Ungemalizia kusema...! Kwa uonavyo wewe!!
Kwa sababu ulichoandika ni fikra zako zinazoendana na mwisho wa upeo wako
Maana tamanio lako ulidhani Marekani yeye hawezi kupata changamoto yoyote hasa linapokuja suala la vita
Uliamini kwamba, Nchi kama Marekani... unapoangalia uwezo wao wa kijeshi, bajeti yao na jinsi Dollar yao ilivyotamalaki duniani n.k, basi wao mambo ya vita ni kama kunywa chai
Fahamu kabisa, Marekani na usuper power wake, hata Sisi Tz tunaweza kumsumbua licha kwamba atatuchakaza
Mkuu, jamaa ana hoja ila alitakiwa aelezee uzuri.
Kwa mfano Hispania kaeleza kinagaubaga kwamba hii vita iloanzishwa na Marekani na Israeli ni illegal yaani kinyume cha sheria za kimataifa na wamekataa kutumika kwa vituo vyake vya kijeshi kuishambulia Iran.
Na Hispania pia aliungana na Afrika Kusini kusema kwamba vita ya Gaza ilikuwa ni Genocide.
Akiongelea hilo la Iran, waziri mkuu wa Hispania Sanchez alipohojiwa na gazeti la Wall Street Journal alisema namnukuu “Good allies are like good friends. We tell each other the truth no matter what, “In my view, this war in Iran is a big mistake for the world and therefore for the U.S.”" - Mwisho wa kunukuu.
Kwahiyo watu kama akina Sanchez wakisimama na kumjibu Donald Trump sie wengine tapaswa kutake notes.
Hivyo unafiki wa Dunia wajidhihirisha zaidi kwa sasa kwani hakuna cha Umoja wa Mataifa wala Umoja wa Ulaya waloo tiyari kumkosoa Marekani na kuiamuru isimamishe vita kwa kukiua mikataba ya kimataifa kama wa Geneva na ila ya UN kwamba nchi moja haiwezi kuivamia nchi ingine bila kuchikozwa au kuvamiwa yeye (unprovoked attack).
Unafiki wa Dunia ni pale pia kwamba Ujerumani, UK, Ufaransa na Ukraine wapo busy (nyuma ya pazia) kuisaidia Marekani na mashambulizi yake kwa Iran. NI haohao nchi za Ulaya ndo walosema kwamba Russia kamvamia Ukraine bila kushambiliwa wao (Unprovoked Invasion) lakini ni haohao ndo walibariki Iran kushambuliwa na Marekani, huku ndege zingine zikitokea kituo cha kijeshi cha Ujerumani na huko Zelensnki akizunguruka duniani kutaka kuuza (counter drones) kusaidia kuidhoofisha Iran kwa sababu tu Iran alikuwa akiuza Drones kwa Russia ambayo hadi leo yaendelea kuishambulia Ukraine.
Unafiki wa dunia pia upo pale nchi za NATO ndozo zenye kuvunja sheria za kimataifa, kuvamia nchi zingine na kudhoofisha mipaka ya nchi hizo (Iran na Syria) na ndo waloweka vikwazo vya kiuchumi kwa Russia na hapohapo kuisaidia Ukraine kwa mamilioni ya fedha kwenye vita yake na Russia laini leo wapo nyuma ya mshirika wao Marekani kuishambulia Iran nchi yenye watu milioni 91 .
Na vita hii ya Iran imepelekea watu 1500 kuuawa hadi sasa, mfereji wa Hormuz kufungwa na Iran na pia kutishia kufunga mfereji wa Ban El Mandeb jambo ambalo hadi leo limezua taharuki, tafrani na sintofahamu ya kiuchumi Duniani kote kwa gharama za mafuta, vyakula, mbolea na gesi kuendelea kupanda huku kukiwa hakuna dalili ya kutafuta suluhisho kwasababu tu ni Marekani ataka mafuta na gesi ya Iran kwa nguvu.
Hivyo mleta mada aweza kuwa na hoja hapo.