Hii tabia ya wanawake wa siku hizi kupenda uke wenza inasababishwa na nini?

Tulia kikurambe mwenetu.
 
Mwl Tu wanatamani hata kama Kipato chake kidogo lakini maisha yanakwenda, Sisi Mainjinia ndio balaa, mtu unamwambia kabisa Nina wake wawili na bado anasema " Hesabu Mimi wa Tatu" na wala hatanii
 
Njaa.
Tamaa.
 
Unajua suala sio kusamehe kucheat suala ni mfumo wankuendesha mahusiano ambao tayari sisi waafrika tumeshausimika. Kuanzia mwanzo wa mahusiano mwanaume anabebeshwa maintenance costs zote. Hii inatengeneza mtazamo kwamba mwanaume ni mmiliki. As you know, the one with financial power have leverage in relationship. Ndio hapo inaonekana mwanaume akicheat ni sawa, ila mwanamke akicheat amani lazima itoweke.

Ku-adapt mfumo wa kuendesha mahusiano ambao kuanzia mwanzo mwanaume abebeshwi maintenance cost, kama ilivyo kwa wazungu itamaliza hili suala.

Mwanamke akiingia kwenye mahusiano na hela zake na kujihudumia mwenyewe mahitaji yake bila kujiona yupo entitled kwenye hela na mali za mwanaume. Hii itamuweka huru hata yeye kucheat atakapocheatiwa. Infact, sio kucheat tu. Hata pale mapenzi yatakapoisha atakua uhuru kubunja mahusiano. Lakini suala la kusema mwanaume amuhudumie mwanamke halafu mwanamke alipize kisasi kwa yeye pia kucheat ni ngumu kukubalika kwa sababu tayari mwanaume ashafanya uwekezaji
 
Huyo kisebengo wako wa nje anamwambia mwenzake wa ndani hayo maneno sababu si yeye aliyeolewa, angekuwa yeye ndio mke wa ndoa chances are angefanya same same.

Waoneeni huruma wanawake zetu, nadhani sio jambo jepesi kujua mume ana mwanamke mwingine nje.
 
Inawezekana mtaani kuna lundo la wanawake ambao wanapitia stress nyingi za kukosa permanent relationship..... Kuna mshikaji wangu nlisoma naye A level, jamaa ana maisha ya kawaida.
Ila ameshazaa na wanawake watatu tofauti, watoto wawili tuu ndo amewatambulisha kwao, mtoto mmoja imebidi amfishe kuepuka aibu nyumbani. Cha ajabu zaidi jamaa anasema katika hao wote watatu hajaona wa kuoa, anasema wote ni kama walimtegeshea, kwa kumdanganya wa safe kumbe wana mipango yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…