Hii tabia ya kukata pesa pembeni inaharibu pesa zetu, tuiacheni jamani

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2021
Posts
2,035
Reaction score
2,715
Wabongo ni watu waajabu sana, tuna viimani vya kipumbavu sana, sijui tumetoa wapi tabia zisizo na maana yeyote.

Hii tabia ya kukata hela pembeni kwa dhana kwamba inakuepusha na chuma ulete haina maana yeyote,
Kila pesa nayoishikilia iwe jero, buku, kaki hata msimbazi hukosi kukuta haijakatwa pembeni wanasema ukikata inakuepusha na chuma ulete...

Hakuna kitu kinaitwa chuma ulete, kwanza siaminigi viimani vya kipumbavu kama hivyo, daima akili ndogo huwaza ujinga...

Watanzania wenzangu tuacheni imani za kijinga, kama huna matumizi na hela yanayoeleweka daima utapoteza pesa zako, sio unasingizia chuma ulete...

Chuma ulete ni hadithi za kufikirika tu,hazina maana tuzitukuze...

ONE TIME,
ONE FOR THE ROAD,
APPROXIMATELY ONCE AGAIN.....
 
 
boss chuma ulete sio hadith za kufkrika hv v2 vipo kwel km unabisha sbr tumuite Mshana Jr aje kukuadithia chuma ulete walivyobeba pesa zake za kiwanja cha urithi
 
Serikalin wanatakiwa kuingilia kati ili swala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…