Hiki anachofanya Masanja Mkandamizaji sio sahihi kabisa

Hiki anachofanya Masanja Mkandamizaji sio sahihi kabisa

Maombi kwa muktadha wa kujua na kueneza neno la Mungu sidhani ni tatizo. Hilo jambo lipo. Mashehe kwa wachungaji kufundisha n kuabudu mashuleni lakini hili ni tofauti. Huku ni kukemea mapepo kwa makanisa ya mitaani yafanyavyo. Nmeshindwa kuiweka hapa ile clip jaribu kuitafuta utaiona then utajua ninachozungumzia
Siku za mwisho yametabiriwa haya,maandiko yapo wazi,acha watimize unabii ila kibaya wazazi ndio hawasomi maandiko na kuruhusu watoto wao kuchezewa bongo na kuachiwa mapepo wakue nayo,fuatilia hao watoto 10 yrs to come,utawaonea huruma
 
Kwanza usinibwatukie. Nikuulize kitu labda utajielewa na kuacha kubwatuka. Wakati wa ukuaji wako (utoto wako) uliwahi kushuhudia uotaji wa haya makanisa mitaani kama ilivyo sasa? Kulikuwa na makanisa rasmi na yanajulikana. Nadhani jibu umelipata.
Huyu uliemjibu hapo juu nae ana kanisa lake huko alipo ss unategemea atakuja hapa kusapoti hili suala?
 
Anazunguka kwenye mashule ili kutesti kwanza nguvu zake kama ziko sawa ndo aingie kitaani mkoa kwa mkoa aje kuombea vidume na mikurumbembe ya mjini.
Maana akikurupuka kuingia mitaani bila kufanya testi ya mitambo anaweza kukutana na makubwa.!
Kuna jamaa aliibukaga kijijini kwetu miaka hiyo akajifanya nabii eti akawatukana wachawi wa kijiji kwamba yeye hawamuwezi haikupita hata siku tatu alikutwa uchi wa mnyama amelala mku.ndu juu chini ya mwembe wa shule ya msingi na inasemekana alichezea "kifiro"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwahiyo jamaa alikutana na kih fih rho hevi?
 
Mkuu serikali haina dini ila inatambua uwepo wa dini na imani za watu, na ndo mana ata mashuleni kuna muda umetengwa maalumu na kuingizwa kwenye time table kwa ajili ya vipindi vya dini.

Apo sidhan kama kuna tatizo
Acha kuchanganya mambo ndugu.
 
Amina ubarikiwe kwa Neno zuri. Watu wanashindwa tambua kubwa Ulimwengu unaendeshwa kwa mambo mawi. Neno(Unabii) na Nyakati. Sasa ni utimilivu wa unabii wa Injili kuhubiriwa kwa Kila kiumbe. Injili inahubiriwa sasa na ndio maana utaona nyimbo za kikristo zinapigwa Vilabuni, kwenye mabasi hata sherehe za wenzetu watoto wa Ajiri.
Tulishawapiga marufuku kuhubiri kwenye mabasi,bado hizo nyimbo.....
 
Kuna video imesambaa mtandaoni ikimuonyesha Masanja Mkandamizaji na vijana wengine nadhani ni wafuasi wake katika kanisa lake lile liko pale Leaders club. Clip inaonyesha wako ktk shule fulani nmeshindwa kujua ni shule gani exactly lakini kwa mazingira inaweza kuwa Arusha, anaonekana Masanja anaomba na watoto wanaanguka kimapepo.

Hii kitu sio sahihi kabisa kwa mazingira ya eneo la elimu na pia kwa mazingira ya watoto wadogo. Sijui uongozi wa shule waliweka wapi akili na fikra zao kuruhusu hili.

Binafsi nmeona ni jambo lisilo na mantiki kabisa. Sioni kabisa logic ya hii kitu kabisa. Inaweza kuleta madhara ya kisaikolojia hapo baadae kwa wanafunzi na hata shule husika pia.

Tunajua jinsi baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu kutumia nguvu tofauti tofauti kujifanya wanakemea mapepo na watu wakianguka ovyo, huwa sijui lengo hasa ni lipi lakii kwa watu wazima wenye akili timamu ambayo hawajapelekwa pale kwa bakora, walienda kwa matakwa yao ni sawa.

Lakini kwa watoto wadogo kama wale hakika sio jambo sahihi kabisa. Unless hiyo shule iwe na shida fulani inayohitaji maombi kama yaliyofanywa na Masanja na watu wake.

Lakini kwa uchunguzi kidogo nimebaini ni kama tour huyu Masanja anafanya katika mashule kufanya anachokifanya. Hapa namaanisha kuzunguka katika mashule na kuombea na watoto kuanguka ovyo. Nadhani si sahihi na shule sio eneo sahihi kwa haya anayofanya Masanja.

Naona ni busara kwa wenye mamlaka kuzuia hii kitu kufanyika katika mashule.
Hayo mambo huwa yanafanyika sana,au wewe ni mgeni wa hizi ishu? Au tatizo ni kuwekwa mtandaon.... Ungekuwa wazi kama unatetea faragha za watu au unapinga maombi yasiwepo school
 
Kumlaumu Masanja kwa akifanyacho huku ukiwaacha Wakongwe wengine kama wa Kawe, Ubungo na Mwenge ni Unafiki mkubwa na Chuki kubwa iliyojaa Wivu uliyonayo Kwake.

