Hiki ndicho kikosi changu cha kwanza cha mchezo wa maruduo kati ya wananchi Yanga dhidi ya Madeama

Apunguze beki aanze mudathiri
Mabeki watano mechi ya nyumbani sio poa
Coach ajilipue ashambulie tuko home ground
Tatizo wale Medeama wanashambulia kama nyuki. Ikitokea hivyo basi nahodha Bakary Mwanyeto ndiyo apumzishwe.
 
Hiyo mechi inabidi kocha atanue uwanja apunguze viungo wengi
Nadhani moloko aanze ili ile winga yao ya kushoto isimbue Yao sana
 
Sijui kwanini ila nauchukia sana mpira wa bongo. Tena hasa baada ya kuibuka hawa matapeli wanaojiita wahisani sijui watoa pesa, yaani wameviteka kabisa. Wana take advantage ujinga wa watu wengi , wananufaika wao wenyewe, na wabongo maskini hawana habari , wamegeuzwa mtaji. Wamekaa kushangilia upumbavu tu..

Hawa mnaowaita wawekezaji wanapata faida kubwa sana , Hakuna mkataba wowote upo hadharani, wamejimilikisha vilabu. Wameweka matangazo mpaka matakoni, yaani sijui hata nisemeje mnielewe. Aisee soka linakua , ila kuna watu wanafaidi sana hivi vilabu

Naishia hapa Kwa leo
Bila Mo na GSM hakuna Simba na Yanga za kimataifa huu ndiyo ukweli wenyewe.
 
Dah! Pole sana Kiongozi. Bongo bila ya wawekezaji, maisha hayaendi!! Na kama huamini, basi subiri Mo atangaze leo kujitoa pale Msimbazi!! Nakuhakikishia kuna watu watamlamba hata migui, ili tu abadili huo uamuzi wake.
Kama vile Mzee Akilimali na wazee wenzake walivyomlamba miguu Yusuf Manji .
 
Naomba nisiwachoshe.

1. Djugui Diarra
2. Kwasi Jeshi
3. Joyce Lomalisa/Farid Mussa Malick
4. Dickson Job
5. Bakary Mwamnyeto
6. Ibrahim Bacca
7. Khalid Aucho
8. Max Nzengeli
9. Stephen Aziz Kii
10. Hafiz Konkoni
11. Pacome Zouazoua.

Subs: Abutwalib Mshery, Kibwana Shomary, Nickson Kibabage, Gift Fred, Zawadi Mauya, Sure Boy, Mudathir Yahaya Abbas, Clement Mzize, Kenned Musonda, Jesus Moloko.

Lengo la kuanza na hicho kikosi ni kuhakikisha timu inashambulia kwa kasi, inamiliki mpira na pia kukaba kwa wakati mmoja. Mzize akiingia dakika za mwisho atasaidia timu kwenye kuongeza mashambulizi. Maana hao Medeama kwenye ile mechi ya yao awali kule Ghana, walionesha dalili za kukata pumzi kwenye dakika za mwisho.

Napendekeza Hafiz Konkoni kuanza, kwa sababu anawafahamu zaidi hao Medeama kuliko hata Mzize au Musonda.

Aziz Kii mchezaji mkubwa. Uwepo wake kwenye mechi kama hiyo ya kufanya maamuzi, ni muhimu sana.
All in all, mechi hii ushindi ni lazima ili kufufua matumaini ya kusonga mbele. Naitakia ushindi mnono timu ya Wananchi Yanga.
Yaani Aziz Ki acheze straika? Aucho namba 7? Konkoni namba 10?
 
Hii formation inaitwa 3- 2- 4- 1. Mabeki 3 nyuma. Mabeki wa 2 wa kushoto na kulia wanakaba na kushambulia kupitia pembeni, Striker namba 9 ni Hafiz Konkoni. Aucho 6! Halafu hawa watatu waliobaki~Pacome, Aziz Kii na Nzengeli ni mwendo tu wa kukichafua pale katikakati.

Hapa Medeama lazima wapoteane.
 
Sijui kwanini ila nauchukia sana mpira wa bongo. Tena hasa baada ya kuibuka hawa matapeli wanaojiita wahisani sijui watoa pesa, yaani wameviteka kabisa. Wana take advantage ujinga wa watu wengi , wananufaika wao wenyewe, na wabongo maskini hawana habari , wamegeuzwa mtaji. Wamekaa kushangilia upumbavu tu..

Hawa mnaowaita wawekezaji wanapata faida kubwa sana , Hakuna mkataba wowote upo hadharani, wamejimilikisha vilabu. Wameweka matangazo mpaka matakoni, yaani sijui hata nisemeje mnielewe. Aisee soka linakua , ila kuna watu wanafaidi sana hivi vilabu

Naishia hapa Kwa leo
Anzisha uzi wako au una stress mwenzetu
 
Konkoni ni finisher mzuri akicheza na viungo wengi wanaomzunguka. Sema mwalimu hajampa nafasi ya kutosha, kama ilivyo kwa beki mkatili Gift Fred.
Kumbe Gift Fred ni beki mkatili? Ni mkatili uwanjani au kwa familia yake kuwalisha watoto ugali dagaa huku anakula mshahara mnono toka Yanga?
 
Tatizo wale Medeama wanashambulia kama nyuki. Ikitokea hivyo basi nahodha Bakary Mwanyeto ndiyo apumzishwe.
Mimi sio Yanga ila sitaki Nahodha Mwamnyeto apunguzwe mara ya mwisho kucheza bila yeye Yanga iliruhusu magoli matatu
Kupanga ni kuamua
 
Naomba nisiwachoshe.

1. Djugui Diarra
2. Kwasi Jeshi
3. Joyce Lomalisa/Farid Mussa Malick
4. Dickson Job
5. Bakary Mwamnyeto
6. Ibrahim Bacca
7. Khalid Aucho
8. Max Nzengeli
9. Stephen Aziz Kii
10. Hafiz Konkoni
11. Pacome Zouazoua.

Subs: Abutwalib Mshery, Kibwana Shomary, Nickson Kibabage, Gift Fred, Zawadi Mauya, Sure Boy, Mudathir Yahaya Abbas, Clement Mzize, Kenned Musonda, Jesus Moloko.

Lengo la kuanza na hicho kikosi ni kuhakikisha timu inashambulia kwa kasi, inamiliki mpira na pia kukaba kwa wakati mmoja. Mzize akiingia dakika za mwisho atasaidia timu kwenye kuongeza mashambulizi. Maana hao Medeama kwenye ile mechi ya yao awali kule Ghana, walionesha dalili za kukata pumzi kwenye dakika za mwisho.

Napendekeza Hafiz Konkoni kuanza, kwa sababu anawafahamu zaidi hao Medeama kuliko hata Mzize au Musonda.

Aziz Kii mchezaji mkubwa. Uwepo wake kwenye mechi kama hiyo ya kufanya maamuzi, ni muhimu sana.
All in all, mechi hii ushindi ni lazima ili kufufua matumaini ya kusonga mbele. Naitakia ushindi mnono timu ya Wananchi Yanga.
bila mudathir yanga ni mtibwa sugar tu.
 
Tukutane leo saa 10 jioni kwa Mkapa. Ushindi ni muhimu sana kwa Wananchi. 💚💛
 
Yuko wapi Makudubela sasa!!! Hata Sub!!!
Hii siyo mechi ya Makudubela, hapa wanatakiwa wanaume wa shoka. Skudu anafaa kwenye mechi soft. Ile mechi ya Azam tu alishindwa kuhimili vishindo akakaa majeruhi kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom