Hii tabia ya Wanawake kuibiwa hela imeshamiri sana!

Hii tabia ya Wanawake kuibiwa hela imeshamiri sana!

Uje na mbinu kabambe,ambayo itaonyesha na Mimi nitafaidikaje, na hicho kizinga,wallahi hapo sichomoki🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣ila hizo mbinu za gari Iko garage Niazime ikitoka nitakupa hapana,tutapanda bolt
Mi tunaandikishana halafu from no where makaratasi uliyotunza kama ushahidi yanaliwa na panya!.. there's panyas called economic panya! They are coming from no where when they see opportunity...😅
 
Kuna mmoja hapa katoka kunipiga mzinga wa laki tatu nimeukwepa kikauzu simpi hata mia mbovu...

Eti wiki iliyopita katoka kutoa ela ATM ya kodi 300k kabla hajaenda kulipa akakutana na kijana mtanashati njiani akamwambia yeye ni meneja wa kampuni ya kuuza dawa za kisukali na presha pamoja na madonda ya tumbo kwa mitishamba iliyoboreshwa pamoja na vyakula asili..

Akamshawishi ajiunge na kampuni kwani anaweza kujiingizia kipato nje ya kazi zake za kila siku hivyo ili kujiunga itatakiwa alipe laki mbili ya commission halafu 50K atanunua bidhaa. Na kila atakaemuunganisha katika kampuni na kufanikiwa kumuuzia bidhaa basi na yeye hisa zake zitaongezeka. Hatimaye atakuja kua milionea.

Kampa mifano mingi ya waliojiunga na hiyo kampuni, wengi wakiwa wamefanikiwa sana wanaendesha magari mazuri. Akamuonesha mpaka picha zake huyo kijana akiwa amepiga na wazungu maeneo mbali mbali. Kuonyesha ni mtu anaeaminika. Binti kashawishika. Sasa akili imemrudi na yule bwana kashasepa na mwenye nyumba anadai kodi yake...
 
Back
Top Bottom