Kibarua kikubwa kwa intelligence ya Iran kwa sasa ni kuuvunja mtandao wa Mossad na CIA uliofanikiwa kujipenyeza kwenye taasisi zao za usalama na kiraia.
T14 Armata 100 others zitto junior Nguruvi3
Kwa maoni yangu ujasusi ama kwa kinyume chake ugaidi,hauna bingwa wala fundi.
Mara nyingi hii ni kama vita ya kuviziana, ni kama vile wewe ukiwa kwako hujui jirani Yako ana kuwazia Nini,ana mipango Gani ovu dhidi Yako na atakufanyia Nini na atakufanyia lini.
Ila Siku akikufanyia ubaya ndipo utakapoanza kuchunguza kua kafanyaje ndio utagundua mengi.
Israel imejiwekea utaratibu wa kujilinda kwa njia za kuumiza wenzake kwa njia za kijasusi/kigaidi,lkn nchi nyingine hazijawekeza sana huko zaidi ya kutambua,kuchunguza na kuzimaTU, matukio yasitokee kabla.
Kwa Nini hapo juu nimesema ujasusi /ugaidi hauna mwenyewe?wala hauna bingwa?
Sababu zangu na mifano ni hizi.
Tusirudi nyuma sana.
Majasusi wa kipalestina walienda kwenye kambi ya Israel katika michuano ya Olympic mwaka Fulani wakaua wa Israel kadhaa.
Hapa intelligence ya Israel haikujua kabla lkn haimaanishi Israel ni dhaifu kiintelijensia.
Mwaka Jana kama sijakosea Hamas walipanga mpango na kuingia ndani ya Israel na kuua na kuteka watu na askari kadhaa ambao wengine Hadi Leo hawajapatikana,
Hapa pia haimaanishi Israel ni dhaifu kiintelijensia.
Mwaka Fulani Majasusi/magaidi wa Al Qaeda walipiga Kwa siku moja saa moja ofisi za ubalozi za Marekani zilizokuwepo Dar es salaam na Nairobi.
Hapa haimaanishi Marekani Ina intelligence dhaifu.
Pia Majasusi/ magaidi ya Al Qaeda yaliteka ndege Tano za Marekani,ndani ya marekani na kuanza kuzibamiza kwenye Kuta za majengo muhimu ya Marekani mfano jengo maarufu na refu zaidi duniani Kwa wakati huo la World Trade Center na majengo mengine,matokeo ya operation hiyo walikufa watu Karibu 3000.
Hapa pia haimaanishi Marekani Wana intelligence dhaifu.
Juzi hapa Majasusi/magaidi wa Ukraine na NATO walijipenyeza na kuingiza vifaa Urusi na baadae kulipua viwanja vya ndege muhimu za Urusi,pamoja na ujasusi/ugaidi wa kuua baadhi ya Makamanda wa jeshi wa Urusi.
Hapa pia haimaanishi Urusi ni dhaifu kiintelijensia.
Sasa pia ukija kwa Iran.
Kwa Israel kupenyeza Majasusi/magaidi wake Iran na kufanya operation zake bado pia haimaanishi Iran ni dhaifu kiintelijensia.
Pia kumbuka Iran iliweza kupata taarifa zote muhimu za jeshi la Israel na kuzitumia kupiga maeneo muhimu ya Israel ,hapa pia haimaanishi Israel ni dhaifu kiintelijensia.
Kumbuka nilisema Israel imejikita sana katika ujasusi wa kuua Viongozi au watu tishio kwake kutoka kwa n hi adui zake na Hali hii Kwa upande wa west wanaita ni ujasusi ,lakini Hali kama hiyo ikifanywa na wapinzani wa Israel kwa kuua Viongozi tishio kwao,mfano tishio kwa Iran wamagharibi watatia tukio hilo ni tukio la kigaidi.
Mfano TU kulikua Kuna propaganda inapigwa kua Iran inataka ilitaka kumuua Trump,tufanye kweli au sio kweli.
Kama ingekua ni kweli na Trump akauliwa kwa mkono wa Iran nadhani wamagharibi Dunia nzima wangepiga kelele na kulaani na kuita tukio hilo ni la kigaidi.
Wangepeleka majeshi Yao yote kwenda kuisamabratisha Iran.
Lakini umekua ni wimbo pendwa na kauli inayosifiwa na wamagharibi wote Dunia nzima kusema Ayatollah lazima auwawe ili kuweka na regime change huko Iran.Kauli hii haijalaaniwa na taifa lolote la west.
Na kama Israel ingefanikiwa kumuua Ayatollah Leo hii wangesema na kusifu kua ni operation iliyofanikiwa.
Kwa bahati mbaya Iran sera zake za kijasusi sio kuua watu wa Mataifa mengine.
Lee Vladimir Cliff Sina upande katika mzozo huu.
Niko upande wa amani.