Hiki anachofanya Masanja Mkandamizaji sio sahihi kabisa

Hiki anachofanya Masanja Mkandamizaji sio sahihi kabisa

Shule za msingi na sekondari sio sehemu ya kufanyia mambo ya kidini.
Nani alikudanganya kwamba kukemea pepo kwa jina ka Yesu ni kazi ya makanisa ya mitaani ? Unaweza kuniambia hapa nini maana ya makanisa ya mitaani ? Kazi ya kukemea pepo iliagizwa na kufanywa na Yesu mwenyewe, leo unatuambiaje wewe ? Kama huna cha kuposti ni bora ukaacha kuandika upuuzi kama huu. Ninakushauri uokoke ili Yesu awe Bwana na Mwokozi wako.
 
Vipindi vya dini mashuleni vifutwe
Mkuu serikali haina dini ila inatambua uwepo wa dini na imani za watu, na ndo mana ata mashuleni kuna muda umetengwa maalumu na kuingizwa kwenye time table kwa ajili ya vipindi vya dini.

Apo sidhan kama kuna tatizo
 
Hawa wachunga ng'ombe wana matatizo sana maamae zao wengine wanakula kondoo wengine wanaua waumini wengine wanawafanya mazuzu yaani ilimradi tu ,ila yakikukukuta umeyataka maana umejipeleka mwenyewe kwenye anga zao kama yule umbwa aliyewaua kwa kuwakanyagisha kimiminika kule Moshi. Watu wameacha kufanya kazi wamekua mazuzu wanasubiria eti miujiza mxiuuuuuuuuuuuuuu
 
Kuna video imesambaa mtandaoni ikimuonyesha Masanja Mkandamizaji na vijana wengine nadhani ni wafuasi wake katika kanisa lake lile liko pale Leaders club. Clip inaonyesha wako ktk shule fulani nmeshindwa kujua ni shule gani exactly lakini kwa mazingira inaweza kuwa Arusha, anaonekana Masanja anaomba na watoto wanaanguka kimapepo.

Hii kitu sio sahihi kabisa kwa mazingira ya eneo la elimu na pia kwa mazingira ya watoto wadogo. Sijui uongozi wa shule waliweka wapi akili na fikra zao kuruhusu hili.

Binafsi nmeona ni jambo lisilo na mantiki kabisa. Sioni kabisa logic ya hii kitu kabisa. Inaweza kuleta madhara ya kisaikolojia hapo baadae kwa wanafunzi na hata shule husika pia.

Tunajua jinsi baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu kutumia nguvu tofauti tofauti kujifanya wanakemea mapepo na watu wakianguka ovyo, huwa sijui lengo hasa ni lipi lakii kwa watu wazima wenye akili timamu ambayo hawajapelekwa pale kwa bakora, walienda kwa matakwa yao ni sawa.

Lakini kwa watoto wadogo kama wale hakika sio jambo sahihi kabisa. Unless hiyo shule iwe na shida fulani inayohitaji maombi kama yaliyofanywa na Masanja na watu wake.

Lakini kwa uchunguzi kidogo nimebaini ni kama tour huyu Masanja anafanya katika mashule kufanya anachokifanya. Hapa namaanisha kuzunguka katika mashule na kuombea na watoto kuanguka ovyo. Nadhani si sahihi na shule sio eneo sahihi kwa haya anayofanya Masanja.

Naona ni busara kwa wenye mamlaka kuzuia hii kitu kufanyika katika mashule.

Masanja ni TAPELI tu na Chawa wa Mwanyika.
 
Anafanya kwa watoto janja janja yake ili waje kuwa waumini wake in the future. Watoto ni Taifa la kesho
 
Anafanya kwa watoto janja janja yake ili waje kuwa waumini wake in the future. Watoto ni Taifa la kesho
Utapaza vipi sauti kwa jamii yako ili iweze kushtukia mchezo wa masanja. Au na ww sauti yako imeminywa
 
Nilidhani una akili kumbe una matope. Pole sana
Matapeli tu nyinyi! Hamna lolote!!! Karne ya 21 hii bado mnawaibia tu watu kupitia hayo mazingaombwe yenu! Masanja ni mchekeshaji tu wa siku zote! Hana tofauti na wachekeshaji wenzake akina Joti, Mpoki, Kingwendu, nk.
 
Huyu uliemjibu hapo juu nae ana kanisa lake huko alipo ss unategemea atakuja hapa kusapoti hili suala?
Cheza na vitu vingine ila nakuonya usicheze na Kanisa la Mungu linaloongwa na nguvu za Roho Mtakatifu.
 
Kama unapenda dini badala kumpenda Mungu endelea hivyo upotevuni.
Unahaki ya kuipenda hiyo ndiyo dini yako,kuhusu Kila mtu kufungua kanisa,ni agizo la BWANA YESU mwenye,ukisoma Biblia kitabu cha Mathayo mlango wa 28,Mistari kuanzia wa 18,anasema enendeni ulimwenguni mkawafanye watu kuwa wanafunzi wangu......
Kwa mujibu wa hilo andiko huwezi ukawafanya watu kuwa wanafunzi wa YESU kwa kufungua mabaa,inambidi mtu afungue kanisa ili kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa YESU.
 
Nilidhani una akili kumbe una matope. Pole sana
Wewe ni mtoto! Utajuaje kama nina akili? Muulize mama yako! Yeye ananifahamu vizuri kama nina akili au matope. Wewe endelea tu kunyonya ili ukue.
 
Hivi kuna wachungai ambao huenda mahospitalini kuwatoa mapepo wagonjwa?
Hao wagonjwa nao huanguka na kugalagala watolewapo mapepo?
 
Back
Top Bottom