Hiki ndicho kikosi changu cha kwanza cha mchezo wa maruduo kati ya wananchi Yanga dhidi ya Madeama

Apunguze beki aanze mudathiri
Mabeki watano mechi ya nyumbani sio poa
Coach ajilipue ashambulie tuko home ground
Tatizo wale Medeama wanashambulia kama nyuki. Ikitokea hivyo basi nahodha Bakary Mwanyeto ndiyo apumzishwe.
 
Tatizo wale Medeama wanashambulia kama nyuki. Ikitokea hivyo basi nahodha Bakary Mwanyeto ndiyo apumzishwe.
Hiyo mechi inabidi kocha atanue uwanja apunguze viungo wengi
Nadhani moloko aanze ili ile winga yao ya kushoto isimbue Yao sana
 
Bila Mo na GSM hakuna Simba na Yanga za kimataifa huu ndiyo ukweli wenyewe.
 
Dah! Pole sana Kiongozi. Bongo bila ya wawekezaji, maisha hayaendi!! Na kama huamini, basi subiri Mo atangaze leo kujitoa pale Msimbazi!! Nakuhakikishia kuna watu watamlamba hata migui, ili tu abadili huo uamuzi wake.
Kama vile Mzee Akilimali na wazee wenzake walivyomlamba miguu Yusuf Manji .
 
Yaani Aziz Ki acheze straika? Aucho namba 7? Konkoni namba 10?
 
Yaani Aziz Ki acheze straika? Aucho namba 7? Konkoni namba 10?
Hii formation inaitwa 3- 2- 4- 1. Mabeki 3 nyuma. Mabeki wa 2 wa kushoto na kulia wanakaba na kushambulia kupitia pembeni, Striker namba 9 ni Hafiz Konkoni. Aucho 6! Halafu hawa watatu waliobaki~Pacome, Aziz Kii na Nzengeli ni mwendo tu wa kukichafua pale katikakati.

Hapa Medeama lazima wapoteane.
 
Anzisha uzi wako au una stress mwenzetu
 
Konkoni ni finisher mzuri akicheza na viungo wengi wanaomzunguka. Sema mwalimu hajampa nafasi ya kutosha, kama ilivyo kwa beki mkatili Gift Fred.
Kumbe Gift Fred ni beki mkatili? Ni mkatili uwanjani au kwa familia yake kuwalisha watoto ugali dagaa huku anakula mshahara mnono toka Yanga?
 
Tatizo wale Medeama wanashambulia kama nyuki. Ikitokea hivyo basi nahodha Bakary Mwanyeto ndiyo apumzishwe.
Mimi sio Yanga ila sitaki Nahodha Mwamnyeto apunguzwe mara ya mwisho kucheza bila yeye Yanga iliruhusu magoli matatu
Kupanga ni kuamua
 
bila mudathir yanga ni mtibwa sugar tu.
 
Tukutane leo saa 10 jioni kwa Mkapa. Ushindi ni muhimu sana kwa Wananchi. 💚💛
 
Yuko wapi Makudubela sasa!!! Hata Sub!!!
Hii siyo mechi ya Makudubela, hapa wanatakiwa wanaume wa shoka. Skudu anafaa kwenye mechi soft. Ile mechi ya Azam tu alishindwa kuhimili vishindo akakaa majeruhi kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…