Kwani umeambiwa hawa Watoto katika Makanisa ya hawa Wakongwe wengine wa Imani hizi za Kitapeli nchini Tanzania hasa Mkoani Dar es Salaam huwa hawaendi huko?

Kutokana na Waumini wengi wa Kitanzania kupenda zaidi Miujiza badala ya Neno la Mungu lenye Thamani ndilo limefanya hawa akina Masanja na wengine watumie mwanya huu Kuwadanganya Kiimani huku wakijipatia Pesa zao kwa njia rahisi sana.

Watanzania wengi wanaokwenda katika haya Makanisa ya Kiroho si kweli kwamba huwa na Mapepo bali wote wana matatizo makubwa ya Kisaikolojia kutokana na Ugumu wa Maisha na kupotea kwa Utaratibu mzuri wa Kiustawi hasa katika Familia.

Kilichopo sasa na nakuomba Chunguza ni kwamba Watu wengi wanaouhudhuria haya Makanisa ya Kiroho wanaanza kupatwa na matatizo ya Akili kuanzia katika Kauli zao na hata Matendo yao kama umebahatika Kukaa nao.

Acheni hawa Wachungaji wa Imani hizi za Kitapeli wawakamue ipasavyo Pesa zao ili waendelee kuwa Masikini na Wendawazimu huku hao Wachungaji wakiendelea tu kuwa Matajiri kiasi kwamba kuwa mwingine ana Helikopta yake na mwingine hayuko mbali Kununua Meli yake.
Hata hao uliowasemea tunawapinga sana ila Masanja ameenda mbali zaid,kwanin aende shuleni hao ni watt isitoshe kuna wtt hawajalelewa kwenye hio imani anayoiamini yeye,serikali iangalie hilo jambo kwa jicho la tatu

Nb:hao wanaoenda huko kwa sijui mwamposa,kawa na sehemu waache wapigwe mpaka akili zitakapowakaa sawa
 
Siku za mwisho yametabiriwa haya,maandiko yapo wazi,acha watimize unabii ila kibaya wazazi ndio hawasomi maandiko na kuruhusu watoto wao kuchezewa bongo na kuachiwa mapepo wakue nayo,fuatilia hao watoto 10 yrs to come,utawaonea huruma
Inawezekana aiseee
 
Naipenda sana dini ya Kiislam huu uzuzu na uzwazwa haupo. Kila mtu anajifungulia kanisa lake kama nini sijui.
Unahaki ya kuipenda hiyo ndiyo dini yako,kuhusu Kila mtu kufungua kanisa,ni agizo la BWANA YESU mwenye,ukisoma Biblia kitabu cha Mathayo mlango wa 28,Mistari kuanzia wa 18,anasema enendeni ulimwenguni mkawafanye watu kuwa wanafunzi wangu......
Kwa mujibu wa hilo andiko huwezi ukawafanya watu kuwa wanafunzi wa YESU kwa kufungua mabaa,inambidi mtu afungue kanisa ili kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa YESU.
 
Kuna video imesambaa mtandaoni ikimuonyesha Masanja Mkandamizaji na vijana wengine nadhani ni wafuasi wake katika kanisa lake lile liko pale Leaders club. Clip inaonyesha wako ktk shule fulani nmeshindwa kujua ni shule gani exactly lakini kwa mazingira inaweza kuwa Arusha, anaonekana Masanja anaomba na watoto wanaanguka kimapepo.

Hii kitu sio sahihi kabisa kwa mazingira ya eneo la elimu na pia kwa mazingira ya watoto wadogo. Sijui uongozi wa shule waliweka wapi akili na fikra zao kuruhusu hili.

Binafsi nmeona ni jambo lisilo na mantiki kabisa. Sioni kabisa logic ya hii kitu kabisa. Inaweza kuleta madhara ya kisaikolojia hapo baadae kwa wanafunzi na hata shule husika pia.

Tunajua jinsi baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu kutumia nguvu tofauti tofauti kujifanya wanakemea mapepo na watu wakianguka ovyo, huwa sijui lengo hasa ni lipi lakii kwa watu wazima wenye akili timamu ambayo hawajapelekwa pale kwa bakora, walienda kwa matakwa yao ni sawa.

Lakini kwa watoto wadogo kama wale hakika sio jambo sahihi kabisa. Unless hiyo shule iwe na shida fulani inayohitaji maombi kama yaliyofanywa na Masanja na watu wake.

Lakini kwa uchunguzi kidogo nimebaini ni kama tour huyu Masanja anafanya katika mashule kufanya anachokifanya. Hapa namaanisha kuzunguka katika mashule na kuombea na watoto kuanguka ovyo. Nadhani si sahihi na shule sio eneo sahihi kwa haya anayofanya Masanja.

Naona ni busara kwa wenye mamlaka kuzuia hii kitu kufanyika katika mashule.
Amehamishia comedy kwenye dini?!
 
Ukiruhusu kila mtu akafanyie mambo ya dini yake shuleni kwa watoto wadogo itakuwa ni upuuzi.
Hayo hayakua maombi? Labda unataka serikali ipinge marufuku Dini za wenzetu, ndo jinsi wanavo omba brother
 
Shule za msingi na sekondari ni sehemu za watoto kusoma na kucheza tu sio kuendesha mambo ya kidini.

Back
Top Bottom