mfuko wa hela. Toka wakati huo sijapoteza hela kimazingara.
Kama una wallet unawekaje hiyo ndimu na mkaa?
 
Weka mkaa. Siyo lazima uweke vyote. Na suala la chuma ulete lipo sana kwenye maeneo ya biashara yaani wahanga ni wafanyabiashara na siyo wateja. Kwa hiyo uwezekano wa mfanyabiashara kuwa na chombo au mfuko mkubwa unaoweza kuwekea ndimu ni mkubwa
 
Dahh hizi imani hizi
 
Kuna jamaa ikishafika usiku hakupi helaaa ng'oooo.Hata kama alikuahidi ntakulipa siku fulani bora uwahi mchana usiku hulambi hata 100.Ni msomi na ana biashara yaani yuko freesh tu.Imani za kipumbavu sana hizi.
 
Wabongo ni watu waajabu sana,tunaviimani vya kipumbavu sana,sijui tumetoa wapi tabia zisizonamaana yeyote.

Hii tabia ya kukata ela pembeni kwa dhana kwamba inakuepusha na chuma ulete haina maana yeyote,
Kila pesa nayoishikilia iwe jero,buku,kaki hata msimbazi ukosi kukuta haijakatwa pembeni wanasema ukikata inakuepusha na chuma ulete.

Hakuna kitu kinaitwa chuma ulete,kwanza siaminigi viimani vya kipumbavu kama hivyo,daima akili ndogo huwaza ujinga.

Watanzania wenzangu tuacheni imani za kijinga,kama huna matumizi na ela yanayoeleweka daima utapoteza pesa zako,sio unasingizia chuma ulete.

Chuma ulete ni hadithi za kufikirika tu,hazina maana tuzitukuze

ONE TIME,
ONE FOR THE ROAD,
APPROXIMATELY ONCE AGAIN.....
Chuma ulete utaiskia Kwa maskini Tu na watu wa uswahilini
 
Back
Top Bottom