Hiki ni kiwango kilichopitiliza cha Ukatili kwa watoto

Kuna shule ya ipo karibu yangu hapa madogo wanakula sana mboko, sasa imagine dogo kala mboko skuli, kafika home msosi hakuna, anawahi madrasa huko nako anakutana na bakora 5 za moto.

Huyu akija kua kibaka kukutia bisu hataona kazi dadeki.
Kulingana na umri wa mtoto, na saikolojia Tete ya mtoto, lazima achukie kuja duniani na akiwa kwa mfano na watoto wengine natoa mfano ukatili wa baadhi ya wasaidizi wa ndani dhidi ya watoto tunaowaachia, nyuma ya historia ya maisha yao, kunakuwa na maumivu mengi Sana ... Hawajui kingine kuhusu kulea zaidi ya akili inamwambia piga...... Halafu tunakuja tena kulalamika na kusifiana eti sisi tulipigwa. Tunasahau hiyo spirit inabebwa na kusambaza Hadi kwa msaidizi wako, mke wako na mume wako. Halafu tunashangaa tena. Tunachopanda, ndiyo tutavuna.

Tarehe 24 x space tuna mjadala kuhusu sayansi ya malezi na makuzi na madhara ya hizi hatua za kupiga piga. Karibuni
 
Kuna watu ni makatili kuliko huyo lakini nikwambie binti yangu nilimwachishaga huko.Hao wamezidi
 
kuolewa sio mafanikio je huko kwenye ndoa mambo yanaenda???

Wajukuu zako watakuzwa kimaadili au kibroilabroila kesho wakifanikiwa kumaliza elimu zao kisha wakapangiwa kazi huko Nanjilinji wakashindwa kucope na mazingira kwasababu ya malezi mabovu.
Usipime malezi mazuri kwa mzani wa fimbo.Wengine tumeishi bila hata kutishwa na kupigwa na tunaheshimu na kuheshimiwa na watu mbalimbali.
 
Uko sahihi mimi nakumbuka shule ya msingi nilipata hesabu 90,ila mwalimu wa hesabu aliniadhibu tena sawa na waliopata F kwasababu mimi nilikosa maswali marahisi nikapata magumuπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.Kwa kipindi kirefu nilimchukia sana yule mwalimu mpaka nilipokuja kuelewa alimaanisha nini kwa wakati ule.

Imagine kila alipokuwa akisahihisa paper za hesabu mimi alikuwa hakosi kunichapa kwasababu ya kukosa hesabu ndogondogo na kufaulu zile complicated.Ila ndo maisha leo naelewa kuwa alikuwa ananikumbusha kuzidisha umakini na kutochukulia mambo kwa wepesi hata kama unayamudu.
 
Usipime malezi mazuri kwa mzani wa fimbo.Wengine tumeishi bila hata kutishwa na kupigwa na tunaheshimu na kuheshimiwa na watu mbalimbali.
kwa mazingira yetu ya kiafrika yaliyojaa vurugu.Fimbo na ukali kidogo ni lazima kwa hawa watoto zetu lazivyo siku za mbeleni tutaanza kushikana uchawi.

πŸ“ŒπŸ“ŒWatoto zetu wanakulia katika mazingira ambayo yapo soo vunarable kiasi kwamba ukilegeza kidogo unampoteza huyo mtoto.
 
Alivyokuvua kaptula alikulawiti?acha kutetea upumbavu
 
THAT WAS UKATILI ULIOPINDUKIA,
 
Mbona sijaona ukatili wowote hapo? Alie toa post hii lazima atakuwa mzungu tena wa kike au diaspora.


Ustaadh yupo sahihi kabisa anawafundisha watoto discipline.

Sema alicho kosea tu ni kwenye hesabu wengine alikuwa anawapiga fimbo nane wengine fimbo nne, au zingine alikuwa hazihesabu anazifuta nini?
 
NOT THAT WAY SI AJABU HUYO KACHEELEWA NDIYO UNAWAPIGA WATOTO HIVYO
 
HAKUNA NJIA NYINGINE?
 
ASANTE MAMA YETU. LIMENIUMA SANA. UMRI ULE KUNA NAMNA YA KUWAADHIBU SIYO KWA MIKWAJU YA NGUVU MA MISURI VILE!
 
NOT THAT WAY SI AJABU HUYO KACHEELEWA NDIYO UNAWAPIGA WATOTO HIVYO
Sijamtetea mwalimu ila naongea kwa experience.

Kama umesomea hapa hapa Tanzania basi unajua mila na desturi za kitanzania( UVIVU NA UZEMBE).

Enzi zetu tupo shule mtu anajua saa moja kamili ndio muda wa kengele ya mstarini ila yeye anaamka saa kumi na mbili na dakika 55πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ akili za kiuanafunzi bila mboko na mwalimu kuliamsha huko mabwenini watu hawaendi paredi.

Kila siku mwalimu mkuu anaongea ila watu hawafati baada ya mboko na adhabu za nje na kukosa vipindi watu wakaanza kukaa kwenye mstari.Leo hii baadhi ya wale madoja ndio hawa wanatetea mtoto asiadhibiweπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Bila kujali kosa la hao watoto hiyo adhabu ni kubwa kwao.

Nawashangaa sana ninyi mnaofananisha dunia ya sasa na hiyo ya miaka ya tisini.

Mfano kosa la uchelewaji, hilo kosa kwa miaka yetu ya giza utakumbushwa kwa viboko, ila siku hizi kuna means nyingi unaweza kuelekezwa zikakufanya ukawahi kuamka/kuwahi jambo fulani.

Hao madogo wamechelewa, mtoto kama huyo kuchelewa madrasa mara nyingi huwa sio kosa lake, kuna mwingine hapo kabeba kapu kabisa ikiwa na maana aidha akitoka hapo au alikotoka huko kahemea ndio kaenda madrasa.

Hivi kweli unashindwa kuicontrol akili ya mtoto hadi umpige, mbona akili yake unaisoma chap tu na kupredict his/her next move.
 
HAKUNA NJIA NYINGINE?
Unavyosema hakuna njia nyengine unafurahisha sanaπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„

1.Je hao waalimu mmewaanda kuwa walimu???
2.Tunapenda miujiza bila kuandaa process ya kuifikia!!!

Ndomaana ninasema kwa mazingira yetu watoto wachapwe tu,,,,hakuna namna wachapwe!!!! Elimu ya kubembelezana wanaweza wazungu tu ila sisi weusi hatuwezi kwakua hatujajiandaa kufanya hayo.
 
Mzee hiyo clip ni ya madogo ambao hata miaka 10 hawana, hao magoja ndio sie ambao tulikua umri wa balehe. Na sio kua huko nyuma tulikua hatulimwi mboko, tulilimwa na tukazoea na tulikalili tukidakwa ni mboko then inaisha iyo.
 

Madam, ningeshauri suala hili waelekezwe Bakwata wadili nalo kwa sababu vinginevyo jamii inaweza kutafsiri kwamba serikali inaingilia masuala ya Imani. Kwa sababu kutoa adhabu kwa watoto walio fanya makosa mbalimbali ya kinidhamu ni sehemu ya mafundisho ya dini.

Ni hayo tuπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…