Hii Trending ya kujifanya Mcha-Mungu wakati wa Ramadhani ni kujilisha upepo na ubatili mtupu

Hii Trending ya kujifanya Mcha-Mungu wakati wa Ramadhani ni kujilisha upepo na ubatili mtupu

Mimi hamna watu nawaona wanafiki kama wanaobadilisha maisha mwezi wa ramadhani, ukiisha wanarudi uchafuni
- mtu anaacha uzinzi/anavaa kwa stara kwa mwezi mmoja. ukiisha anarudi kwenye laana.
mi naona ni either ubadilike moja kwa moja or uendelee na mambo yako ya sikuzote.
Kuna watu wao sikuzote huwakosi msikitini wala mavazi hayabadiliki hawa mi naona ndo wanastahili kufunga
Wewe unaweza kubadilika moja kwa moja?
 
Ukitaka kutambua kiwango cha unafiki wa kiwango cha SGR basi angalia kwa umakini maisha ya wafuasi wa dini.

"Religion is the opium of the people" karl marx
 
mtu anangoja mwezi mmoja kila mwaka ili afanye jema??? mko serious kweli
ukiamua kuwa mbaya kuwa mbaya l,ukiamua kuwa mwema kuwa mwema
vinginevyo ni unafiki
Hata siku moja kwa Mungu ina thamani , mbona mwezi mkubwa sana, binadamu anaweza kukaa sawa muda wowote , endelea kumtia moyo kwa kufanya jambo jema, sio kukatishana tamaa kwenye mambo mema, ukifanya jema wakati wowote utalipwa thawabu zako na ukifanya baya wakati wowote utalipwa dhambi zako, tuendelee kutiana moyo kwenye mema, mbona wana wa Israel Mungu amewavumilia sana pamoja na utukutu wao, akiwakataza hili wanarudia tena , hii ni tabia ya wanadamu , Daudi alimpeleka mtu vitani ili akauwawe achukue mke wake, lakini alipata msamaha
 
Mimi hamna watu nawaona wanafiki kama wanaobadilisha maisha mwezi wa ramadhani, ukiisha wanarudi uchafuni
- mtu anaacha uzinzi/anavaa kwa stara kwa mwezi mmoja. ukiisha anarudi kwenye laana.
mi naona ni either ubadilike moja kwa moja or uendelee na mambo yako ya sikuzote.
Kuna watu wao sikuzote huwakosi msikitini wala mavazi hayabadiliki hawa mi naona ndo wanastahili kufunga
Kwahiyo wewe dhambi zote kwasasa umeacha?
 
Nipo Sehemu za Uswahilini naona wanawake na wahuni wote wanavaa vizuri wanapiga ushungi Kama wa Madam president so niseme ni Jambo zuri Sana endapo mkaishia hivyo Maisha yenu yote.

Imekuwa kawaida watu kumuigizia Mungu wakati wa Ramadhani na baada ya huu Mwezi kuisha watu wanarudi katika uchafu so this is None-sense iidiotism philosophy

The repentance is now there's no reason to Fake anymore.

Ramadhan KAREEM
Hizi dini tulizoletewa ni mzigo tu
 
Kama ramadhan inatosha kuwafanya wamkumbuke Mungu hata kidogo basi hilo ni jambo kubwa sana linalo vutia mtu huwa habadiliki siku moja, Ramadhan ni kipimo sahihi cha hofu yao haitakiwi wewe kuumia kwa mambo yasiyo kuhusu, huwezi kuisemea nafsi yake Mungu ndo anajua kuwa anaigiza au anaomba toba.

Ramadhani ni mwezi wa toba kwa waislam wote haijalishi alikua anatenda dhambi kiasi gani huu ni muda wao wa kuomba msamaha.
Kila matendo yanalipwa kutokana na nia ya mtu kwa macho yako wewe ni kuwa wanaigiza ila ndani ya nafsi zao anajua Mungu zaidi.
Word!
 
Sijasema niko daraja moja hayo umesema ww

Hee mbona jazba? hata mimi Mungu ndo anajua we nani kumsemea Mungu
Mimi nimekushangaa wewe kuita watu wanafiki wakati hilo jambo Mungu ndio anajua dhati ya mioyo ya hao watu, mtu akifunga , akiacha dhambi au akirudia hili jambo Mungu anajua maana yeye ndio mlipaji, hivyo basi acha kuita watu wanafiki wakati wewe hujui chochote juu ya mioyo ya hao watu, Mungu ndio anajua unafiki au ukweli wa mtu sio wewe
 
Ukweli mtupu . M/mungu anawachora tu kwa ufupi baadhi ya waislamu wengi wao ni wanafki
 
Back
Top Bottom